Young killer Aelezea Alipomtoa Edu Boy

Msanii wa hip hop Bongo nchini, , Young Killer,  amefunguka na kusema ameshangazwa sana  na kauli ya Edu Boy kusema kwamba Baghdad amemfahamu yeye kupitia Edu boy wakati Young Killer ndio alimtoa Edu boy mkoani na kumleta Dar kufanya muziki.

Akizungumza na eNEWZ amesema kuwa wanahip hop nyuma yake wapo yeye sio wa mwisho hadi kufikia Baghdad kusema hivyo inawezekana kuna vitu ambavyo ameviona ndio maana vikampelekea yeye kusema hivyo hata hivyo amemshukuru kwa kumuona yeye kuwa anafanya vizuri hadi kufikia kumtaja.

Young killer anasema kuwa Edu boy anatakiw kukumbuka kuwa yeye ndio aliemtia shule na kumleta Dar na wasla sio hao anaowataja yeye katika mitandao ya kijamii.akiongea na waandishi anasema ”

“Sioni kama hakuna kwa mtazamo wangu inawezekana yeye hadi kusema hivyo kuna vigezo ameviona, ila pia Bahgadad  ni mdau mkubwa wa muziki wa hip hop pia ni mtangazaji na msanii  hivyo hadi kusema hivyo ni kwamba kuna vitu tayari ameviona kwangu ndio maana akasema lakini mimi naona wapo wengine waliokuja nyuma yangu na wako poa tu “, alisema Young Killer.

“Mama Ni Shabiki Wangu Mkubwa”- Young Killer

Msanii maarufu wa hip hop nchini Kassim Yusuph ‘Young Killer’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mama yake mzazi ni shabiki wake  mkubwa wa kazi zake za kisanii.

Young Killer ‘Msodoki’ amesema mama Yake shabiki wa kazi zake kiasi ya kwamba anaweza kuflow ‘Kurap’ nyimbo zake zote.

Msanii Young Killer na Mama Yake Mzazi

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Young Killer amesema kuwa kitendo hicho kinamfanya azidi kumpenda mama yake huyo ambaye pia amekuwa akimpa sapoti kwenye mishe zake za kimuziki.

Naweza kusema mama yangu ni shabiki wangu namba moja, ananisapoti kwa kila hali lakini pia hata nyimbo zangu zote anazi-floo fresh kabisa, ni mtu muhimu sana kwangu”.

Lakini pia Young Killer ameweka wazi kuwa ni muhimu kwake kupata sapoti ya mama yake kwani ni kama baraka inayomsaidia kufanikiwa zaidi katika kazi zake.

Young Killer aingilia ndoa ya Dogo Janja na Irene.

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini, Young Killer ‘Msodoki” amefunguka juu ya maneno aliyoyatumia katika wimbo wake wa kama inavyodaiwa kuwa ulilenga ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya.

Katika wimbo huo, Young Killer ametumia maneno yanayosema, “hata ukinitukana ni kawaida kama hizi ndoa za mabibi na vijana” ambayo wengi wametafsiri kuwa ni ‘dis’ kwa msanii mwenzake huyo lakini mwenyewe amesema kuwa hakumaanisha hivyo.

Akizungumza katika mahojiano na Friday Night Live (FNL) ya EATV, Young Killer amesema kuwa yale ni maneno tuu ambayo wasanii wa Hip Hop wamekuwa wakiyatumia lakini hayakumaanisha kuwa anamzungumzia Dogo Janja.

“Yale ni maneno tuu ambayo huwa tunayaandika, lakini sijamaanisha kumzungumzia Dogo Janja. Kwanza mimi na Dogo Janja hatuna ugomvi wowote na hatujawahi kuwa na ugomvi, nimezungumza kwasababu ni suala la kawaida tuu sasahivi kwa vijana kuwa na mahusiano na watu wazima”.

Pia Young Killer amesema mashabiki wake wategemee kazi kubwa kubwa kwa mwaka 2019 kwani alishaanza kufanya ‘Collabo’ za kimataifa mwaka uliopita kwa kufanya na Kaligraph Jones pamoja na Dela, wote kutoka Kenya.

