Young Dee Aibukia Kwenye Gospel.

Mwanamuziki David Genzi maarufu kama Young Dee amefunguka na kuelezea ujio wake mpya wa nyibo yenye maadhi ya injili, wimbo ambao ameimba kwa ajili ya kumshukuru mungu kwa mambo aliyomtendea mpaka hapo alipofikia.

Young Dee anasema kuwa wimbo huo ambao atamuweka msanii mwenzake Ben pol utakuwa moja ya nyimbo za kusisimua kwa sababu uatkuwa na hadithi ya maisha yake halisi na mafanikio na mapito yake kwa ujumla.

Katika ukurasa wake wa instagram, Young dee aliandika stori ya mtu aliyeumwa kwa masaa manenane tu  lakini kutumia gharama ya zaidi ya milion 14 kwa ajili ya matibabu, hata hivyo anasema kuwa pamoja na yote mtu huyo alijua kuwa kama sio mungu basi wala pesa zake zisingekuwa kitu , hivyo kwa historia hiyo fupi aliyoiweka young dee katka ukurasa wake, mwishoni alimalizia kwa kusema

hapa mimi nawaza kuandika wimbo wa kumsifu mungu muweza wa yote,,aisee #amgrateful  ,,,oii @benpol niandalie chorus baller

Wasanii wengi sasa wameanza kutumia style hii ya kuingia katika muziki wa injili ya kufaya vitu tofauti ambavyo pamoja na kwamba wanamshukuru Mungu lakini pia inaleta radha mpya kwa mashabiki.

Young Dee Yuko Tayari Kwenda Mahakamani Kisa Meneja Wake

Msanii wa hip- hop nchi Young Dee amefunguka na kusema kuwa tangu ametoa wimbo wake wa naoa anafaya kazi yeye mwenyewe  bila kuwa na uongozi wowote kwa sababu alishaachana na uongozi uliokuwa ukimuongoza hapo awali.

Young dee ambae alitangaza kuwa kwa sasa anafungua kampuni yake mwenyewe hivyo kila kitu anachofanya atakuwa akisimamia yeye mwenyewe,.

Hata hivyo alikuwa akiongea na eNEws ta EATV ,YoungDee aliulizwa kuhusu swala la meneja wake huyo anaejulikana kwa jina la Sudi kutaka kwenda kumgungulia mashtaka kwa kile kinachodaiwa kuwa amevunja mkataba bila kufuata makubaliano yao.

Baada ya kuulizwa Young Dee alisema kuwa hata yeye yuko tayari kwenda mahakamni kwa sababu ya swala hilo kwa sababu anachojua ni kwamba walishamalizana siku nyingi.

Mimi nilishafuta kila kitu kisheria na  kuhusu mkataba kama anataka  kufanya chochote afate sheria maana mimi niko tayari hata kwenda mahakamani.

Young dee anasema kuwa alikuwa na malengo aliyokuwa amejiwekea lakini ilifika muda akaona kuwa itakuwa ngumu kuyafanikisha na kwa sababu yeye ni mwanaume na ana majukumu hakuona sababu ya kukaa hapo zaidi ya kupambana.

Young Dee Anyanganywa Gari na Uongozi Wake wa Zamani

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Young Dee amefuguka na kutoa siri kuwa ile gari ya gharama aliyowahi kununuliwa na uongozi wake aliokuwa akifanyanao kazi hana tena kutokana na kwamba kwa sasa yeye na uongozi huo hawafanyi kazi pamoja hivyo  wamechukua gari lao.

Young Dee ambae kwa sasa ametangaza kuwa na uongozi wa kwake mwenyewe na kwamba kwa sasa hana uongozi amekuwa akijiongoza mwenyewe anasema kwa sasa gari hilo hana tena .

Hata hivyo , young dee anasema kuwa anaamini kuwa mambo yake yatamuendea vizuri  ana mpango wa  kununua Lambogini.

Young Dee Akana Kuwahi Kuwa Kwenye Mahusiano na Amber Lulu

Msanii wa Bongo fleva Young Dee ameibuka na kumtolea maneno shombo aliyekuwa mpenzi wake Amber Lulu na kudai hajawahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi.

