“Wema Sepetu Hajanifundisha Tabia Mbaya”- Diana Kimari

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimari amefunguka na kuweka wazi kuwa Msanii mwenzake Wema Sepetu hajambadilisha tabia kama wengi wanavyodai.

Siku za nyuma Wema na Diana walikuwa na ukaribu uliopitiliza na kusababisha maneno Mengi kuzungumzwa kwenye Mitandao ya kijamii ikiwemo tetesi za wawili hao kuwa kwenye mahusiano ya jinsia moja.

Katika Mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Diana alisema watu wengi wanahoji kuhusu ule ukaribu wake na Wema kuwa haukuwa wa kawaida, huku wengine wakiongeza kwamba alikuwa anasali lakini tangu alipoanza kuwa karibu na staa huyo ameacha kitu ambacho amesema hakina ukweli.

Unajua zamani nilikuwa naposti sana mambo ya kanisani kwenye akaunti yangu, lakini mambo yalikuja kubadilika baadaye nikaona hakuna umuhimu tena wa mimi kuendelea kuposti kila kitu changu mtandaoni, hivyo watu wakadhani nimeacha kusali kitu ambacho si kweli, kutoposti hivyo vitu haimaanishi kwamba nimeacha ulokole wangu.

Pia mimi ni mdogo sio mkubwa kihivyo kwa hiyo mpaka sasa bado nipo chini ya uangalizi wa wazazi wangu hata kipindi naishi kwa Wema wazazi wangu walikuwa wanajua, kwa hiyo hawatakubali wanione naharibikiwa wakati wao wapo hai, wananichunga sana yaani sijui nisemaje“.

 

Wema Afunguka Kudhulumiwa Milioni 64 na Mwanaume Aliyehaidi Kumuoa

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweza wazi kuwa amekuwa akipitia kipindi kigumu tangu alipoachana na aliyekuwa Mpenzi wake Patrick ambaye pia alimdhulumu milioni 64.

Wema Sepetu ameeleza kuwa ameanza upya maisha kutokana na misukosuko aliokutana nayo ya kutapeliwa shilingi milioni 64 na aliyemdanganya anataka kumuoa, Patrick Christopher ‘PCK’.

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa mwanaume huyo alimtapeli kiasi hicho cha fedha hivyo amejifunza kutokana na makosa na anamuomba Mungu asirudie tena kosa kama hilo lililotokea maana angekuwa ameshafanya vitu vingi vya maana ambavyo vingemsaidia kwenye maisha yake.

Nilipita kwenye kipindi kigumu sana jamani, nimerudi nyuma sana yaani kifupi naanza maisha upya na mpaka sasa siamini kile ambacho kilinitokea yaani kama mtu alinipumbaza sijui kwa nini ila kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ndiyo kosa”.

Wema ameweka wazi kuwa amekuwa hayupo kwenye mahusiano kwa miezi sita sasa na hataki mwanaume kwani yupo bize kujenga maisha yake.

 

Wema Sepetu- Nimekaa Bila Kufanya Mapenzi Kwa Miezi Sita

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa hajafanya mapenzi kwa muda miezi Sita sasa tangu amalize mahusiano yake ya mwisho.

Kama utakumbuka mahusiano ya mwisho ya Wema yalikuwa na kijana anayejulikana Kama PK lakini mahusiano hayo yaliishia vibaya na kusababisha Wema kuwa na kesi mahakamani.

Lakini pamoja na kesi kuendelea Lakini Wema Hivi sasa anaendelea vizuri na ameweka wazi kuwa hana Mpenzi na tangu sakata lake na PK yeye yupo single hana Mpenzi.

Hivi karibuni katika Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) alifanya mahojiano na vyombo vya habari na kujibu maswali mbalimbali kama ifuatavyo.

Swali no 1: VIPI MAHUSIANO?

“Niko ‘single’ tangu mwezi wa tisa mwaka jana, tena sija-du na mtu yeyote.S

Swali no 2: KUNA WANAUME WA­NAOKUFUATA?

