Swala la Kuolewa Silipi Kipaumbele Sana:-Wolper

Msanii wa bongo movies na mjasiriamali maarufu , Wolper amefunguka na kuweka wazi swala la yeye kuolewa kwa sasa kutokana na watu kuwa wanahoji na kusema sana kuhusu swala hilo huku wakishangaa ni  kwa sababu gani  amekuwa na msululu wa wanaume wengi lakini haonyeshi dalili ya kuolewa hata kidogo.

Wolper anasema kuwa pamoja na yote lakini swala la kuolewa kwake sio la muhimu sana kwa sasa kwa sababu ameumizwa sana na mapenzi na hana haja ya kuyaendekeza  kwa sasa.

Kwenye mapenzi silipi kipaumbele sana swala la kuolewa kwa sababu nilishaumizwa sana huku mwanzoni, lkaini naomba huyu wa sasa niweze kumfikiri sana kuhusu swala la kuolewa kwa sababu nataka nimpende sana kuliko wanaume wote niliowahi kuwa nao.

Hapo awali Wolper alikuwa katika penzi zito sana na msanii Harmonize na kusemwa kuwa wawili hao hawawezi kauchana hata siku moja lakini baadae mapenzi yalikuja kuwashinda.

 

 

Ndoto Yangu ni Kutoka na Rais :-Wolper

Mwanadada wolper amefunguka na kusema kuwa amekuwa na ndoto ya kutoka kimapenzi na moja ya maraisi wa afrika kwa sababu anaamini kuwa hao watakuwa wakimuheshimu kama mwanamke mwenye hadhi yake lakini sio hawa wanaume wa kawaida.

Wolper anamini kuwa kutoka kimapenzi  na rais haitampa maumivu ya kutendwa kama ambavyo amekuwa akitendwa na wanaume wengine ambao kwanza hawajui thamani yake katika mapenzi.

Unajua ndoto yangu ni kutoa penzi langu kwa raisi yoyote Africa maana najua hao kwanza  atakuwa ananiheshimu sana  kutenda kama wanavyofanya wengine haitakuwa raisi, na hapo nitatulia kabisa wala sitatafuta wanaume waigizaji.

Wolper ambae amekuwa akiumizwa na mapenzi mara nyingi anasema kuwa kwa sasa anaamini kuwa hiyo ndio njia itakayo mpa amanai na wala sio vinginevyo.

 

Wolper Ajiita Bossy Lady, Akataa Kufananishwa na Mwanamke Yoyote Afrika.

Mwanadada Wolper Jackilne amejitangaza kuwa kwa sasa na yeye ni bossy lady ingawa hapo awali hakuwahi kujiita hivyo lakini kwa sasa anweza kujitangaza kama bossy lady.

Akiongea na waandishi kaika birthday party ya Jux, Wolper anasema kuwa kwa sasa ana bwana ambae anamuwekea pesa katika akaunti yake kila siku.

Lakini pia pamoja na ktajiwa baadhi ya wanawake mabao wamekuwa wakijulikana matajiri, wolpr amekataa kufananishwa na  mwanamke yoyote kwa sababu wanawake wenye pesa kwa anavyojua yeye huwa hawajitangazi kabisa kama wana pesa katika mitandao.

mimi zamani nilikuwa sio bossy lady lakini sasa hivi, nina mwanaume ananiwekea pesa katika akaunti yangu kila siku. mimi  ninaweza kujihita kama bosssy lady lakini sipendwi kufananishwa na mwanamke yoyote afrika, sio tanznia maana Tanzania usiniweke kabisa, kwa sababu wanawake wengi wa tanzania wenye pesa huwa hawaongei  wala hawajiweki katika mitandao.

Amber Ruty Amvaa Tena Jackline Wolper.

Mwanadada Amber Ruty amemvaa jackiline wolper na kuanza kumtolea kashfa mwanadada huyo kwa madai kuwa hawaendani hata kidogo wala hawawezi kulinganishwa kwa kitu chochote.

Amber Ruty ambae aliwahi kusikika mara ya kwanza baada ya kupiga picha za utupu na kuziweka katika mtandao wa kijamii na ndipo ackline wolper alipoamua kufunguka kukwera na tabia hizo huku akimtolea mfano mwanadada huyo.

Hata hivyo reaction ya Amber ruty baada ya wolper kumsema kwa tabia ya kupiga picha hzio za ajabu ikawa ni matusi an dharau pia.hata hivyo mwanadada huyoa likuwa ametulia kwa muda na sasa ameibuka tena na kumtukana tena Wolper.