Wawili hao waliingia Kwenye bifu zito siku za hivi karibuni na kurushiana maneno mazito na matusi Kwenye mitandao ya kijamii.

Young Dee ameibuka na kuweka wazi kuwa hajawahi kuwa Kwenye Mahusiano na Amber Lulu yaani hajawahi kuwa girlfriend wake bali alikuwa ni mtu aliyekuwa yupo kwa ajili ya kukutana naye kimwili kila muda anaotaka.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Tv, Young Dee amefunguka haya:

Amber hajawahi kuwa girlfriend wangu alikuwa ni bootycall wale watu unawapigia sana kumi usiku tu sasa unamuitaje Ex girlfriend wangu wakati sijawahi hata kukutana naye mchana”.

NIlikuwa nakutana na Amber kipindi kile nakunywa makonyagi tu siku hizi nimeacha pombe sina sehemu za kuktana naye maaana sio level zangu”.

Amber Lulu aliweka wazi kuwa bifu lake na Young Dee lilianza mara baada ya Amber kukataa kuwa kwenye Mahusiano naye.

Young Dee Akana Kutoka Kimapenzi na Rosa Ree.

Msanii Young Dee amefunguka na kukanusha habari zinazosambaa kuhusu mahusiano yake na mwnadada Rosa Ree,Young dee anasema kua wamekuwa na uhusiano ya kufanya kazi kwa muda sasa kutokana na nyimbo yao mpya inayokuja hivi karibuni.

Young Dee anasema kuwa wamekuwa karib sana na Rosa kutokana na kazi na wala sio kitu kingine chochote kama wao wanavyosema.

Hatujawahi kuwa na mahusiano na rosa ree, kinachotukutanisha ni muziki tu na waa sio kingine, yeye ni rapa na mimi ni rapa, kwaio tunakutana kwa sababu ya kazi za muziki tu, ni kama mimi na wewe kinachotukutanisha ni kazi na wala hatuuiz vitumbua.- Aliongea young dee akiwa katika The playlist ya Times Fm.

 

 

Ndoa ya Young Dee Yayeyuka , Kumbe Ilikuwa Kiki.

Kulikuwa na picha zilizokuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii zikiomyesha kuwa msanii wa bongo flev, Young Dee amefunga ndoa na mwanamke mmoja inaeemekana kuwa sio wa nchini,maswali mengi yalitanda kutokana na ukimya na usiri wa ndoa hiyo.

Hata hivyo wengi walikuja kuamini kutokana na pongezi nyingi walizokuwa wakipewa  kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu hatua aliyoichukua ya kufunga ndoa na mwanamke huyo.

Ndoa hiyo imeota mbawa baada ya kuonekana kwa video  mpya ya Young Dee ya wimbo ulikwenda kwa jina la naoa ambapo picha hizo ni photoshots za wimbo huo.

Imekuwa ni jambo la kawaidia kwa wasanii kufanya kitu kikubwa kitakachowafanya mashabiki kukaa attention kumbe inakuwa ni kiki ya kutaka kutoa wimbo mpya, hiki alichofanya Young Dee pia walishafanya watu wengi katika game.

Young Dee Aukacha na Uongozi Wake.

msanii wa muziki wa rap  nchini young dee amefunguka na kusema kwa sasa amecahana na ule uongozi wake alikuwa chini yake hapo awali ana anategemea kuanza kufanya kazi pekee yake.Young dee anasema kuwa kwa sasa amefungua kampuni yake mwenyewe ambayo itakuwa ikisimamamia kazi zake za sanaa na kampuni hiyo itakuwa chini ya uongozi wake yeye mwenyewe.

Young dee anasema kuwa wiki ijayo atatoa wimbo wake mwenyewe , wimbo ambao ndip utakuwa wimbo wake wa kwanza kutoka katika kampuni yake ambayo ataanza kufanya nayo kazi kupitia wimbo huo unaokuja.

Wikiendi  hii pia kumekuwa na picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha msanii huyo akiwa na mwanamke pembeni yake huku wakiwa katika mazingira ya kufunga ndoa.

 

Picha za Young Dee akiwa na Vazi la Harusi Yaleta Utata.

