Wema Sepetu afika Mahakamani kusikiza kesi yake ya kosa la kukamatwa na bangi

Mrembo Wema Sepetu ambaye alikamatwa miezi kadhaa baada ya kupatikana na misokoto ya bangi nyumbani kwake alifika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuta mapema leo kuisikiza kesi yake.

Wema Sepetu alifika na mama yake, Mariam Sepetu na watuhumiwa wenzake wawili kuisikiza kesi na kulingana na ripoti mitandaoni, Wema Sepetu anasemekana kuwa amekana mashataka hayo na hivyo kesi yake kusogezwa mpaka tarehe 1 mwezi wa nane ambapo itaanza kusikilizwa.

Wema Sepetu (courtesy of Millard Ayo)

Kesi hii hata hivyo imekuwa ikisogezwa tangu miezi ya kwanza ya huu mwaka na bado Mahakama inadai kuwa wanamchunguza mrembo huyu huku wakiwapa mashabiki kiwewe kwani wanaona kuwa kesi hii imevutwa sana.

Wema atafikia mahakamani mwezi ujao kujua kitachotokea sasa.

Mrembo kweli kweli; Wema Sepetu atisha kwa picha mpya

Ingawa Wema Sepetu amekawia Kabla ya kuachia picha zozote mpya mrembo huyo hivi Leo amewaacha picha mpya ambayo imewazingua wengi.

Wema Sepetu aliwekaa picha hiyo Instagram na kulingana na maoni ya mashabiki wake, mrembo huyu kweli ameumbwa akaumbika.

Kwenye picha hiyo Wema aliandika kusema,

I am speechless laviemakeup… you killed with this look. They don’t just call you Ms Forbes for nothing… my dada your hands are magical. Yaani nikimaanisha zimetengenezwa kwa magic… you know there are good pictures and then once in a while you get stunning pictures and then in while you get stunning pictures, Jamani this is a stunning picture…Hata usipokubali basi hata kimoyo tu.

Tazama picha hiyo hapa;

Steve Nyerere asema asihusishwe na scandal ya audio ya Wema Sepetu

Rafiki wa karibu wa Wema Sepetu amefunguka kudai kuwa hataki watanzania wamuhusishe na audio ambayo Mrembo huyo anasikika akiongea na Mbowe.

Steve Nyerere ambaye ni mchekeshaji anayejulikana sana Afrika Mashariki alitaka Watanzania wajue kwamba hawezi kumfanyia rafiki wake wa karibu jambo kama hilo alipokuwa akizungumza na Bongo 5. Steve alisema,

“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile, Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,”

Mbowe hata hivyo amekana kuwa sauti hiyo sio yake lakini kwa sasa watalaamu wanafanya uchunguzi kujua nani aliyesambaza audio hiyo.

Mbowe aeleza mahusiano yake na Wema Sepetu

Freeman Mbowe ambaye ni kwenye kitu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu baada ya clip ya sauti inayosambaa mitandaoni.

Freeman amekana kutoka kimapenzi na kukana
clip hiyo. Kulingana na yeye hakuna kitu kinachoendelea Kati yake na Wema Sepetu. Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds FM alisema,

“Kitu ambacho naweza kukisema kwa sasa hizo taarifa sio za kweli na timu yangu ya mtandao inajaribu kufuatilia kujua, na ukweli utajulikana muda sio mrefu.”

Hata hivyo alikataa kuzugumzia clip hiyo kwa kudai kuwa hawezi kusema nani alizindua audio hiyo…aliendelea kwa kusema

“Hapana yule ni kiongozi wa kijamii kwa maana kwamba ni mwanachama wetu aliyejiunga na chama chetu, na wapo wanawake, wasichana, wapo watu wengi kwenye chama chetu ni kwamba kuna mahusiano si kweli ni taarifa tu za upotoshaji.”

Gigy Money amchana Wema Sepetu kwa Kumuita Fake woman

Hakuna anayejua kilichotokea katikati ya Gigy Money na Wema Sepetu lakini kuna fununu kuwa wawili hawa hawapatani hata kidogo. Hapo mbeleni wengi walijua kuwa Gigy Money anatani kuwa kama Wema Sepetu lakini kwa sasa mambo yamebadilika.