“Wako wengi sana, yaani wengimno, mpaka daaah!

Swali no 3: UNAWEZAJE KUKAA SIN­GLE KWA MUDA WOTE HUO?

“Kuna muda mtu unaona bora upumzike masuala hayo, kama mimi nimechukua muda wa kuwa mwenyewe tu bila ya masuala hayo.K

“Ninaweza kujizuia, tena watu ambao wanaonizunguka na kunipenda wananipa furaha.

Source: Global Publishers:

Sio Kila Siku Apate Tuzo Wema, Tupate na Wasanii Wapya :-ESMA

Mwanadada Esma Platinumz alifungua usiku wa tuzo za SZIFF na kusema kuwa itakuwa inapendeza zaidi kama katika tuzo hizo angepatikana msanii wengine wa kupata tuzo lakini sio kila siku kusikia wasani  wale wale kama Wema Sepetu.

Esma alijibu hayo alipooulizwa ama anadhani wema anaweza kupata tuzo kwa usiku huo ndipo aliposema kuwa antegemea kuwa watapata wengine pia maana wenye vipaji wako wengi,

akiongea na waandishi Esma aliwajibu hivi”

sio kila siku tuzo apate wema tu , tunataka tupate na wasanii wengine wapya pia , sio kila siku tunakuja hapa tunaanza kusema tunategemea Wema Apate tuzo inakuwa Kama hakuna wasanii wengine wa Kupata hizo tuzo, inakuwa kama hakuna watu wengine wenye vipaji , kwaio tunapenda pia watokee na wengine wapate tuzo.

Hata hivyo icho ndicho kilichokuja kutokea baada ya tuzo kupatikana kwa sababu hakupata mwanadada wema sepetu hakupata tuzo hizo.

Wema Sepetu Akana Kuchapisha Picha Chafu Mtandaoni

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amekana kuchapisha video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa Machi 18, 2019.

Hatua hiyo inatokana na msanii huyo kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde na Wakili wa serikali, Glory Mwendi ambaye alianza kwa kumkubushia shitaka Wema.

Wakili Mwendi ameeleza kuwa mshitakiwa anaitwa Wema Isaack Sepetu(30), anamiliki akaunti yaInstagram ya Wema Sepetu na alirekodi video ya Ngono October 18,2018.

Hakimu Kasonde alimtaka Wakili Mwendi kueleza ama kudadavua hiyo video ya ngono ikoje ama ni kitendo gani kilichofanywa na Wema, ambapo alijibu kuwa video inamuonyesha Wema akinyonyana ndimi na mwanaume.

Ameeleza kuwa October 25, 2018 Maafisa wa TCRAwaliiona video hiyo na kuiripoti kituo cha Polisi Kijitonyama.

Baada ya kuripotiwa upelelezi ulianza na October 29, 2018 alikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi ambapo alihojiwa na kukana maelezo hayo kisha kufikishwa mahakamani November 1, 2018.

Katika maelezo hayo,Wema alikubari wasifu wake ikiwemo majina, anuani na umriwake huku akikana kurekodi na kuchapisha video hizo katika akaunti yake.Pia alikiri kukamatwa na kupelekwa Polisi.Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi March 18, 2019 kwa ajili ya kusikilizwa

Wema Akanusha Kukatwa Utumbo

Mwanadada Wema sepetu amefunguka na kukanusha taarifa zinazosambaa siku nyingi katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa alikwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuata utmbo ili kupunguza unene na uzito.

Hata hivyo maneno hayo yanakuja baada ya mwana dada wema sepetu kuoneana alipungua mwili kila siku kiasi kwamba mashabiki zae wamekuwa wakipata wasiwasi na afya yamsanii wao.

