Kesi ya Wema Kuhairishwa Tena.

Kesi ya mwanadada Sema sepetu imehaishwa tena mpaka mwezi  ujao tarehe 12  ilipokuwa imetajwa na kusikilizwa tena leo katika mahakama ya kisutu.

Mwanadada Wema Sepetu anashitakiwa na TCRA kwa kosa a kuchapisha video chafu akiwa faragha na mpenzi wake  hapo siku za nyuma na wema amekuwa huru kwa dhamana kutokana na kesi hiyo.

Hata hivyo kesi hiyo bado inaonekana kumtesa Wema ukizingatia kuwa hana muda mrefu tangu amekuwa na ksei nyingine ya kukutwa na madawa ya kulevya.

 

Martin Kadinda Abeba Tuzo Ya Ubunifu Wa Mavazi

Mbunifu wa mavazi na aliyekuwa meneja wa muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu, Martin Kadinda amenyakua tuzo Kama mbunifu bora wa mavazi wa mwaka 2018.

Katika Usiku wa Maonyesho ya Mavazi ya Kiume yaliyofanyika Lagos nchini Nigeria siku ya Novemba 16, 2018, mbunifu wa mavazi maarufu Bongo, Martin Kadinda alijinyakulia tuzo hiyo kubwa na ya heshima.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Martin Kadinda aliandika:

To the World., Designer of The Year Africa?@themanawardsAfrica’s Designer of The Year 2018…!! ??Am Humbled. The World Is ReadY?

Shukurani Za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa Afya, akili na ubunifu…Shukrani kwa Wizara Ya Habari, michezo na Utamaduni Kupitia Basata.Shukurani za Dhati kwa Familia, mama Yangu, dada na kaka zangu.. wadogo zangu na ndugu zangu wote…@wemasepetu and Ur Amaizing Team wema and die Hard fans??????..MK empire with All the Love and Support always??My friends mnajijua.. cant mention all of you.. ila asante sana.

Las Vegas nawasahauje sasa????. Majirani zangu vipenzi sijawasahau.Nitamaliza wote ? My fans in Belgium, south africa, Holland, china, states and All of the World ?.

Martini alianza kujizolea umaarufu kwenye ulimwengu wa fashion miaka kadhaa iliyopita Baada ya kutoka na staili ya makoti ya single button ambayo ilivaliwa na mastaa wakubwa Kama Diamond Platnumz na Hemed PHD.

Nandy Adaiwa Kumnyakua Bwana Wa Wema

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Aibu’ Faustina Charles maarufu Kama Nandy amedaiwa kumchukua Mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano na muigizaji Wema Sepetu.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa Mwanaume mmoja anayejulikna Kama Rajabu ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza alikuwa ndio anamuweka Wema mjini lakini Baada ya skendo ya Wema na PCK kutokea inadaiwa bwana huyo alimtosa Wema na kuhamisha majeshi kwa Nandy.

Gazeti hilo linaendelea kuripoti kuwa mara tu baada ya mwanaume huyo kutua kwa Nandy alimpangishia nyumba Masaki jijini Dar na kumnunulia gari la kifahari aina ya BMW X 1 na pia siku ya birthday yake mwanaume alimwagia pesa chafu ukumbini.

https://www.instagram.com/p/Bp9dZByBMxh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=pqpdgwd4nx78

Baada ya tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Nandy ili kupata ukweli wake juu ya ishu ambapo alikana kabisa taarifa hizo na kukana kumjua jamaa huyo.

Mh! Waja wana mambo sana, kwanza niseme nashtuka wewe kuniambia mambo ya bwana wa Wema, mimi yule bwana alinipa kama milioni tano hivi nilipozihesabu na nilishangaa kwani sikuwa nikijua kuwa nitapewa pesa hizo lakini si mpenzi wangu, wala sijawahi kujua kama anatoka na Wema.