Young Killer Adai Wasafi Festival ni Ukombozi Wa Kweli Kwenye Burudani

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Young Killer ameibuka na kulimwagia sifa kibao Tour ya WCB ya Wasafi Festival Baada ya kushiriki katika tamasha Lao la kwanza mkoani Mtwara.

Young Killer Msodoki amefunguka kwa kulisifu tamasha la Wasafi Festival na kudai kuwa ni ukombozi halisi katika sekta ya Burudani Nchini Tanzania.

Katika mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Young killer amefunguka haya zaidi kuhusu shoo hiyo:

Ujio wa Wasafi Festival ni mkubwa na umekuja kiutofauti sana na kiukweli tasnia yetu inahitaji vitu kama hivi kwa sababu haya ni mapinduzi kwani muda mrefu tumekuwa tukimiss matamasha yamekuwa machache kwaiyo kuja kwa Wasafi Festival ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwani inaonyesha ni kwa jinsi gani Sanaa yetu hivyo Big Up sana kwa Wasafi”.

Young Killer pia atakuwa mmoja wa wasanii Watakaoperfom kwenye shoo nyingine ya Wasafi Festival itakayofanyika Mkoani Iringa siku ya Leo.

Young Killer Akanusha Kumtukana Uwoya

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Young Killer ameibuka na kukana tetesi zilizosambaa kuwa alimdhihaki Msanii wa Bongo movie Irene Uwoya kwenye moja ya nyimbo zake.

Tetesi hizo zilisambaa Baada ya maneno aliyoimba  kwenye moja ya nyimbo yake kuzua utata ambapo alinukuliwa akiimba “Sishangai Hawa pimbi wakinitukana ni kawaida Kama bibi na vijana”.

Kufuatia maneno hayo kwenye verse ya nyimbo yake mashabiki wengi walidhani amemtupia dongo Dogo Janja ambaye kwa kipindi hiko alikuwa kwenye ndoa na Uwoya na walikuwa Kama na Bifu na Young Killer.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Young Killer amekanusha dongo hilo kumlenga Uwoya na kuweka wazi kuwa vijana waliooa Vibibi ni wengi sana kwenye mitandao ya kijamii.

Sikumaanisha hivyo na sidhani kama Uwoya ni bibi kwa kweli Mimi kwanza sidhani kama Irene Uwoya ni bibi wapo wengi waliooa watu ambao ni mabibi wapo wengi hata mitandaoni tunawaona usimchukulie tu Dogo Janja au namna gani vipi hebu mtoe kuna watu wengine kibao”.

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja ilipigwa sana vita kutokana na tofauti ya kiumri iliyokuwepo baina yao ambapo Uwoya alidaiwa kuwa mkubwa kuliko Dogo Janja.

 

Young Killer Afungukia Sababu Za Kukimbia Wanene

Msanii wa muziki wa hop hop nchini Young Killer amefunguka na kusema kuwa sababu iliyompelekea kuondoka katika music label ya Wanene ni kuisha kwa mkataba Wake wa miezi Sita.

Young Killer ameweka wazi kuwa baada ya kuisha kwa mkataba Wake hakutaka kusaini tena na label hiyo kwa sababu kwa muda ambao amefanya nao kazi kuna matarajio aliyategemea ndani ya kampuni hiyo lakini hakufanikiwa kupata alichokuwa anatafuta na kwamba badala yake aliona ni bora alipokuwa anafanya kazi akiwa mwenyewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Young Killer aliweka wazi kuwa moja kati ya mambo aliyokuwa anayatarajia lakini hakuyaoni ni pamoja na kukuza wigo wa muziki wake nje ya mipaka ya Tanzania.

Unajua hakuna kitu kizuri katika muziki wetu kama mafanikio ya kuzidi kupata connection tofauti-tofauti. Pia, nilikuwa nategemea kuona nyimbo zangu hata zinapigwa ‘Trace’, ili kuleta utofauti wa Young Killer yule ambaye alikuwa anafanya kazi mwenyewe na huyu ambaye anafanya kazi na Menejimenti kubwa kama Wanene. Hiyo ni moja ya mambo, lakini vitu ni vingi“.

