Wolper akumbwa na haya baada kuonyesha uso wa mpenzi wake

Wolper ambaye anatoka na kijana amayeaminika kuwa Mudigi wake ameanza kuchambuliwa na mashabiki ambao wanamtambua.

Ingawa wameamua kutoficha mapenzi yao, kuna tatizo kwani picha moja ya Brown imeachiwa kwenye mitandaoni akionekana na mwanaume mwenzake na hivi sasa watu wanadai kuwa Brown amewai kuwa na mpenzi wa jinsia moja.

Mpenzi mpya wa Wolper, Brown

Ingawa hakuna dhibitisho tosha kuhusu picha hiyo, wengi bado wajiuliza maswali kwani Brown na huyo mwanaume huyo wanaonekana wakiwa katika pozi kitandani.

Hata hivyo Brown na Wolper hawajazungumzia jambo hili…lakini tunatarajia kuyasikia maoni yao. Tazama picha hiyo hapa;

Wolper adhibitisha kuwa kijana huyu ndiye mpenzi wake mpya! (Picha)

Baada ya kutemana na Harmonize, Wolper anaonekana ashapata mpenzi mpya na kulingana na ubuyu….mrembo huyu anatoka na kijana mdogo na pia ni mrembo kumliko Harmonize.

Hata hivyo Wolper amedhibitisha kuwa kwa sasa anatoka kimapenzi na mwanaume anayetambulika kama Brown. Akizungumza na Wikendi ya Global publishers. Mazungumzo yao yalienda hivi;

Wikienda: Kwa hiyo ni kweli Brown ndiye mpenzi wako kwa sasa?
Wolper: Ndiyo. Kwani kuna sababu gani ya kuficha? Awali hakuna mtu aliyejua lakini kwa sasa tuna muda kama miezi miwili, naona watu ndiyo wanajua sasa hivi.

Wikienda: Je, kweli kwamba unafanya hivyo kumkomoa Harmonize kwa vile inasemekana naye ana mwanamke mjamzito wa Kizungu?
Wolper: Aaah! Wapi! Ili iweje sasa? Kila mtu ana maisha yake jamani.

Wikienda: Je, huyo Brown ni nani au ana wasifu gani?
Wolper: Ndiyo kwanza watu wanaanza kumfahamu, wasijali watamjua tu.

Wikienda: Inasemekana umemzidi umri kama ilivyokuwa kwa Harmonize, je, ni kweli unapenda vijana wadogo?
Wolper: Nani kasema mdogo? Hebu watu waniache nitulize mawazo miye!

Tazama picha hiyo hapa;