Ukweli ni kwamba nilimualika kwenye pati yangu akanipa pesa kama mlivyoona lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi na wala gari hili hajaninunulia yeye, mimi nimejinunulia mwenyewe kwa kazi zangu tu. Kuhusu nyumba nimepangishiwa na mpenzi wangu ambaye siwezi kumtaja kwa sasa ila ni mtu maarufu tu.

Lakini Nandy alipobanwa zaidi kuhusu jamaa huyo alisema:

Alinipigia simu na kuniambia kuwa anataka kufanya biashara na mimi, akaniambia atakuja Dar, huwezi kuamini alikuja Dar na ikawa ndio imefika siku ya sherehe yangu ya kuzaliwa, nikamualika kwa bahati nzuri akaja”.

 

 

Wema- Aunty Ndiye Rafiki Pekee Ambaye Hanichoki

Muigizaji wa filamu za Bongo movie Wema Sepetu amedai rafiki yake Aunty Ezekiel ndiye rafiki pekee ambaye amekuwa naye bega kwa bega Bila kuchoka katika hiko kipindi kigumu anachopitia.

Wiki chache zilizopita Wema Aliibua gumzo zito mara Baada ya kuachia video za faragha akiwa na mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii jambo lililomuingiza katika matatizo.

 

Wema Sepetu amefunguka na kudai rafiki yake wa kweli ni  Aunt Ezekiel kwani hajawahi kumchoka na kumtenga kama wafanyavyo wengine na kusisitiza kuwa kuwa ana marafiki wengi lakini baadhi ni wanafiki ila Aunt ana upendo wa kweli kwake.

Nimegundua kuwa rafiki wa kweli kwangu ni Aunt, amenipa faraja ya kweli kipindi chote cha matatizo, naamini ana upendo na mimi”.

Baada ya kuingia katika sakata hilo wasanii kadhaa walimgeuka na kutaka apewe adhabu ambayo itamfanya asirudie makosa hayo huku wengine wakiwa Upande wake.

Wema Adaiwa Kukimbia Nyumba, Majirani Wafurahi Kupunguziwa Kero.

Akiwa bado anakumbwa na majanga kibao, mwanadada wema sepetu ameripoti wakukimbia nyumba anyokaa kwa madai kuwa ameshindwa kueledelea kulipo kodi katika nyumba hiyo aliyokuwa akikaamaeneo ya salasala.

Gpl, lilipokua likiongea na watu wa karibu , majirani zake wanasema kuwa ni afadhali mwanadada huyo kuwa ameondoka katika mtaa huo kwa sababu amewapunguzia shida walizokuwa wakizipata kila mara.

Baada ya kutaka kuthibtisha habari hizo, GPL waliamua kwenda alipouwa akikaa wema na  hawakufanikiwa kukutana na Wema bali majiran zake ambapo moja ya majirani hao alisema kuwa ni kweli Wema alihama nyumba hiyo usiku wa jana yake mida ya saa mbili alipokuja na gari na kubeba kila kitu chake cha ndani.

Majirani hao wanasema kuwa wamefurahi sana kuhama kwa wema kwa sababu yeye pamoja na marafiki zake walikuwa ni watu wneye fujo na vurugu wakianza mtaa mzima unakuwa hauna amani, na hata serikali yao ya mtaa imefurahi kupungziwa kesi mtaani gapo.

Akizungumza na waandishi wa habari, mjumbe wa mtaa huo wa salasala ansema kuwa amekuwa akimfahamu wema lakini amekuwa akishangazwa sana na tabia zake na hata kulipokuwa kukitokea tatizo wema amekuwa hajihusishi na kitu chochote katika mtaa huo lakini pia hakupata taarifa za kuhama zaidi ya kuona vyombo kwenye gari likibeba vitu kutoka ndani.