Msanii wa bongo fleva nchini, David Kenzi , ameonekana katika mitandao ya kijamii akiwa na mwanamke pembeni yake huku wakiwa katika vaz la hshima , vazi la harusi huku ikisemekana wawili hao kuwa wamefunga ndoa.

Hata hivyo watu weng wamekuwa wakishangaa kutokana na kitendo hicho kufanyika kimya kimya na hakuna hata wasanii wengi waliokuwa wakijua swala hilo.Hata hivyo msanii huyo mwenyewe pia hakuweka wazi swala hilo , kitu amacho kimewaacha masgabiki katika mshangao wa kutaka kujua kama ni kiki ya muziki mpya unaokuja au ni kweli wamefunga ndoa na mrembo huyo.

Hata hivyo kumekuwa na pongezi kutoak kwa watumbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine ni vigumu kujua kama ni kiki kutokana na nyadhifa zao katika jamii, moja ya watu hao ni maulid kitenge ambae alimpongeza sana young dee na kulalamika kwanini hakumualika katika harusi yake.

Lakini pia Jackline Wolper alimtumia Young Dee salamu za pongezi na kumtakia maisha mema katika  ndoa yake hiyo mpya.

Amber Lulu Apewa Kichapo Cha Mbwa Koko na Young Dee

Video Vixen na msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na Single yake ya ‘Jini kisirani’ Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu amekiri kupokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa msanii mwenzake Young Dee.

Wiki iliyopita kipindi cha XXL cha Clouds Fm waliripoti kuwa Kwenye studio fulani hapa Mjini Amber Lulu alionekana akiwa anapigwa vibao, ngumi na hadi mateke na Young Dee.

Baada ya kipigo hiko Amber aliweka wazi kuwa sababu iliyomfanya mpaka Young Dee ampige ni baada ya kukataa kuwa naye Kimapenzi na kisha kutinga ndani ya studio hizo na mwanaume mwingine.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Amber alikiri kupigwa na Young Dee lakini amesisitiza kuwa ulikuwa ni wivu wa kimapenzi:

Kweli Young Dee amenipiga kwa ajili ya wivu mimi ni mzuri lazima unitamani we mwenyewe umeona hili tak* usilitake Tena ? Mimi ni mzuri alafu ananitaka halafu mimi simtaki siwezi kuwa na bwana mariooo alivyoniona akaanza kuniletea Sholo nyingi alafu mimi sitaki shobo”.

Amber Lulu ameshawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee katika siku za nyuma lakini wawili hao walishaachana ingawa Amber amekiri mara kwa mara kuwa anampenda sana.

Young Dee- Nataka Kumsaini Young Killer

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vyema katika ulimwengu wa kuchana Young Dee aka Paka Rapa amefungukia mipango yake kumsaini msanii mwenzake Young killer Msodoki.

Kwa mara ya kwanza Young Dee aliweka wazi mipango yake ya kumsaini Young Killer kwenye label ya King cash ambayo anafanya nayo kazi kwa sasa na  kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Hahaha siku ya kwanza ofisini wakati nataka kumsign mdogo wangu #youngkillermsodokii?? ni kweli anachana sana kijana ana kipaji!”.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Young Dee alifunguka na kumwagia sifa kibao msanii huyo ambapo aliandika:

Young Killer ni rapa mzuri sana, namkubali sana lakini ishu za kumsaini ni mapema sana pale niliandika kama masihara lakini mimi nadhani ni jambo ambalo linawezekana kama nikiamua kwa sasabu ana kila kitu”.

Hivi sasa Young Killer Msodoki anafanya  kazi chini ya label ya Wanene Entertainment.

Agnes Masogange Alikuwa Mtu Wa Watu- Young Dee

Staa wa Bongo fleva David Genzi maarufu kama Young Dee amefunguka na kusema kuwa marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ alikuwa mtu wa watu sana.

Ikiwa imepita wiki moja sasa tangu Masogange aage dunia mastaa wenzake bado wanaendelea kumkumbuka na kumlilia huku ikionekana wazi kabisa kuwa itakuwa ngumu kuziba pengo lake.