Wema anasema kuwa kitu kikubwa kilichomfanya kwenda nje ni kwa ajili ya kuangaika swala lake la kupata mtoto na hata alipoenda huku aliambiwa kuwa anatakiwa kupunguza mafuta ili aweze kupata  mtoto kwa sababu mara nyingi hata mafuta usababisha kukosa kupata mimba.

Wema anasema kuwa kinachomfanya akonde kila siku ni stress za hapa na pale lakini pia amekuwa akinywa dawa ambazo zinamsaidia kupunguza uzito  na kupunguza mafuta pia.

Utumbo wangu mimi sijawahi kukataam wala kupunguza, nilivyosafiri na kwenda India, nilienda kwa sababu ya tumbo langu lakini niliambiwa kuwa mara nyingi kukosa mtoto husababishwa na Mafuta.Hivyo nilipewa vidonge kwa ajili ya kupunguza mwili na mafuta.

Bodi Ya Filamu Yamfungulia Wema Sepetu

Bodi ya filamu Tanzania siku ya leo imetangaza kumfungulia Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu Baada ya kumkingia kwa miezi kadhaa na kujihusisha na Shughuli zozote za kisanaa.

Akitoa uamuzi huo mbele ya vyombo vya habari, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB),  Joyce Fissoo, amesema  Wema amefuata maelekezo aliyopewa na bodi hiyo kwa asilimia 75.

Hatujamfungulia sababu ya huruma, tumemfungulia sababu amefanya tuliyoagiza kwa zaidi ya asilimia 75“.

Mwaka jana mwezi wa kumi Bodi ya filamu ilitangaza kumfungia Wema na kujihusisha na Shughuli zozote za kisanaa Baada ya Msanii huyo kusambaza picha zake za utupu katika Mitandao ya kijamii.

Kabla ya kufungiwa, Wema aliomba msamaha kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambalo lilimuonyesha akiwa faragha na mwanamme anayesemekana ni raia wa Burundi, aliyedai kuwa ni mume wake mtarajiwa.

Kesi Ya Wema Sepetu Yazidi Kupamba Moto

Upelelezi wa kesi ya kusambaza video za ngono mtandaoni inayomkabili Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu umekamilika na yupo tayari kwa ajili ya Kusomewa mashtaka ya awali.

Akiwa mahakamani hapo Mwanasheria wa Serikali,  Glori Mwenda amesema,

Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na taarifa njema ni kwamba upelelezi wa shauri hili umekamilika, hivyo tunaomba tarehe  kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali, mshtakiwa huyu”.

Wema anatetewa na wakili, Ruben Simwanza, alifikishwa na katika kesi ya msingi anashtakiwa Oktoba 15, 2018 jijini Dar es Salaam.

Wema Sepetu anatuhumiwa kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wake wa kijamiii ambapo kupitia hatua hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 21, 2019 kumsomea maelezo ya awali.

Kesi ya Wema Kufikia Ukingoni

Mwanadada Wema Sepetu ambae amekuwa aikabiliwa na kesi ya kuchapisha picha na video chafu katika mitandao ya kijamii , amefika mahakami tena February 13 kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo imekuwa ikitajwa mahakamni kila siku na kusemwa kuwa uchunguzi haujakamilika , wapelelezi waliamuliwa kutakwa kufanya uchunguzi kwa haraka  kwa sababu kesi hiyo imekuwa ikitajwa bila kufanyiwa kazi kabisa.

hata hivyo , baaada ya kesi hiyo kusomwa tena siku ya february 13, Kesi hiyo ya Wema Sepetu itatakiwa kusomwa tena february 21 , hivyo kumalizika kwa haraka kamaitaanza kusoma.

Wema kuonekana kwenye CopsEnenmy

Mwanadada Wema Sepetu pamoja na kwamba wengi wanajua kuwa alikuwa katika adhabu ya muda mrefu kutokana na kufungiwa kutokufanya kazi yoyote ya sanaa, anaweza kurudi tena hewani na kuonekana katika video mpya ya CopsEnemy  ambayo pia kuna mkono wa zamaradi mketema.