Mjumbe huyo anasema kuwa hata alipohamia hakuwa amejitambulisha kwa uongozi owowte hivyo na wao hawakutaka kumfatilia sana kwa sababu hakufata utaratibu,lakini hata alipokuwa akifanya vurugu mara nyingi amekuwa akitumiwa ujumbe na hakuwahi kufika kwa mjumbe na hata mlango wake haukuwa ukifunguliwa zaidi ya kuongea na mlinzi katika kitobo getini.

Wema Sepetu Agoma Kushiriki Katika Maombi

Kuna tangazo lilikuwa likipita katika mitandao ya kijmii likielezea na kutoa taarifa kuwa mwanadada Wema sepetu atakuwepokatika moja ya makongamano ya dini lililokuwa likitegemewa kufanyika wikiendi hii katika kanisa moja  jijin dar.

Baada ya kusambaa sana kwa taarifa hzio, mwanadada wma sepetu ameibuka na kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa huo ni uongo kwa sababu hata tangazi hilo lilipotoka hakuna na taarifa nali lakini pia hawezi kufanya kitu kama hiko.

Wema anasema kuwa hata yeye amekuwa na shida nyingi ikiwemo kilio chake cha kupata mtoto lakini hawezi kwenda katika  mkesha usiokuwa na taarifa rasmi.

Akikanusha taarifa hizo katika ukurasa wake wa instagram, wema anasema kuwa amechukizwa sana na uwepo wa taarifa hizo ambazo yeye hakuwa na habari nazo hata kidogo na wala hakutoa rughusa ya jambo hilo.

Wema anasma kuwa amekuwa akisikia kuwa kuna watu wanajikusanya kwa ajili ya kumfanyia maombi na aliona kuwa hayo ni mapenzi ya dhati lakini swala la yeye kuwepo katika mikesha mbalimbali kwa dhumuni hilo ambalo wanalisema kwake yeye hakuwa na hizo habari kabisa.Wema anasema kuwa ni kweli kwa sasa amekuwa mgonjwa lakini hakuna ukweli wa kuwepo katika mikesha hiyo.

 

Jeshi la Polisi Wasisitiza Bado Wanamtafuta Mpenzi wa Wema.

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamesema wanamsaka mwanaume aliyeonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii Wema Sepetu.
Akizungumza leo Jumanne Novemba 6, 2018, Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo, Liberatus Sabas amesema polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata wanamfikisha mahakamani.
“Polisi tunaendelea kumtafuta huyu jamaa, hatujakata tamaa na ikiwa tutamkamata lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.
Amesema kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.
ikumbukwe kuwa mwanadada wema sepetu na PCK walikuwa katika mahaba mazito yaliyotikisa mitandao ya kijamii na hata kufiki ahatua ya kutangaza  kufunga ndoa hivi karibuni,lakini ghafla kulizuka kwa tafrani kubwa kati yao na kusambaa kwa picha chafu na hata mwanaume huyo kutuhumiwa kumdhulumu wema pesa.

Wakati Wengine Wakimsema Vibaya, Faraja Amfariji Wema.

wakati baadhi ya watu na hata wasanii wenzake wakimsema na wakitaka mwanadada Wema Sepetu achukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu pia, mwanadada   Faraja Nyarandu amefunguka na kuonekana kuguswa na yanayoendelea katika maisha a mwanadada wema na kumfariji kwa hili analolipitia kwa sasa.

Akiwa kama moja ya ma-miss waliopita na kufanikiwa sana lakini pia kujiweka mbali  na mambo yanayiweza kuchafua historia yake, faraja amaemuombea wema ujasiri na pia Mungu amuongoze  na kumtoa katika anayoyapitia.

Faraja aliandika ‘sote ni wakosefu mbele zake, I believe in the power of redemption, i beleieve in second chance, lets us forgive and  be forgiven, nimekuwaza kwa sauti mdogo wangu wema ,Mungu atupe neema zake.”

Faraja na kundi lake la ma-miss miaka ya nyuma kidogo wamekuwa kundi bora la wanawake waliopitia katika ulimwende na kufanikiwa katika maisha yao na jamii zinazowazungiuka kwa ujumla huku watu wengi wakimpigia kelele wema kufuata mfano wao.