Kwenye mahojiano na Championi Jumatano, Young Dee alisema kipindi cha uhai wake, Masogange alikuwa ni mtu wa watu ambaye alikuwa hapendi ugomvi na hajawahi kusikia akigombana na mtu japo yeye hajawahi kufanya naye kazi.

Japo sijawahi kufanya naye kazi, lakini alikuwa mtu wa watu kwani sijawahi kusikia akigombana na mtu yeyote, kwa sasa wasanii tuendelee kumuomba Mungu na tuachane na maovu pia tuwe wamoja kwani hujui lini utakufa“.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua Ugonjwa wa Nimonia na upungufu wa damu mwilini na kisha kuzikwa wiki hii siku ya Jumatatu kijijini kwao Mbeya.

Nisha Akana Skendo Ya Kumtongoza Young Dee

Muigizaji wa Bongo movie anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya Bachela amejibu tuhuma alizotupiwa kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo fleva Young Dee.

Siku ya jana msanii wa Bongo fleva Amber Lulu alitoboa Siri na kusema kuwa kipindi ana Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, mwanadada Nisha alikuwa anamtongoza Young Dee.

Amber Lulu aliweka wazi kuwa jambo hilo lilikuwa la wazi hadi alikuwa ana ushahidi kwani alikamata meseji za wawili hao huku alikiri kuwa Nisha ni fundi wa mapenzi maana alikuwa anampa maneno matamu Young Dee.

Baada ya kutupiwa tuhuma hizo Enews ya EATV ili mtafuta Nisha kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na moja kwa moja alikataa na kusema kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee zaidi ya urafiki:

Mimi sina Mahusiano na Young Dee ila kilichotokea ni kwamba nilikuwa nataka ni kuingia kwenye muziki hivyo  Young Dee kama msanii wa Bongo fleva alikuwa ananisaidia na lazima niwe karibu na wasanii we zangu.

Alafu mimi nimemjua Young Dee kabla hata hajawa na Mahusiano na Amber Lulu kwaiyo ni mtu wangu wa karibu na trust me angekuwa mpenzi wangu nisingeweza kuficha maana mimi nikipenda nataka watu wote wajue”.

 

Amber Lulu: Nisha Alikuwa Anatembea na Young Dee Wakati Niko Naye

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amepasua jipu na kumuanika hadharani msanii mwenzake Nisha na kudai alikuwa anaingilia penzi lake na staa wa Bongo fleva Young Dee kwa kumtongoza.

Amber Lulu aliyewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Young Dee amekiri kuwa wakati akiwa na Mahusiano na Young Dee alikuwa mtu wa michepuko sana kiasi ya kwamba alishawahi kubamba meseji za  Young Dee na Nisha wakichat kama wapenzi.

Amber Lulu alitoa siri hiyo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya EATV ambapo amesema ushahidi kuwa wawili hao walikuwa wakichepuka anao:

Nikiona meseji zao walikuwa wanavhat vizuri tu sema kiroho safi sikumaindi sana kwa sababu hatukuwa official na mimi mwenyewe nilikuwa na mambo yangu pembeni lakini nina ushahidi kuwa Nisha Kapita kwa Young Dee.

Nakusema ukweli Nisha fundi maana ana maneno matamu nini nilisoma mpaka mwenyewe nikakubali”.

Nisha alipoulizwa habari hiyo alikana kusema meseji alizoziona Amber Lulu zilikuwa ni meseji za kikazi tu lakini hajawahi kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee.

Naibu Waziri Asema,Wimbo wa Bongo Bahati Mbaya Unapoteza Dhana ya Utanzania

Kwa mara ya kwanza siku ya March 14, Baraza la Sanaa nchini pamoja na Naibu Waziri walifanya presss conference na team nzima ya XXL kutoka Clouds Media Group na kufunguka mengi juu ya wasanii na nyimbo zilizofungiwa.

Naibu Waziri na BASATA wameamua kufanya press conference hiyo ili kuzungumza na kuweka wazi mambo mengi ambayo yalikuwa yakizunguka vichwani mwa watu juu ya kufungiwa kwa baadhi ya wasanii na nnyimbo zao huku baadhi ya watu wakisema kuwa BASATA na naibu waziri wamekuwa wakifanya swala hilo kwa miemuko yao wenyewe.