Mwanadada Wema ambae kwa sasa amekuwa akitumikia kifungo chake kutoa chama cha wasanii wa filamu, anaweza kuonekana tena kwa sababu movie hiyo iliweza kuchezwa nae kabla hajapata adhabu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuinadi muvi hiyo, meneja wa Wema Sepetu  neema ndepanya anasema kuwa filamu hiyo inategemea kutoka hivi karibuni na wema atakuwepo kwa sababu haliweza kucheza kabla ya kupata adhabu.

Anasema kuwa , wema amekuwa akifata masharti yote ya adhabu na adhabu hiyo ambayo imekuwa imekuwa ya awamu tatu na wameshamaliza awamu mbili hivyo wanasubiri kumalizia kwa sasa.

Wema Sepetu: “Sijakatwa Utumbo, Nimekonda Kwa Mawazo”.

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu ameibuka na kuweka wazi kuwa yeye hajakonda Kwajili ya kukatwa utumbo kama inavyodaiwa bali amekonda kwa ajili ya mawazo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Wema kwa mara ya kwanza aliweka ‘plain’ kuwa kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

Watu nawashangaa sana, wanaona kukatwa utumbo ni kitu rahisi ee? Mimi nimekon­da kwa sababu ya mawazo makali niliyokuwa nayo na si vitu vingine maana nilikuwa kwenye wakati mgumu sana”.

Lakini pia Wema ameongeza kwa kusema kwamba, licha ya kupungua anaufurahia muonekano wake mpya kwani kuwa mnene zaidi nayo siyo poa.

Yaani hujui tu ninavyoufura­hia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa sio mzito tena na navaa nguo ambazo nataka na napendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo“.

 

Wema na Diamond Uso Kwa Uso Waishia Kukumbatiana (video)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekutana uso kwa uso na aliyekuwa Mpenzi Wake Wema Sepetu katika mkutano siku ya jana.

Diamond alikutana na Wema uso kwa uso katika mkutano uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda wakati anaongea na wasanii Mbali Mbali.

Diamond alionekana akisalimiana na Wema kwa Kumkumbatia kamaalivyo wakumbatia wasanii wengine mbali mbali waliokuwa katika ukumbi huo.

Kama utakumbuka mara ya mwisho Wema na Diamond walipoonekana wanakumbatiana mbele ya hadhara Zari alithibitisha kuwa Wema bado alikuwa anatembea na Mondi na hata kumtuhumu kwa kuvunja mahusiano yake na Diamond.

Hii ni video ambayo inawaonyesha Wema Diamond wakiwa wanakumbatiana:

Kesi Ya Wema Sepetu Yapigwa Kalenda Tena

Kwa Mara nyingine tena kesi ya staa wa Bongo movie Wema Sepetu imepigwa kalenda kwa kile kinachodaiwa kuwa upelelezi haujakamilika bado.

Wakili wa Serikali, Mosia Kaima kudai kuwa kesi ya Wema iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya kutajwa siku ya leo, upelelezi wake bado haujakamilika, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka kuhakikisha upelelezi wa kesi hiyo unakamilika kwa wakati.

Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Nataka upande wa mashtaka mkamilishe kwa wakati upelelezi ili kesi iweze kuendelea kwa sababu ni kesi ya muda mrefu tangu ifunguliwe mahakamani hapa Novemba mwaka jana na hadi sasa upelelezi bado?”.

Mbali na hayo Wakili wa Muigizaji huyo ameileza Mahakama kuwa kesi hiyo imeshatajwa mara nne mahakamani hapo huku upelelezi wake ukiwa bado haujakamilika.

Naomba upande wa mashtaka ujitahidi kukamilisha upelelezi kwa wakati kwa sababu shauri hili limeshatajwa kwa mara ya nne sasa, bila upelelezi wake kukamilika”.

Hakimu Kasonde ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 13, 2019 itakapotajwa tena na kuwataka upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wao kwa wakati.