Akiulizwa na waandishi wa habari kuhusu mwisho wa bifu lake na Wolper . Amber Rutty alijibu ‘niliamua tu kumpotezea nilimuona mshamba tu na alikuwa anatafuta kiki kupitia mimi.ni mshamba sana hana hadhi ya kugombana na mimi wala kunifatilia mimi namuona mshamba tu.”

Wolper Afunguka Maisha Mapya Baada ya Kuhamia Kenya.

Jacqueline Massawe ndilo jina alilopewa na wazazi wake alipozaliwa kule kwao Moshi mkoani Kilimanjaro, lakini wadau wa filamu Afrika Mashariki wanamtambua kama Jacqueline Wolper.

Kama umebahatika kutazama filamu zake kama Tom Boy au Dereva Taxi utamjua ni mwigizaji wa aina gani. Akiamua kuwa msichana mrembo katika filamu utapenda swaga zake, lakini pia akisema awe mwanamke nunda, utafurahi na roho yako.

Mrembo huyo ambaye amejikita pia katika ubunifu wa mavazi kwa sasa yuko nchini Kenya, amefanya mahojiano na Mwanachi kuhusu mambo mbalimbali ambayo wengi hawayajui tangu alipotua nchini humo.

Wolper anasema tangu ametua nchini Kenya anayafurahia maisha ya huko kwani toka ameingia hakuona mazingira kuwa magumu na anafanya kazi zake kwa utulivu. “Yaani pamoja na Nairobi ni mji wa starehe kwangu, ila ni mji ambao naweza kuishi kutokana na kuona mazingira ya utulivu yanayoweza kukusababishia ufikirie vitu vingi vya maisha bila ya kubugudhiwa,” anasema.

Wolper anasema kuwa Kitu kinachomtesa na kunipa stress kwenye kwenye mahusiano ni uongo na muda. Nafanya sana kazi lakini nahitaji muda wa kuwa na mtu wangu. Kwa hiyo uongo na muda ni tatizo sana kwenye mahusiano.
Mtu akianza kunidanganya au kunipa muda mchache wa kuwa naye na kuwa ‘out of mood’ kabisa na ninaweza nikaamka nikamwambia ‘it’s over’ bila kujali chochote.

Uongo ninaouhitaji mimi ni ule kunidanganya kuwa unanipenda, tangu nizaliwe sijawahi kuona mwanamke mzuri kama wewe. Huo ndio uongo unahitajika kwa kila mwanamke.

Mtu Anaeniita Kufanya Movie ni Lazima Anilipe Pesa Nyingi ili Kufidia Muda Wangu-Wolper

Mwanadada Jackline Wolper amefunguka na kuema kuwa pamoja na kwamba movie ndio kitu kilichomtambulisha katika tasnia lakini bado kwa aa anaona kuwa ni bora ajiingize zaidi katika kazi yake ya kushona kwa sababu anaona kuwa inalipa.

Wolper anasema kuwa sio kwamba yeye ni fundi lakini sio kwamba anajua kila kitu  kwaio hata  yeye pia ni mwanafunzi, kuna vitu anafanya na kukosea na kuna muda anaharibu vitambaa kwa kuvikata na kuvikosea hivyo bado anajifunza vitu vingi bado kwaio yeye ni fundi  mwanafunzi.

Akiongelea kuhusu maswala ya movie jackline anasema kuwa kwa ababu biashara yake kwa sasa imekuwa kidogo na kwamba anahitaji muda mwingi ana anahitaji kuifunza na kuwahudumia sana wateja wake kwaio ndio maana anaona kuwa ili mtu aweze kumpata kwa ajili ya kufanya movie  basi inabidi amlipe pesa nyingi sana ili kufidia ule muda mabao atakuwa ameupotza katika kufanya movies na sio kushona.

Ikumbukwe kwamba Wolper kabla ya kuamua kufanya kazi ya kuwa fundi cherehani ambacho ni kipaji  chake cha muda mrefu , alijulikana sana bongo kwa kuwa moja wa wasanii wa bongo movies waliokuwa wakifanya vizuri , lakini alipoona kuwa kuna kulega lega katika tasnia hiyo aliamua kurudi na kufanya kazi yake ya ufundi.

Wolper Aelezea Ukaribu Wake na Team ya WCB

Wiki iliyopita yalisambaa baadhi ya maneno yakisema kuwa Wolper amesema kuwa yeye sio shabiki wa WCB bali shabiki wa Diamond Platinumz tu, hii ikimaanisha kuwa hana mapenzi na wasanii wengine wa wcb zaidi ya bosi wa lebel hiyo.