Akitoa ufafanuzi juu ya sababu za kufungiwa kwa wimbo wa bongo bahati mbaya, naibu waziri anasema kuwa wimbo huo umekuwa ukitoa dhana ya utanzania kwa sababu unakuwa kama unasifia nchi za nje na kutoa uhalisia wa msanii huyo ambae anaonekana kama kujuta kuwa Tanzania.

ule wimbo umekiuka misingi ya nchi, unaondoa kabisa dhana ya kujivunia utanzania.ndio maana kuna watu wanakaa wanasema no bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa tanzania.tumeufungia kwa kufuata sheria na taratibu kabisa.

Katika mjadala huo pia walikuwepo baadhi ya wasanii kama Vannesa Mdee ambao walikuwepo kusikiliza na kujua mambo ambalimbali kuhusu haki za wasanii .

 

Young Dee na Mzazi Mwenzake Wadaiwa Kumtelekeza Mtoto Wao

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Dar es Salaam Young D amekumbwa na skendo mpya ambayo safari hii inamhusisha yeye na mzazi mwenzake kuhusu kumtelekeza mtoto wao anayeitwa Tamar mwenye mwaka mmoja.

Mwaka jana habari zilisambaa mtandaoni kuwa Young Dee alimkataa mtoto wake ambapo mama wa mtoto huyo alijitokeza kwenye vyombo vya habari kudai ametelekezwa yeye na mtoto na baadae Young Dee alijitokeza na kumkubali mtoto wao.

Hivi karibuni kuna habari zimekuwa zikisambaa zikidai kuwa Young Dee na mzazi mwenzake Mama Tamar wamemtelekeza mtoto wao kwa bibi yake na wote wawili hakuna anayeishi naye kwa sasa.

Mama Tamar amefunguka kupitia Lemut Online na kusema mtoto anaishi kwa bibi yake lakini yeye binafsi hajamtelekeza:

Tamar yuko Tabata ambako ndio nyumbani kwa mama yake na Young Dee analelewa na bibi yake, uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kukaa kikao cha familia na tukaamua kuwa achukuliwe na bibi yake na mimi naenda kumuona kila wiki haipiti namuona na pia taarifa kwamba nilimtelekeza wakati mdogo ananyonya sio kweli nilimuacha akiwa na miezi kumi hivi”.

Mama Tamar amesisitiza kuwa yeye na Young Dee Hawako pamoja na pia hawezi kumlazimisha wawe pamoja kama akiamua walee mtoto pamoja basi atakubali wawe kama familia.

“Sijaona Hasara Kufungiwa Bongo Bahati Mbaya”- Young Dee

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Dar es salaam, Young D amefunguka na kudai hajaona kama amepata hasara yoyote kwa ngoma yake ya Bongo bahati mbaya kufungiwa.

Wiki iliyopita TCRA walitangaza rasmi kuwa wamefungia nyimbo 15 zisipigwe kwenye vyombo vya habari kwa kile walichodai kuwa BASATA wamezipitia na kuagiza zifungiwe kwa kukosa maadili ya Kitanzania.

Moja kati ya wasanii waliofungiwa ni Young Dee ambapo wimbo wake uliofungiwa unaitwa Bongo Bahati Mbaya (BBM) kwenye wimbo huo Young Dee anaimba kuwa hajapenda kuzaliwa Tanzania bora angezaliwa mbele pia wimbo huu ulikosolewa na Waziri Mwakyembe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Young Dee amefunguka na kusema Kufungiwa kwa wimbo wake wa Bongo Bahati Mbaya ilikuwa ni Ghafla na hakupewa taarifa yoyote hapo kabla wala kuonywa zaidi ya kuona kwenye mitandao ya kijamii lakini pia amekiri kuwa mpaka hivi sasa hajaona sababu ya wimbo huo kufungiwa Nay haelewi wanataka nini na nini hawataki.

Young Dee amesisitiza kuwa mpaka hivi sasa hajafikiria kwenda BASATA kuulizia kuhusu wimbo wake kufungiwa kwani mpaka hivi sasa hajaona hasara ya nyimbo hiyo kufungiwa labda atakuja kuiona mbeleni lakini hivi sasa.