Mama Wema Aliwahi Kumchongea Wema kwa Hili.

Kama kutakuwa na kumbukumbu nzuri ya hapo nyua mama mzazi wa mwanadada Wema sepetu aliwahi kusikika katika vyombo vya habari akisema kuwa mtoto wake Wema sepetu amekuwa na tabia ya kuwafuga wanaume katika nyumba yake ambao wamekuwa na tabia za kike ( mashoga).

Hivi karibuni Mh Paul makonda ametangza kuwa wanaojulikana kuwa ni mashoga na wanaorekodi video za utupu wanatakiwa kuripotiwa na kukamatwa ili kukomesha tabia hiyo kabisa.

Akiongea na waandishi wa habari hapo awali mama wa mwanadada Wema sepetu aliwahi kusema kuwa amekuwa akichoshwa na tabia ya mtoto wake huyo ya kuwa akiwafuga wanaume wenye tabia chafu kaka hizo.

Hata hivyo iliwahi kusikika bila kuthibitika kuwa mwanadada wema sepetu aliwahi kuitwa polisi hivi karibuni kwa ajili ya mahojiano kutokana na sakata hilo la kufuga watu kama hao ambao kwa sasa wanataka kukomeshwa katika jamii yetu.

Na katika kuonyesha kuwa zoezi hilo linatiliwa mkazo, mh Paul Makonda alisema kuwa alishaanza kupokea mesji na simu nyingi zikiwataja wanaohusika na biashara hizo.

Rado Akiri Kumjua PCK kabla ya Kutangazwa na Wema.

Msani Rado amefunguka na kusema kuwa PCK kweli ni tapeli wa siku nyingi kabla hata hajaanza kuwa na mahusiano na wema ila wema aliingia kichwa kichwa katika mapenzi na mwanaume huyo.

Akiongea, Rado anasema kuwa yeye alimjua PCK baada ya kumtapeli rafiki yake mmoja na kwenda mpka akituo cha polisi ambapo baada ya kufuatilia waliambiwa kuwa mwanaume huyo amekuwa na tabia ya kuwapiga picha za uchi wanawake na kisha kuziweka katika mitandao ya kijamii.

Mahusiano ya Wema na PCK yamekuwa ya muda mfupi lakini yameleta madhara makubwa sana kwa dada huyo mpaka kufikia hatua ya kutapeliwa zaidi ya shilingi milioni 40 zilikuwa zikitegemewa na wema kwa ajili ya biashara  yake mpya ya hivi karibuni.

Inasemekna kuwa wawili hao walianza kujitangaza katika mitandao hasa baada ya video ya wawili hao ya kwanza kuvuja na ili kuwanyamazisha watu , Wema aliamua kuweka wazi kuwa huyo ndo future husband wake.

“Mitandao Ya Kijamii Inavuruga Wasanii”- MB Dogg

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva ambaye anahusika kwa kutengeneza vibao vikali kama vile ‘Latifah’ na ‘Ina Maana’ Mbwana Mohamed ‘Mb Dogg’ amefunguka na kuitupia lawama mitandao ya kijamii na kudai ndio imesababisha wasanii kuharibikiwa.

MB Dogg amefunguka hayo alpokuwa anaongelea baadhi ya matukio ambayo yamewakumba wasanii kadhaa kama Wema Sepetu na Amber Rutty wanaodaiwa kusambaza video zao chafu kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mb Dogg alisema anashukuru viongozi wamekuwa macho na kuchukua hatua lakini anachukia mitandao kwani imefanya watu wengi kuiga kwa kila wanachokiona.

Sisi watu weusi tuna njia zetu za kuishi sasa mitandao imetuletea ugeni na sisi hatuwezi kutumia, tukiona mtu fulani kafanya hivi basi tunaiga.

