“Zamaradi Moyo Wangu Unaumia Kwa Ajili Yako”- Zari

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kumtumia salamu za rambi rambi Zamaradi Mketema Baada ya Ruge Kufariki.

Marehemu Ruge Mutahaba alikuwa kwenye mahusiano na Zamaradi Mketema kwa miaka mingi na  kufanikiwa kuzaa naye Watoto wawili wadogo.

Tangu Ruge amefariki Zamaradi amekuwa akionekana mwenye majonzi na hasa kwa sababu baba wa Watoto Wake amefariki.

Zari amemtumia salamu za kumfariji Zamaradi kwa sababu na yeye mwaka jana alifiwa na baba wa Watoto Wake watatu Ivan Semwanga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameweka picha ya Zamaradi na Watoto Wake wakiwa kwenye msiba na kuandika maneno machache “My heart bleeds for you Zama”.

“Mume Wangu Angenishangaa Kama Nisingemsaidia Ruge”- Zamaradi

Mtangazaji na mdau mkubwa wa Bongo movie Zamaradi Mketema amefunguka na kuweka wazi sababu ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha michango kwa ajili ya matibabu ya baba Watoto Wake Ruge Mutahaba.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Zamaradi alisema kuwa angeonekana mtu wa ajabu na watu wangejiuliza endapo na yeye angekuwa nyuma kutohamasisha watu kuchangia matibabu ya Ruge ambaye pia ni baba wa watoto wake wawili.

Unajua watu wangekuwa kwenye mshangao endapo nisingefanya kitendo cha uungwana cha kuamua na mimi kuchangisha. Hata mume wangu angenishangaa, lakini pia ugonjwa siyo kitu cha kufanya mashindano hata kidogo maana yeyote anaweza kuumwa“.

Watoto wangu wanampenda baba yao na wanampenda baba anayewalea hivi sasa, lakini mimi kutoonesha kuguswa katika hili, hata watoto wangu wangenishangaa sana. Unajua suala la mgonjwa linamgusa kila mtu”.

Ruge alianza kuchangiwa fedha za matibabu mwanzoni mwa wiki hii baada ya familia yake kuomba kusaidiwa katika kipindi hiki ambacho jamaa huyo anaendelea na matibabu ya matatizo ya figo nchini Afrika Kusini.

“Babu Tale Alinitambulisha Kwa Ruge”- Zamaradi

Mtayarishaji na Mdau wa filamu za Bongo movie Zamaradi Mketema amefunguka na kuongelea mahusiano yake na baba Watoto Wake Ruge Mutahaba.

Kwa miezi kadhaa sasa Ruge amekuwa hospitali nchini Africa ya Kusini ambapo ndugu zake wamejitokeza na kuomba msaada kwa Watanzania kutokana na matibabu kuwa makubwa kupitiliza.

Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wamekuwa waliwaalika wadau mbalimbali ambao wanaguswa na maisha ya Ruge na kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu mwanaharakati huyo wa muziki wa Bongo Fleva.

Siku ya jana alialikwa Zamaradi  ambaye ni mama watoto wa Ruge ambapo amefunguka mambo mbalimbali pamoja na namna alivyokutana na bosi Ruge.

Tulikutana na Ruge kwenye mazingira ya kazi, na mimi nimemjua Ruge kupitia Babu Tale. Tale ndio mtu ambaye alinitambulisha kwa Ruge kwa mara ya kwanza, alinipa namba yake akanimbia mtafute huyu bwana lakini usimwambie kama mimi ndiye niliyekupa namba”.

 

Zamaradi Mketema Akana Kabisa Kuajiriwa Wasafi Tv

Mtangazaji na Mdau mkubwa wa tasnia ya Bongo movie Zamaradi Mketema ameibuka na kukataa kata kata kuwa amewahi kuajiriwa na kituo cha televisheni cha Wasafi Tv.

Miezi michache iliyopita Baada ya Zamaradi kuachana rasmi na Clouds Media alikokuwa anafanya kazi kwa muda mrefu alianza kuonekana na Mkurugenzi wa Wasafi Tv Diamond Platnumz na kuaminika kuwa ataanza kufanya kazi katika kituo hiko.

Lakini sasa Zamaradi anakataa na kusema kuwa tofauti na watu wengi wanavyoamini yeye hajawahi kuajiriwa na Wasafi bali aliingia nao mkataba wa kufanya nao kazi kama mtu anayejitegemea.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online, Zamaradi alifunguka hay kuhusu ishu yake ya kufanya kazi na Wasafi:

Kwani ni lini nilisema nipo Wasafi au sio huko Wasafi Tv ni partners tu na sijawahi kuajiriwa kokote na hii nilishawahi kuongea zaidi ya mara mia”.