Young Killer amesema pamoja na kuondoka katika label hiyo yupo tayari kufanya kazi na label nyingine endapo tu atapendezwa na mkataba atakaopewa.

Sijawahi Kuachwa na Mwanamke :-Young Killer

Msanii young killer amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake hajawahi kuachwa na mwanamke hata mara moja zaidi ya kuwaacha yeye.

Akiongea kuhusu muziki anasema kwa sasa anafanya vizuri katika muziki na kusema kuwa katika maisa yake yote ya mahusiano hajawahi kuachwa na mwanamke na kama watu wanajua kuwa kwa sababu yeye ni handsome asiekuwa na matunzo basi hajui kutupia watakuwa wanajidanganya.

kwenye mapenzi mimi sijawahi kuachwa na mwanamke yoyote,  na wasije wakaksikia kuwa kwa sababu mimi ni handsome nisie na matunzo basi wakajua kuwa siujui kutupia wanajidanganya,

Young killer liwahi kutangaza hivi karibuni kuachana na mrs superstar kwa sababu ambazo haziweza kuzuilika kati yao lakini walikuwa katika mahusiano kwa muda mrefu.

Young Killer atoa siri, Hakupata Alichokitengemea Ndani ya Wanene.

Msanii Young Killer wa Msodoki amefungka sababu kubwa ya kuondoka katika kampuni ya wanene entertainment mara vbaada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita bila hata kufikiria kuongeza muda katika kamouni hiyo iliyokuwa ikisimamia muziki wake.

Young killer anasema kuwa sababu kubwa ni kwamba hakukipata kile alichokuwa akitegemea kukipta pindi anaingia katika kamouni hiyo hivyo aliona kuwa ni bora kuondoka kwa sababu hakukuwa na adadhali huku akisema kuwa ni bora kule alikokuwa ametoka awali.

Young killer anasema kuwa alikuwa anategmea sana kupanua muziki wake nje ya Tanzania endapo ataingia katika kampuni hiyo lakini hakuona hivyo zaidi ya  kuendelea kukaa ndani ya nchi tu.

unajua hakuna kitu kizuri kama kuona mtu unafanikiwa katika muziki wake, kitu kikubwa nilitegemea hata kuona muziki wangu ukipigwa Trace  ili kuleta utofauti wa Young killer aliekuwa akifanya kazi mwenyewe na huyo wa kwenye menejimenti,  kuba kama wanene, hiyo ni sababu moja lakini vipo vitu vingi.

Young killer anasema kuwa yuko tayari kufanya kazi na klebo nyingine yoyote ilhali watakuwa tayari kumpigisha hatua na kutoka pale alipo.

 

Young Killer Aondoka Wanene Entertainment

Msanii Young killer amefunguka na kusema kuwa mkataba wake na uongozi wa Wanene Entertainment umemalizika hivyo kwa sasa hayupo tena katika uongozi huo.Young killer anasema kuwa mkataba huo ulikuwa ni wa miezi sia na kwa sababu umekwisha hawezi kuendelea nao tena.

katika ukurasa wake wa instagram, Young killer aliandika “nawashukuru sana wanenen stuido kwa kuniamini na kupiga kazi na mimi kwa mkataba wa kipindi cha miezi sita ambacho mkataba wetu umekwisha na sitaweza kuendelea nao tena.

Nawashukuru sana kwa kipindi chote cha miezi sita cha mkatab kwa kushirikiana pamona na kazi nzuri tulizozifanya, tulifanya kazi pamoja na lengo lilikuwa ni kuniona mimi ninafika mbali zaidi.nimepitia vitu vingi sana na changamoto nyingi na zaidi ninasema tu nimejifunza mengi , ambavyo vitabaki kama alama  na kuniongoza katika safari yangu nyingine ya muziki.

Ikumbukwe kuwa Young killer alisaini mkabata na studio hiyo mapema april mwaka huu na akiwa katika uongozi huo aliweza kutoa wimbo na msanii Khaligraph Jones.