Hata hivyo hivi karibuni Wolper alifunguka na kukanusha kuhusu maneno hayo na kusema kuwa watu waliomsikia walimuelewa vibaya kwa sababu si hivyo ambavyo wamefikiria ndivyo alivyomaanisha.Wolper anasema kuwa kwa mtu anaelewa mahusianao yake na WCB hawezi kutilia mashaka swala kama hilo au kufuatilia kwa undani maneno hayo.

Mtu akisikiliza kauli kama hiyo na ananijua mimi lazima atashangaa, mimi sio shabiki wa wcb, how? mimi nilijibu kutokana na swali nililokuwa nimeulizwa siku ile.kwaio watu wenye akili zao na wanaonielewa hawawezi kufatilia hivyo vitu.-Alisema Wolper.

Hata hivyo hivi karibuni Wolper alisema kuwa anacha kumsapoti msanii Harmonize ambae alikuwa mpenzi wake hapo zamani kutokana na wivu alio nao mpenzi mpya wa msanii huyo.

Wolper Kuitangaza Tanzania Kupitia Mavazi

Msanii wa maigizo na ujasiamali nchini, Jackline Wolper  anasema kuwa pamoja na kufanikiwa sana katika duka lake alilonalo la mavazi anatarajia kuanza kuitangaza tanzania kupitia kazi yake hiyo ya mavazi nje ya nchi.

Wolper ambae kwa sasa anamiliki duka la mavazi linalojulikana kama Wolper stylish  anasema kuwa anashukuru kuona biashara yake  sasa inafanya vizuri lakini pia anaona kuwa saa ndio muda wake wa kuanza kuitangaza baishara yake nje  Tanzania.

Najivunia sana kazi ninayoifanya kwa sasa,imekuwa ikinizalishia wateja kila kukicha, imefika kipindi sasa natamani sana  kufanya kazi nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda  na kwingine ili niweze kuitangaza  kupitia mavazi yangu ninayotengeneza.

Wolper anasema kuwa kipindi ananza biashara hiyo hakujuakabisa kama ataweza kufnaya biashara hiyo na kupata thamani kama ambavyo imekuwa ikimuingizia sasa, lakini kwa sasa anajipanga kuongeza kwanza maduka yake ya nguo nje ya Dar Es Salam ili kuwapatia pia wateja wake wa mikoani huduma yake.

Wolper Akana Kutambulisha Mwanaume Nyumbani

Mwanadada mkongwe kabisa katika tasnia ya filamu nchini ambae pia ni  mjasiriamali Jackline Wolper , amefunguka na kusema kuwa hajawahi kumtambulisha mwanaume yoyote nyumbani kwao kwa sababu alishaona kuwa hakuna ambae anasifa za kutambulishwa kwao au kumuoa yeye.

Mwanadada huyo ansema kuwa wanaume wengi aliokuwa nao ilikuwa ni kwa ajili ya kupeana starehe na kula raha lakini hakuwa na umakini wa kumpekleka nyumbani kwa sababu hawakuwa na sifa za kuwa wakwe.

Akionge na Global Online Tv, Jackline Wolper ambae alikuwa na usiku mzuri wa Stylish Night kwa ajili ya kuji-brand yeye na biashara yake alisema kuwa  pamoja na kwamba ameshapiata kiampenzi na wanaume wengi sana wa nje na ndani ya tasnia ya sanaa lakini hakuwahi kumpeleka mwanaume hata mmoja kwao kwa sababu walikuwa na lengo la kufanya starehe tu.

Sijaolewa na siajwahi kutolewa mahali wala kumtambulisha mtu, kwanini nimtambulishe mwanaume?

Akiendelea kuongea Wolper alisema kuwa anayoyafanya katika mitandao ni kwa sababu mama yake hayupo huko ila angekuwepo wala asingethubut.u

kwa kuwa nafanya vitu vya kijamii , najaribu kuepukana na baadhi yta mambo, mahusiano yangu mnayoyaona katika mitandao huwa ni ya kujifurahishga tu kwakweli na ndo maana mnaona nachiachia sana lakini endapo mama yangu angekuwa katika mitandao ya kijamii wala  nisingejaribu kufanya hivyo, lazima niwaheshimu wazazi wangu.

Hizi Ndo Sababu Watu Wanadai Kuwa Wolper Kaachana na Mpenzi Wake

Muuigizaji wa Bongo Movie na mrembo Jacqueline Wolper anadaiwa kuachana na Mpenzi wake Brown.

Habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zinasema kuwa Wolper na mpenzi wake wameachana kwa muda mfupi sasa.Huku hakuna hata mmoja kati yao aliyekataa au kuthibitisha habari hizo mpaka hivi sasa lakini kuna tetesi zinazoenea chini ya kapeti zinadai hivo.

Wolper kafuta picha zote za Brown kwenye ukurasa wake wa Instagram na Brown naye kafanya hivyo hivyo pia. Katika mapenzi yao wawili hao walikuwa watu wakupiga picha pamoja na kila mmoja kuziposti kwenye kurasa zao sasa ilipotokea siku mbili hizi kila mmoja kafuta picha za mwenzake ndipo watu walipoanza kuhidi kutakuwa kuhlna jambo linaendelea baina yao.

Pia sababu nyingine inayopekekea watu kuhisi wawili hao wameachana ni kitendo cha Wolper kuenda kwenye sherehe ya birthday ya Diamond ambapo alijua kabisa atakutana na mpenzi wake wazamani Harmonize na pia Wolper alienda kwenye sherehe hiyo mwenyewe bila Brown ambaye ni mpenzi wake na pia habari za udaku zinasema Wolper alionekana akipeana mkono na Harmonize.

Inasemekana kuwa Brown alikuwa amechora tattoo ya Wolper kifuani lakini kwa picha inayosambaa mtandaoni inaonyesha wazi kuwa amekwishaifuta tatoo hiyo ikimaanisha wameachana.

Je kutokana na sababu hizo unahisi kuna ukweli wowote wa Wolper na Brown kuachana?

Toa maoni yako tafadhali.

 

Kajala, Wolper na Harmonize Waingia Katika Bifu Zito

Mastaa wawili wa Bongo movies Kajala Masanja na Jacqueline Wolper wameingia katika bifu zito baada ya maongezi kwa njia ya video ‘video call’ baina ya Kajala na mpenzi wa zamani wa Wolper mwanamuziki Harmonize kuvuja mtandaoni na kuibua makubwa.

Kajala alikuwa akizungumza kwa njia hiyo ya kisasa na Harmonize ambae alionekana akila tunda aina ya apple kitandani kwake huku na Kajala akiwa kitandani kwake, baadaye Harmonize aliirusha picha hiyo mtandaoni na kusababisha minong’ono ya chini chini kusambaa. Picha ile ilimkera Wolper ambaye ametoka kuachana na Harmonize miezi si mingi na Kajala pia ni rafiki yake hivyo ilipelekea Wolper kuandika maneno yafuatayo kwenye picha ile: “Yaani nimekaa hapa mwenyewe nimewaza mapenzi ya siku hizi yana drama mno, mara leo huyu mara kesho yule”. Akijua wazi Kajala ameumizwa na kitendo hicho. 

Wema Sepetu naye aliingilia kati ishu hiyo na kuandika maneno chini ya picha hiyo “Be carefully my baby huyo nyakunyaku asije akapita maana keshaambiwa mlango uko wazi”. Maneno hayo yalionekana kumuuma Kajala ambaye mara moja alikimbilia mabatini kituo cha polisi kwenda kumshtaki Harmonize kwa kitendo chake cha kuweka picha hiyo mtandaoni na kuleta tafsiri kuwa huenda wawili hao ni wapenzi kitu ambacho sio cha kweli, na yeye amepewa RB No/ KJN/ 73/2017 Jalada la uchunguzi

Kajala amesema;

“Nimemshtaki Harmonize ili ajue mimi sio mtu wa mchezo  kila wakati, maana ile video tulikuwa tukizungumza kawaida kwa nini aisambaze ili iweje kama sio kuchafuana huko”.

Kajala aliongeza kuwa anawashangaa wasanii wenzake Wolper na Wema kuingilia vitu kama hivyo kwa sababu wanaona kama yeye ni wakula mizoga yao. “Mimi nashangaa hivi wamenionaje, wanafikiri mimi ni wakula  mizoga yao nini wanayoiacha, wamenishangaza sana”.

Harmonize aliwasili kituoni hapo na kwa mujibu wa chanzo kinachoaminika kutoka kituoni hapo, Mwanamuziki huyo alijitetea kuwa sio yeye aliyeweka picha hizo mtandaoni bali ni mwanamke wake wa kizungu ndo aliyemtumia mtu mwingine kwa nia ya kutaka kumjua Kajala.

