Z-Anto Afungukia Tetesi Za Kuoa Mke Wa Pili Kwa Siri

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Ally Mohamed maarufu kama Z- Anto ameibuka na kukana taarifa zinazosambaa kuwa ameoa mke wa pili bila kumtaarifu mke wake .

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa  mwana­muziki huyo hivi karibuni alifunga ndoa na dada wa msanii wa filamu, Wastara Juma aitwaye Naima huku mke mkubwa akiwa hajui, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Dini ya Kiislamu.

Mke wa Z-Anto alisema alikuwa anakuta meseji kwenye simu ambazo mumewe huyo alikuwa akiwasiliana na huyo Naima akawa anamuuliza lakini anakuwa mkali, baadaye aligun­dua kuwa walishafunga ndoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Z-Anto amekataa Tetesi Za kuoa mke mwingine na kusisitiza kuwa taarifa hizo zinazosambaa hazina ukweli wowote.

Niwaambie tu kwamba hizo habari za mimi kuoa hazina ukweli, mimi na mke wangu tuko vizuri kabisa hatuna tatizo ila kama anasema ameenda Bak­wata mimi ndio kwanza nawasi­kia nyie.

Ningekuwa nimeoa ningeweka wazi tu lakini hakuna kitu kama hicho, kuhusu kuwa karibu na familia ya Wastara ni kwamba nil­ianza urafiki na familia hii kama miaka 10 iliyopita, nilikuwa nam­fanyia dua mume wa Wastara marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ alipokuwa anaumwa”.

Kuhusu picha zake na Naima za ndoa zilizosambaa kwenye mitandao, msanii huyo alisema kuna kitu walichokuwa wana­kifanya kuhusiana na sanaa ambacho kwa sasa hawezi kukiweka wazi.

 

 

Z-Anto Atoa Sababu Inayomfanya Wasanii wachanga kukata Tamaa ya Kuimba

Msanii Z-anto ambae alitamba sana na wimbo wake wa binti kiziwi amefunguka na kusema kuwa mja ya sababu kubwa iliyowahi kumaktisha tamaa katika kufanya kazi za muziki ni kutokana chuki zinazoendekezwa baina ya wasanii na wadu wa muziki.

Akitoa uzoefu wake katika hili z-anto anasema kuwa mwaka 2008 aliwahi kuwekwa katika kinyanganyio kimoja nchi lakini hakuweza kupata chochote ingawa  alikuwa anaonekana kuwa alikuwa anafaa kwa kinyanganyio icho na hiyo yote ni kwa sababu tu  moja ya watu walioandaa mashindano hayo alikuwa amegombana nae.

Akiongea na clouds media anasema “mwaka 2008 nilikuwa kwenye kinyanganyio cha msanii bora chipukizi , lakini sikuingia wala kushinda kwa sababu kuna mtu mmoja kati ya wale waliokuwa wakisimamia shindano ilo nilikuwa nimegombana nae, japo nilikosa tuzo lakini haikunifanya niache muziki.”

Z Anto Kuja na “Mpaka Naogopa” Baada Ya Kimya Kirefu

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na vibao vyake kama vile ‘Binti kiziwi’ na ‘Mpenzi jini’ Z Anto ametangaza kurudi kwenye  gemu baada ya kimya kirefu.

Baada ya kufanya vizuri sana miaka ya nyuma Z Anto alikaa kimya kwa muda mrefu mpaka mwaka jana alipoachia Wimbo Mpya ‘Cheza unapochezaga’ ambao haukuweza kumrudisha vizuri Kwenye chati.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Z Anto amesema kwamba wimbo wa kwanza ‘Kacheze Unakochezaga’ ulikuwa wakuombea msamaha kwa watanzania kutokana na ukimya wake na baada ya kuona amekubaliwa anajipanga kuachia wimbo wake mpya alioupachika jina ‘Mpaka Naogopa’.

Ni project mpya inakuja soon, wimbo nimefanya kwa Mazuu ni ngoma kali sana ambayo itakuja kuwaonyesha mashabiki kwamba mimi ni nani katika muziki wa BongoFleva, nimefanya vingi lakini pia naweza kubadilika.

Kacheze Unakochezaga ni wimbo ambao niliuachia kuwaomba mashabiki msamaha baada ya kukaa muda mrefu bila kuachia wimbo. Na wimbo wangu mpya ‘Mpaka Naogopa’ ni wimbo ambao utawafanya mashabiki wangu waamini kwamba Z Anto ni mtu au msanii tofauti sana katika tasnia ya muziki na ni tofauti na hao wengine ndio maana nikasema mimi siji kushindana kwa sababu nina kitu tofauti“.

Z Anto amewataka mashabiki zake wanaenda mkao wa kupata burudani kwani ana akiba zaidi ya nyimbo ya 20.

Z Anto: Sina haja ya kushindana na Diamond na Ali Kiba

Z Anto amegonga vichwa vya habari kwa kutoa madai ambayo imewatikisha mashabiki wa Diamond Platnumz na Ali Kiba.

Mwimbaji huyo ambaye alivuma kwa ngoma yake kali – ‘Binti Kiziwi’ amekiri kuwa Diamond na Ali Kiba ndo mabingwa wa muziki wa Bongo lakini ako na uhakika kuwa atawaangusha kumuziki.

Z Anto

Z Anto alifunguka kuhusu mpanga wake ya kuwabwaga Diamond na Aki Kiba akiongea na Bongo5. Alisema kuwa haitaji kushindana nao kwani muziki wake utapita katikati yao na kunawiri kuwashinda.

“Mimi ni mkongwe kwenye huu muziki na bado nina nafasi ya kufanya mambo makubwa zaidi. Najua kwa sasa Diamond na Alikiba ndio wasanii wanaozungumziwa zaidi lakini mimi sina haja ya kushanda nao muziki wangu nitaupitisha katikati yao,” alisema Z Anto.