Model huyu wa video za Bongo hivi karibuni alifunguka kudai kuwa Wema Sepetu ni mtu fake na anataka kuwajulisha watu ambao bado hawajapata nafasi ya kumuona live. Akizungumza na Bongo 5 Gigy Money alisema,

“Wema ni mtu ambaye she is fake, Yaah! She is fake. Ukimuona WQema hivi live na ukimuona mtandaoni unaweza ukavurugwa, watu wengi ambao hawajawahi kumuona Wema hivi live wanachanganyikiwa, sio kama mimi sasa hivi. Mimi nilikuwa navurugwa magazeti kila siku nikiensda shule napitia Wema kafanya nini? Sasa hivi naishi hayo maisha sasa huwezi kuniambia Wema she is real. Mimi naishi hayo maisha by real sasa ndio maana kwake inakuwa changamoto, atafanya nini. Mimi ni changamoto kubwa sana kwa kila mtu ambaye yupo kwenye industry hii, maana sasa hivi unaweza ukaenda kwenye interview ukamfanyia msichana anayekuja interview akamtaja Gigy from nowhere pia. Mimi sifanyi kwaajili nashindana, nafanya kwa ajili yangu.”

Aliongeza kwa kusema kwamba walipokutana kwenye birthday ya Sallam, Wema Sepetu alinuna baada ya kumuona akikatika na Diamond Platnumz. Aliendelea kwa kusema

“Last time nimekutana naye hawezi kupiga stori na mimi tena, nimekutana naye kwenye birthday ya Sallam, nilicheza sana lakini nilikuwa ba bae Dangote. Alumina kweli na alikuwa ananiangalia vibaya lakini unajua ni mtu ambaye alishakuwa inspiration kwangu kwa hiyo siwezi kuonyesha action yoyote kwangu na kiukweli am the first person nilimwambia umependeza, wakati anaingia, am real. Ni kweli alivaa kizamani na umbo lake lilivyokubwa mashallah, alipendeza lakini nilivyopingia ndani tena sasa nilivyoitwa na Dangote kisa kuna Wema tena, niacheni kidogo siwezi kuvumilia. Sasa nikawa nacheza mimi na Dangote akawa ananiangalia mimi,”

Huyu ndiye mpenzi mpya wa Idris Sultan? (Picha)

Idris Sultan ameweka picha mpya ya mrembo ambaye hajukikani ni nani hata hivyo mchekeshaji huyu hakuwapa mashabiki wake nafasi ya kuwacha maoni yao baada yake kufunga comment section yake.

Hata hivyo hakuna anayejua ikiwa wawili hawa wanauhusiano ama ikiwa ni project yake mpya anayoitafutia kiki kwa kutowapa watu nafasi ya kuacha maoni yao.

Kwa sasa hatuna majibu ya maswali ambayo mashabiki wao wanauliza lakini imekuwa muda tangu Idris Sultan kuonekana na mrembo yeyote baada yake kuachana na Wema Sepetu. Hata hivyo kuna fununu mitandaoni kwamba wawili hao bado wanapendana lakini wameamua kuyaweka maisha yao kama Siri.

Tazama picha hiyo yake mpya hapa chino:

Huu ndio ujumbe ambao Davido alimwandikia Wema Sepetu

Msanii kutoka Nigeria Davido amewaacha wengi wakiongea baada ya kuacha maoni yake chini ya picha moja ya Wema Sepetu hivi karibuni. Muimbaji huyu ambaye amefanya kazi na wasanii kadhaa kutoka Afrika mmoja wao akiwa Diamond Platnumz amewaonyesha wengi kuwa anaweza kuwa anamtamani Sepetu baada ya ujumbe wake.

Wema
Wema Sepetu

Davido kama shabiki wa Wema aliweza kumfurahisha Malkia huyu wa filamu baada ya kumsifu kwa maneno yaliyodhibitisha kuwa mrembo huyu anadhamani ya juu. Aliandika kusema,

Hii inakuja baada Wema Sepetu aliwaambia mashabiki wake wamuombee apate mtu mzuri ambaye anaweza kutulia na yeye akiongezea kusema pia awe pia na hela za kutosha. Hata hivyo hakuna anayejua ikiwa wawili hawa huongea lakini ujumbe huo wa Davido umekuthibitisha kuwa Wema Sepetu ni mwanamke anayetambulika na wengi.

“Mimi simtaki Naseeb tena!” Wema Sepetu amwambia shabiki wake Instagram

Japo ni wengi bado hutarajia Wema Sepetu na Diamond Platnumz kurudiana, mrembo huyu ameweka wazi kuwa hamtamani Diamond tena na mapenzi yao yalikwisha kitambo sana.