Basata watoe misingi vizuri, walianza na video ambazo zamani ilikuwa mguu ukionekana sawa lakini ukizidisha inawekwa kapuni, wakikaza kwa kutoa elimu kwa wasanii zaidi tunaweza kukaa kwenye laini vizuri na matukio kama haya yasitokee tena.”

Wema Sepetu na Amber Rutty wameshachuliwa hatua za kisheria kwani kila mmoja amekwisha fikishwa mahakamani na kesi zao tayari zinashughulikiwa.

 

 

Uwoya Afungukia Skendo Ya Dogo Janja na Wema Sepetu

Msanii wa filamu za Bongo movie mrembo Irene Uwoya amefungukia skendo ambayo ilikuwa inamkabili aliyekuwa mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Jnja na Bongo movie star Wema Sepetu.

Wiki chache zilizopita habari zilienea kuwa ndoa ya Uwoya na Dogo Janja imefika mwisho baada ya Dogo Janja  kubanjuka na Wema Sepetu wakati bado akiwa kwenye mahusiano na Irene Uwoya.

 

Katika mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi, Uwoya amesema kuwa, hakuwa na muda wa kuwauliza chochote kwa sababu wote ni watu wazima. Uwoya amesema hana mpango wowote wa kuongea chochote kuhusiana na madai hayo kwa sababu kama waliamua kufanya hivyo (kutoka kimapenzi) ina maana hawakuwa vichaa, bali waliamua na walikubaliana hivyo kwa upande wake hawezi kufanya chochote.

Unajua mimi nipo bize, ninafanya mambo yangu, halafu tena nitenge muda mwingine wa kuwahoji watu wazima wanaojitambua kuwa kwa nini waliamua kutembea na kufanya mapenzi? Kwangu mimi hapana kabisa… sina muda huo, wangekuwa hawana akili nzuri ningesema sawa, lakini ni watu wenye akili timamu kabisa”.

Lakini pia Uwoya ameweka wazi kuwa yeye aliishia kuwatazama tu ili aone mwisho wao utakavyokuwa hivyo anashukuru mambo yamekuwa hadharani kwani yeye ndiye alikuwa akionekana mkorofi siku zote.

Alisema katika hali kama hiyo yeye aliishia kuwatazama tu ili aone mwisho wao utakavyokuwa hivyo anashukuru mambo yamekuwa hadharani kwani yeye ndiye alikuwa akionekana mkorofi siku zote.

Niliamua kuwaangalia tu mpaka mwisho kwani nina vitu vingi vya kufanya ambavyo vinaniumiza sana kichwa changu”.

 

Wema Sepetu Aburuzwa Tena Mahakamani

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameonekana kushindwa kukaa mbali na mahakama kwani miezi michache baada ya kesi yake ya madawa ya kulevya kuisha  mrembo huyo amerudi kizimbani kwa kesi ya kusambaza picha chafu kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya jana Novemba 01, 2018  Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam baada ya kuburuzwa mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya Kusambaza picha za faragha mtandaoni.

Wema Sepetu alipata dhamana mahakamani hapo baada ya kukidhi vigezo, ambapo moja ya sharti lilikuwa ni kupata mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Milioni 10.

Sharti lingine alilopewa kwenye dhamana hiyo, ni kutoposti picha au video zenye maudhui ya ngono kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu akiwa mahakamani hapo amekana shtaka hiloo, na kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tena Novemba 20 mwaka huu.

Kajala Masanja Amkingia Kifua Wema

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Kajala Masanja ameibuka na kumkingia kifua msanii mwenzake Wema Sepetu baada ya kukosolewa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kusambaza picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.

Kajala ameibuka na kusema kuwa huu si wakati wa kushangilia kilichomtokea msanii mwenzake ambaye pia alikuwa rafiki yake wa karibu, Wema Sepetu bali inapaswa kumpa moyo na kuwa naye karibu.