Dogo Janja na Young Dee Hawaniwezi Kwenye kazi;-Young Killer

Msanii wa hip hop nchini young kileer ameibuka na kusema kuwa wasanii wenzake wawili vijana young dee na Dogo Janja hawamuwezi katika kazi za muziki kwa kuwa yeye ni bora kuliko hao wengine .

Hii inaweza kuleta tena ugomvi tena kwa mara ya pili kwa sababu hii sio mara ya kwanza kwake kuongea hivyo na kuzuka wimbi la maneno katika mitandao ya kiamii kuhusu kushindana kwao huko.

kwa upande wa Young Dee alishawahi kusema kuwa yeye kwa wenzake hao wawili ni mkongwe na hakupenda hata siku moja kulinganishwa nao kwa sababu uwezo wake ni mkubwa zaidi.

kwenye kazi dogo janja na young dee hawaniwezi hao ni wadogo zangu sana.mimi ndio mkubwa wao katika kazi.

 

Yound killer Angeweza Kupata Pesa Kupitia Neno ‘Pambana na Hali Yako’.

Inawezekana ingekuwa faida kuwa kama msanii Young Killer angeweza kupata faida sana baada ya msemo pambana na hali yako aliowahi kuutumia katika baadhi ya nyimbo zake kuvuma na kutumiwa sana kama msemo halisi katika lugha.

Wasanii wengi nje mfano 50 Cent aliwahi kuuza moj aya maneno yake ya wimbo na kupata faida kubwa tu, huku ni kutokana na nchi aliyopo labda kwa sababu pia wanajua kuwa kuna baadhi ya vitu vidogo vidogo ndivyo vinaweza kuwapatia wasanii pesa.

Young Killer haonekani kuwa na mpango wa kufanya hiyo biashara kwa kuwa hata yeye anahoji kuwa ni nani atakbali kuununua msemo huo na je akinunu ana uhakika gani kama utauza, lakini pia haijawahi kufanyika kwa baishara kama hiyo nchini hivyo ni ngumu sana kwake.

sijafikiria kuuza lakini manen yetu haya haya tungeyageuza yangeweza kutupatia pesalakini hata huyo unayetaka kumuuzia ana kuwa hana uhakika kama anaweza kupata faida kutokana na neno hilo.kwamba ni kweli huo msema unaweza kuwa habari nyingine mpaka yeye akajitoa na kuwekeza ela kwako.

“Siwezi Kumiss Miss Hip Hop Maana Alinitesa Sana”-Young Killer

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri katika miondoko ya Kuchana Young Killer Msodoki amefunguka na kuweka wazi kuwa hajamiss aliyekuwa mpenzi wake Miss Hip Hop.

Young Killer na Miss Hip Hop walikuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu lakini wawili hao walimwagana mwaka jana huu huku sababu Ikiwa sio ya wazi.

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni na kituo kimoja cha habari, Young Killer ameweka wazi kuwa hajamiss aliyekuwa mpenzi wake kwani alimpa mateso sana enzi za penzi lao.

Kusema ukweli kwa sasa hakuna ninachomiss kutoka kwake ila alinitesa sana kwa Mwanzoni kwa sababu ni mtu ambaye nilikuwa nimezoeana lakini kwa sasa nimezoea kwani ni mwaka karibia na nusu unaenda tangu tuachane kwaiyo right now am new Young Killer”.

Lakini pia Young Killer amesema kwa hivi sasa yupo single na anapambana na hali yake tangu aachane na Miss Hip Hop kwa sababu hakutaka kutafuta mwanamke mwingine ili tu amkomoe Ex wake ambaye tayari ana mpenzi mwingine.

Young Dee- Nataka Kumsaini Young Killer

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vyema katika ulimwengu wa kuchana Young Dee aka Paka Rapa amefungukia mipango yake kumsaini msanii mwenzake Young killer Msodoki.