Wema Sepetu alisema haya baada ya mmoja wa mashabiki wake aliandika kumuuliza iwapo ameshindwa kumpata Diamond Platnumz kupitia Instagram. Shabiki huyo aliandika kusema,

Wema Kwa uzuri huo umeshindwa kumkamata Diamond mpaka anakupa mawazo wanaume hawana lolote jitahidi

 

Kupitia tu Instagram Wema pia yeye alimpa shahidi huyo jibu ambalo lilidhibitisha kuwa mrembo huyu ameyaacha maisha yake ya kitambo na hivi sasa anatarajia mwanaume ambaye atamchukua alivyo. Wema aliandika kusema,

@Veronikakihonga Sasa baby alokwambia mi namtaka Diamond ni nani…?Life has to go on… Yule ni baba wa watoto wawili Jamani… Its about time u guys accept that me and Naseeb are no more. Mnachotakiwa ni kuniombua ni nipate mwanaume Bora na sio Bora mwanaume…Mwenye heshima zake tena ambaye hata haijulikani…Kajisemea dada angu @mangekimambi…mwenye hela miiingi

Wema Sepetu na Diamond Platnumz washerekea pamoja katika party ya Sallam

Waliokuwa wapenzi Diamond Platnumz na Wema Sepetu jana uikutana katika sherehe ya kuzaliwa ya Meneja wa Diamond Sallam Sharaff.

Sherehe hii ambayo ilifanyika Castle Lite iliwavutia wasanii kadhaa ambao walijitokeza kama wamevaa mavazi ya kizamani huku ikiwakutanisha Wema na Diamond Platnumz.

Ingawa wawili hawa hawajaonekana wakiwa pamoja katika picha ambazo zinasambaa mitandaoni, wengi wameachwa wakijiuliza ikiwa walipata nafasi ya kuongea kwani hii ndio mara ya kwanza kwa wiwili hawa kuwa katika sherehe moja tangu kuachana mwaka wa 2015.

Hata hivyo Wema Sepetu alionekana kurembeka kwa mavazi yake na mapambo yake ya kawaida.Tazama picha yake hapa.

Wema Sepetu katika party ya Mendez

Wema Sepetu awazingua wengi na picha mpya, ni kweli ameumbwa akaumbika!

Mrembo wa Tanzania Wema Sepetu amewapa mashabiki wake kitu kipya cha kuongelea baada ya kuachia picha zake mpya kupitia mtandao wake wa instagram.

Picha hizi zimekuja baada ya Wema Sepetu kwenda kimya kwa muda mrefu lakini kulingana na maoni walioacha wafuasi wake inaonekana kuwa bado wanampenda muigizaji huyu.

Ingawa pia hakuwachia picha nyingi kama anayvopenda, Wema Sepetu alihakikisha kuwa mashabiki wake wana sababu ya kuongea mitandaoni.

Tazama picha hizo hapa chini na utoe maoni yako.

Gabo afunguka kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu

Baada ya Wema Sepetu kuachia picha za kimapenzi akiwa na Gabo Zigamba, wengi hivi sasa wanaamini kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi kitu ambacho Gabo amekana.

Gabo Zigamba pia amekuwa akizipata habari ambazo zinadai kuwa hivi sasa anamchumbia wema lakini kwa mara ya kwanza ameweza kufunguka kuhusu uhusiano wao. Muigizaji huyu amefunguka kwa kusema kuwa picha zake na Wema Sepetu ni za kikazi wala sio kimapenzi.

Alisema kuwa picha hizi zinaonekana kuwa zakimahaba kwa sababu hivi karibuni wanapanga kuachia movie itwayo Heaventsent ambayo inazungumzia mapenzi. Alisema,

“Movie tunayoifanya na Wema iko very tomantic ndio maana hata picha zenyewe lazima ziwe hivo sasa watanzania naona wao washarasimisha kwamba kuna kitu kinaendelea kumbe hakuna pale tupo kazini na niwaahidi mashabiki zangu naanda kitu kikali sana mara mbili za jinsi wanavyonifahamu.”

Muigizaji huyu amesema haya wiki kadhaa baada ya Wema Sepetu pia kukana mahusiano yake na Gabo.

Kesi ya Wema Sepetu ya hairishwa baada ya upelelezi kukamilika

Jumanne hii Wema Sepetu na wakili wake waliweza kufika kotini kuskiza kesi ya malkia huyu wa filamu miezi miwili baada ya kusemekana anatumia dawa za kulevya.