Kwenye interview aliyofanya na Gazeti la Ijumaa kuhusu suala la kuvuja kwa video za Wema na mpenzi wake aitwaye Patrick Christopher ‘PCK’ wakiwa faragha, Kajala alisema kuwa kila binadamu anakosea kwa sababu hawezi kuwa mkamilifu katika maisha yake yote hivyo kukosea ni jambo la kawaida hivyo anampa moyo Wema, asijione mkosefu sana na kukata tamaa ya kuendelea kufanya kitu chochote.

Sioni kama ni sawa kila mmoja kumuona Wema kama ni mkosefu kupitiliza kwa sababu najua wazi hakuna aliye mkamilifu hata kidogo na siku zote kuteleza sio kuanguka ni wakati tu wa kumpa moyo na kuwa naye karibu”.

Tangu sakata hilo litokee baadhi ya wasanii ambao walikua marafiki wa Wema wamemgeuka na kutaka afungwe ili liwe fundisho mmoja wapo ni pamoja na Steve Nyerere na wasanii wengine kama vile Ray Kigosi, Esha Buheti na wengineo.

“Wema Awe Makini Kuna Watu Wanamuangalia”- Izzo B

Msanii wa muziki wa hip hop nchini anayetokea pande za Mbeya Izzo Business amefungukia sakata lianaloendelea hivi sasa na kushika headlines kwenye mitandao ya kijamii kumuhusu msanii wa maigizo nchini Wema Sepetu.

Wema Sepetu amefikishwa mahakani siku ya jana kwa tuhuma za kusambaza picha zake za faragha na mpenzi wake na kuziweka katika mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Ijumaa, Izzo Business ameibuka na kumshauri Wema kuwa mwangalifu katika siku za mbeleni kwani haileti picha nzuri hasa kwa yeye ambaye ni kioo cha jamii;

Naweza nikasema awe makini sana kutokana na pozisheni ambayo anayo kwa sababu yeye ni brand, anafahamika sana, kuna watu wengi ambao yeye ‘anawa-inspire’ na wengi wanamtazama yeye na kama unavyojua siku hizi kwenye mitandao hadi watoto wa chini ya miaka kumi na nane wapo na wanam-follow Wema kwa sababu wanatamani kuwa kama yeye. Kwa hiyo ushauri wangu ni vitu binafsi kama vile vibaki kuwa binafsi tu, kujirekodi hukatazwi, weka katika sehemu ya siri ili uangalie wewe, lakini siyo mpaka kuvitoa nje siyo kitu kizuri”.

 

Mtangazaji Wa Burundi Aongelea Utapeli wa PCK , Athibitisha kuwa PCK ndio Mvujisha video Za Wema

Moja ya watangazaji nchini burudni katika tv na radio ya rhema Fm amefunguka na kutoa ushaidi wa kuwahi kutapeliwa na mwanaume aliyewahi kusemekana kuwa ni mume mtarajiwa wa wema sepetu.

Mtangazaji huyo aliejulikana kwa jina la aveick anasema kuwa hata yeye aliwahi kuwa rafiki na PCK Kwa muda wa miaka miwili na walipanga kufanya kazi ya muziki pamoja kwa sababu PCK alimwambia kuwa yeye ni msanii na anaitaji promo nchi Burundi.

Aveick anasema kuwa baada ya muda alimuamini mwanaume huyo na hata kumtumia pesa kwa ajili ya kumnunulia simu nchini tanzania , simu ambayo aliipenda na PCK alimwambiakuwa na yeye anayo.

Hata hivyo mtangazaji huyo anasema kuwa PCK amekuwa tapeli kwa muda mrefu na wala sio mara ya kwanza kutapeli wanawake.

Aveick anasema kuwa hata picha na video za wema yeye ndio aliekuwa akiposti na kuzituma mitandaoni  na kwa naman moja amna nyingine wamekuwa wakimshuku kuwa mwanaume huyo kuna nguvu ya ziada amekuwa akitumia kuwarubuni wadada.