Kwa mara ya kwanza Young Dee aliweka wazi mipango yake ya kumsaini Young Killer kwenye label ya King cash ambayo anafanya nayo kazi kwa sasa na  kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Hahaha siku ya kwanza ofisini wakati nataka kumsign mdogo wangu #youngkillermsodokii?? ni kweli anachana sana kijana ana kipaji!”.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Young Dee alifunguka na kumwagia sifa kibao msanii huyo ambapo aliandika:

Young Killer ni rapa mzuri sana, namkubali sana lakini ishu za kumsaini ni mapema sana pale niliandika kama masihara lakini mimi nadhani ni jambo ambalo linawezekana kama nikiamua kwa sasabu ana kila kitu”.

Hivi sasa Young Killer Msodoki anafanya  kazi chini ya label ya Wanene Entertainment.

Young Killer Afunguka Baada Ya Aliyekuwa Mpenzi Wake Kushika Ujauzito Wa Mwanaume Mwingine

Mwanamuziki wa Bongo fleva Young Killer amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya habari kusambaa kuwa aliyekuwa mpenzi wake Halimaty au maarufu kama Miss Hip hop amebeba ujauzito wa njema nyingine.

Young Killer na Miss Hip Hop walikuwa Kwenye Mahusiano kwa muda mrefu lakini Habari za wawili hao kuachana zilisambaa wiki chache zilizopita.

Kwenye mahojiano na Soudy Brown Kupitia Clouds Fm Young Killer amesema hajakasirikia wala kuona wivu kuona Ex wake amebeba ujauzito wa mwanaume mwingine kwani ni jambo la kawaida.

Ni jambo la kheri, hapana siumii kwa sababu hakuna kitu kama kuona mtu ambaye mlikuwa mnapeana furaha anaendelea kufurahi”.

Lakini pia Young Killer amekanusha taarifa kuwa kipindi cha mahusiano yao alikuwa akimnyanyasa mrembo huyo.

Hapana, ni maneno ya watu hayo kwa sababu matatizo madogo madogo, sijui michepuko huwa ni vitu vya kawaida kwenye mapenzi, huwa havikosi, umenisoma?”.

Hivi sasa Young Killer anatamba na wimbo wake mpya unaoitwa Shots aliomshirikisha Khaligraph Jones kutoka Kenya.

 

Young Killer: Siwezi Kubadilisha Muziki Ninaofanya

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap, Erick Msodoki maarufu kama Young KIller ameibuka na kuweka wazi kuwa hana mpango ya kubadilisha muziki anaofanya.

Sio siri kwenye gemu la Bongo fleva imeonekana wazi kabisa kwa miaka ya hivi karibuni muziki unaopewa nafasi na wenye soko zaidi ni muziki wa taratibu ile RnB na mziki wa Hip Hop umeonekana kulega lega kidogo.

Mara kadhaa Young KIller amekuwa akipewa ushauri na mashabiki zake wanataka abadilishe aina ya kuchana ili aweze kuangalia kama mziki wake utapata soko zaidi katika upande mwingine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Vibes, Young KIller amesisitiza kuwa hawezi kubadilisha aina ya muziki anaofanya kwani ndio muziki uliompa mafanikio mpaka leo anajulikana kwa mashabiki zake:

Sasa hapo nibadilike nini. Mtu unayepata shoo nyingi inaonesha wazi kwamba unakubalika. Siwezi kubadilika na nitaendelea kukimbiza zaidi na zaidi“.

Hivi sasa Young Killer anafanya vizuri na wimbo wake wa Shots aliomshirikisha rapa mkali kutoka 254 Kenya anayeitwa Khaligraph.

Young Killer Arudisha Majeshi Kwa Miss Hip-Hop

Siku chache  zilizopita msanii wa hip-hop nchini Young Killer alifunguka na kusema kuwa hana mahusiano tena na mpezni wake Miss hip-uop kutokana na kushindwa kuelewana kwao kuliowafanya washindwe kuwa pamoja kwa zaidi ya miezi sita.

hivi karibuni siku ya wanawake duniani katika snapchat ya msanii huyo ilionekana picha ya mwanadada huyo ambae  alikuwa mpenzi wake na ikasemekana kuwa aliachana nae lakini inavyoonekana ni kwamba wawil hao wako pamoja tena.

                                             

 

Miss hip-hop na Young killer wamekuwa wapenzi kwa miaka mingi , lakini hapo katikati waligombana na kushindwa kukaa pamoja.