Wema Sepetu aliweza kufika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam, ambapo hakimu mkuu aliwajulisha kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa umekamilika na mrembo huyo sasa amebaki kusomewa mashtaka baada ya kupatikana na msokoto wa bangi nyumbani kwake.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, alisema kesi hiyo itaskizwa June 1, ambapo Wema Sepetu ataweza kujibu mashtaka yake kwa mara ya kwanza.

Wakili wa mrembo huyu hata hivyo akona imani kuwa watashinda kesi hii.

Muigizaji wa Bongo Zuberi Mohammed adai Wema Sepetu, Uwoya na wengine hawafikii uzuri wa mke wake

Mwanaume ni kujiamini na muigizaji wa Bongo Zuberi Mohammed anaejulikana kama Niva amefunguka kwa kusema kuwa mke wake anauzuri ambao Uwoya, Wema na Kajala hawana.

Wema Sepetu

Akiongea katika interview, muigizaji huyu hakuogopa kwa kuwachana warembo hawa ambao wamekuwa kwenye sekta ya burudani kwa muda sasa. Kulingana na yeye, alibarikiwa na mwanamke ambaye anauzuri ambao bado hajauona katika mwanamke mwingine.

“Nakuambia ukweli kabisa hakuna mwanamke mzuri Bongo Muvi zaidi ya mke wangu Maisala, wewe muamshe usingizini Uwoya, Wema, Kajala halafu muamshe na mke wangu uone nani anavutia zaidi, hakuna kama mke wangu,”

Uwoya
Uwoya

Jibu hili lake lilikuwa la kuwapasha watu ambao wamekuwa wanaosema eti anauwezo wa kumsaliti mkewe kwani kila wakati anaonekana akitembea na wasanii wa Bongo Muvi wakati alifunguka ndoa na nia ya kutulia na kuanza familia.

Tazama picha za ‘pacha’ wake Wema Sepetu

Inasemekana kila mtu duniani anafanana na mwingine japo hawana uhusiano wowote kijamii.
Wakati mwingi,mtu hutupiwa picha akaambiwa,’angalia mbona huyu mnafanana?’

Wema Sepetu
Wema Sepetu

Na sio jambo geni,imetokea mara nyingi hata hapa Tanzania,ila, mrembo Lisa Deedee aka `Tuerny’ amejipatia umaarufu baada ya kusemekana kuwa ni pacha wa kipenzi cha wengi Tanzania,Wema Sepetu,unakubali,hasa huo mwanya?

Tuerny
Tuerny

Tuerny anasema,’Nakumbuka mwaka 2012 niliweka picha mtandaoni, mama akanitumia sms kwamba ninafanana na Wema, nilishtuka lakini tangu hapo akawa kama amebariki hicho kitu. Nilishangaa kila sehemu niliyokwenda watu wananiambia nafanana na Wema.’

Tuerny msichana anayefanana na Wema Sepetu
Tuerny msichana anayefanana na Wema Sepetu

Mrembo huyu amesema kuwa,hajawahi kukutana na Wema ila hapo nyuma watu walipoanza kunifananisha naye, alifurahi akawa ana-comment kwenye picha zake kwenye mtandao wa Instagram.

Kipindi hicho,akawa ananisifia naye anamjibu, lakini kutokana na maneno ya watu kama ilivyo kawaida ya wabongo na issue ya kutoleana povu,akachukia na kunipotezea…Tuerny amedai.

Picha Hizi ni Ishara tosha kuwa Wema Sepetu ni Binti Mrembo Zaidi Tanzania

Ingawa ni mwanamke ambaye amekuwa na scandals mingi, ni kweli kuwa Wema Sepetu ni binti ambaye ameumbwa kama malkia na ambaye anatambulika Afrika Mashariki na wengi.

Alipoanza career yake kama model sio wengi walidhania kwamba binti huyu angeleta mabadiliko mengi katika burudani ya Bongo. Wema Sepetu si model tu bali mwigizaji na kwa hivi mwanasiasa.

Hata hivyo, yeye ni fashion killa na mwanamke ambaye anajitambua. Akitembea mitaani watu wengi huduwaa kutokana na urembo alionao.

Nimeweza kupata picha kadhaa kama mfano kuonyesha mbona Binti huyu anaurembo watu wengi hutamani. Ingawa hukubaliani na mimi, pia ni sawa kila mtu ana maoni yake. Tazama picha hizi hapa.