Wema alifikishwa kwa mara ya kwanza Kisutu, Novemba Mosi, 2018 kujibu shtaka la kuachapisha video ya ngono na kuisambaza katika mtandao wa kijamii wa Instagram, kosa alilodaiwa kutenda Oktoba 15, 2018 .

Nimelipwa Milioni Saba Kufanya Shoo Bado Sijafulia- Wema Sepetu

Msanii wa filamu za Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kusema wazi kuw taarifa zinazosambaa kuwa amefulia hazina ukweli hata kidogo.

Wema Sepetu amekula shavu baada ya kualikwa kama mgeni rasmi kwenye Usiku wa Zanzibar Sweetheart utakaofanyika Zanzibar Beach Resort hivi karibuni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Wema alisema tayari ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni saba hivyo anamshukuru muandaaji wa tamasha hilo kwa kuona umuhimu wake na kwamba ametambua bado anapendwa.

Bado nina mashabiki wengi sana maana mpaka nimeweza kupata nafasi hii siyo mchezo, ninawashukuru sana waandaaji kunipa nafasi hiyo na hapo kila mmoja ataona muonekano wangu siku hiyo ya tarehe moja mwezi ujao”.

Kutokana na ukimya wake kwenye Mitandao ya kijamii imekuwa ikisemekana kuwa staa huyo amefulia na umaarufu Wake kuisha baada ya skendo yake iliyomchafua mwaka jana.

“Wema Bado Yupo Kifungoni”- Bodi Ya Filamu

Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo amesema msanii wa filamu, Wema Sepetu hajafunguliwa kujihusisha na masuala ya uigizaji kama inavyovumishwa mitandaoni.

Bodi ya filamu Tanzania imetoa tamko hilo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Baada ya tetesi kusambaa kwenye Mitandao ya kijamii kuwa Wema amemaliza adhabu yake.

Karibu mtendaji amesema kuwa endapo msanii huyo atafunguliwa Baraza hilo litaitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kulieleza jambo hilo na si kama inavyoelezwa kwenye mitandano ya kijamii.

Jamaninaombeni muachane na stori za mitandaoni, Wema bado yupo kifungoni na endapo itatokea akaruhusiwa kujihusisha na masuala ya uigizaji bodi itaitisha mkutano na wandishi wa habari na kila mtu atajua,”.

Wema Sepetu alipewa adhabu hiyo ya kufungiwa kujihusisha na kazi za sanaa mwaka jana Oktoba 26 baada ya kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu Apata Bahati Nyingine Ya Kuolewa

Msanii wa muziki wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amejikuta akipata bahati ya mtende Baada ya kijana mwingine ambaye anatajwa kuwa rubani kujitokeza kwa ajili ya kumuoa.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa rubani huyo anayekwenda kwa jina la Ham­dan Zakwani ‘Danzak’amejitosa kumuoa staa huyo ambaye ni Miss Tanzania 2006, kwa gharama yoyote.

Rafiki wa karibu wa Danzak ameliambia Gazeti hilo kuwa, siku nyingi Danzak alikuwa na ndoto za kufunga ndoa na staa huyo lakini hakupata muda wa kufanya hivyo kwa kuwa, alikuwa amebanwa na masomo.

Danzak alianza kumpenda Wema, kipindi kirefu sana na mara nyingi alikuwa akimfuatilia nyendo zake na kumpenda jinsi alivyo.

Baada ya kumaliza masuala yake ya kimasomo na kuajiriwa, ameamua kuja nyumbani kupumzi­ka kidogo na mimi nimekuwa kama mwenyeji wake, kwa sababu za­mani kabla hajawa rubani tuliwahi kufanya naye sanaa ya muziki”.

Gazeti la Ijumaa lilimsaka Wema ambaye hakutaka kauongelea Suala hilo Lakini Meneja Wake anayeitwa Neema Ndepanya amewataka wanaotaka kumuoa Wema waende nyumbani kwao kujieleza.