Wolper Asema Mpenzi Wake Ni Wa Kimataifa

Muigizaji na mfanyabiashara wa mavazi nchini, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai kuwa hatamani kumuona mpenzi wake akifanya kazi zake za kimtindo “Modeling” ndani ya nchi kwa maana ameshaanza jitihada za kumtafutia kazi za kimataifa. Katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni Wolper amesema watu wanadai mpenzi wake ni mbeba poch lakini anachojua ni wivu ndiyo unawasumbua kwa sababu wanafahamu kazi anayofanya lakini kwa kuwa yeye anathamini kazi ya mpenzi wake huyo lazima atahakikisha anamvusha boda kwa kutumia mitandao aliyonayo:

“Kuna mtu anamuita ‘BFF’ mbeba pochi, najua anafahamu ni kazi gani anafanya lakini kwa kuwa anaumia lazima amchafue. Mpenzi wangu ni ‘Model’ ambaye ameshafanya kazi nyingi tu za kutembea kwenye majukwaa lakini si unajua sekta za mitindo hapa nyumbani? hazijapewa kipaumbele sana kwa hiyo mimi kwa kuwa tayari nina connection nje ntampigania kuona anafanya kimataifa zaidi na siyo nyumbani. Suala la kutumika kama video vixen hapa nyumbani sitaki hata kusikia kabisa wala kuona kwa sababu hakuna maslahi na mpaka sasa jiandaeni kuona deal za kazi kutoka South Africa tumeshasaini mikataba kwa hiyo mambo ni mazuri kwa upande wetu”.

Mbali na hayo Wolper amesema haogopi kumsaidia mpenzi wake kwa hofu ya kuja kusalitiwa mbeleni kwani anaamini  Mungu amempatia Brown kwa kuwa ana vigezo vyote anavyohitaji na hata ikitokea akamsaliti hatakuwa na shida kwani atakuwa daraja la mafanikio yake.

Wolper afungukia tetesi za yeye kutaka kumtolea mahari na kumuoa mpenzi wake

Baada ya tetesi kuenea mitandaoni kuwa Jackline Wolper anataka kumtolea mahari na kumuoa mpenzi wake “ben-ten”Brown ambaye ana umri mdogo kuliko yeye  Wolper ameibuka kupitia ukurasa wake wa instagram na kukana na kuzima habari hizo huku akidai kuwa yeye sio muhindi kwani wahindi wanawake ndo wanaoa wanaume.

Habari hizo zilienea baada ya gazeti la udaku kuripoti kuwa Wolper alidai wabongo wengi wamezoea kuona mwanaume ndiyo anatoa mahari na kuoa jambo ambalo kwake anaona ni utaratibu na uamuzi tu si dhambi mwanamke kumlipia mahari mwanaume. Wolper aliendelea kusema:

“Unajua watu wengi wanachukulia mahari ni lazima atoe mwanaume kitu ambacho siyo sahihi kabisa maana hata India siku zote  mwanamke ndiyo anatoa mahari na mimi nataka kuanzisha hiyo bongo. “Najua katika hili, watu wengi wataanza maneno maneno kuwa mimi ndo nimeoa lakini sitajali”.

Kupitia ukurasa wake wa instagram pamoja na kukana kuwa hataki kumuoa Brown kama magazeti ya udaku yalivyodai pia ametumia nafasi hiyo kuelezea hisia zake juu ya mpenzi wake huyo kuwa anampenda na na anapokuwa na yeye moyo wake unajawa na amani na furaha na kumuita mwana wa maisha yake.

Wolper alianza ku-date Brown miezi michache iliyopita baada ya kuachana na mpenzi wake wake wa siku nyingi mwanamuziki Harmonize.  Wolper na Brown walipata umaarufu mkubwa mtandaoni kutokana na umri mdogo wa Brown.

“Mimi Harmonize hawezi kuniacha” Wolper

Wolper alikuwa kwenye mtandao wa Central Filamu wiki hii ambapo alizungumzia uhusiano wake na Harmonize.

Alidai ya kwamba woko pamoja na hakuna ataye watenganisha.

“Wengi wanaongea sana kuhusu mpenzi wangu kama anatoka na wanawake wengi pengine inaweza kuwa ndio sababu ya kuniacha mimi hicho hakiwezekana wanaongea kama kuna wasichana wanajipendekeza watachezewa tu,” alisema Wolper.” Alisisitiza.

Hao wawili wamerudiana wiki kadhaa tu baada ya kusemekana wameachana.