Zamaradi alikana pia tetesi za kuwa amegombana na Diamond ndio maana mkataba Wake na Wasafi umevunjwa:

Sio kwamba tumeachana kuna project zipo zitakapokuwa tayari tutaendelea kufanya kazi kama kawaida kwahiyo siyo kwamba niliajiriwa  nikavunja mkataba au walikuwa wameniajiri wakanivunjia mkataba siajwahi kusaini mkataba na mtu yoyote wa ajira”.

 

Mashabiki Wahoji Mahusiano ay WCB na Zamaradi.

Mtangazaji wa zamani wa Clouds Media Group, Zamaradi Mketema ambaye baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake ya kimapenzi na Mkurugenzi wa CMG, Ruge Mutahaba, alihamia Wasafi Media kuendelea na career yake.

Baada ya uzinduzi rasmi wa Wasafi TV na Wasafi FM, ilitarajiwa mtangazaji huyu mahiri kuanza kuonekana kwenye runinga akiendesha kwa mafanikio kipindi kama alivyokuwa akifanya Take One na kituo chake cha kazi cha zamani.

Tofauti na matarajio ya wengi, ghafla mwanadada Zamaradi ameanza kujiondoa kushiriki kwenye kazi zote zinazohusiana na Wasafi pengine kabla hata ya kuanza. Na kwa tukio la hivi karibuni la Wasafi Festival, hakuonekana kuongelea chochote kama ilivyo ada kwenye projects nyingine za Mwajiri wake huyo mpya.

Sasa, kwa sababu bado hakujatoka official say, naomba kupitia uzi huu tukajaribu kudodosa endapo kuna lolote linaloendelea linalopelekea awe kimya kabisa huku akionekana kuwa busy na shughuli zake nyingine.Maswali ya shauku;

1. Mgongano wa kimaslahi na kukomoana baina ya Wasafi Media na Clouds Media umemweka njia panda?
2. Hali ya Afya ya mzazi mwenzie (Ruge) imemfanya ashindwe kuvumilia kuhimili vishindo vya kejeli kutoka kwa wanaofurahia anguko lake?
3. Ameshindwana malipo na Wasafi Media?
4. Anaamua kuwa freelancer?
5. Ana mpango wa kurudi Clouds Media Group?

Hayo ni miongoni mwa maswali yamekuwa yakiulizwa na mashabiki katika kurasa nyingi za udaku huku wakitaka kujua kwa hamu juu ya swala hlo ingawa pia  moja ya watu wanaopenda kufatilia mambo katuka mitandao dada Mange Kimambi alisema katika mojaya majibu ya mashabiki kuwa zamaradi tayari ameshindwa kuelewana kikazi na WCB hivyo ameona ni bora kuachana nao tu.

Irene Paul Afungukia Bifu La Zamaradi na Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Irene Paul amefunguka na kupima uzito bifu lililopo kati ya rafiki yake kipenzi Zamaradi Mketema na Hamisa Mobetto.

Wiki chache zilizopita Zamaradi na Mobetto waliingia Kwenye bifu zito mara baada ya kutokea sintofahamu Kwenye mavazi ambayo Zama aliyavaa kwenye arobaini ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Irene alisema Zamaradi alipoingia kwenye ugomvi na Mobeto hivi karibuni kisa kikiwa mshono wa nguo aliyovaa kwenye arobaini ya mwanaye, yeye aliamua kujiweka pembeni kwa sababu aliogopa kuchukuliwa hatua za kisheria kwani serikali kwa sasa haitaki mchezo.

Si unajua tena siku hizi sheria za mtandao, unaweza kujifanya kimbelembele yakakukuta mazito kwa hiyo niliona nikae pembeni licha ya kwamba Zamaradi ni rafiki yangu sana kwa sababu nilifahamu pia wawili hao wangeweza kumalizana bila tatizo lolote”.

 

Sijaajiriwa , Mimi ni Boss Mwenyewe :-Zamaradi

Mwanadada Mamaradi mketema anasema kuwa sio kwamba yeye ni mwajiriwa katika studio za wasafi lakini yeye amejiajiri mwenyewe kutokana na kazi anayoifanya huko wasafi.

Zamaradi anasema kuwa kwa hatua aliyofikia hawazi kuajiriwa kwa sasa kwa sababu ameshakuwa na anatamani kuwa zaidi ya hapo lakini sio kupitia kuajiriwa kwa sababu kwa kipindi alichoajiriwa kinamtosha kujendelea kujikuza yeye mwenyewe.

Hata hivyo Zamaradi amsema kuwa misingi mikubwa aliyojiwekea ni kufanya kazi pamoja na watu mbalimbali kwa mikataba na muda fulani baada ya kazi kuisha basi anatafutwa watu wengine wanaotaka kufanya  nae kazi.

Mimi sasa hivi ninaweza kusema kuwa ni boss wangu mimi mwenyewe,nilishaajiriwa na Clouds na sehemu mbalimbali zilizonikuza na kuwa zamaradi kama zamaradi mimileo. na kwa stage niliyofikia sasa hivi nafikiri ni bora kufanya kazi katika misingi itakayonikuza zaidi, na kwa ninavyoamini mimi sidani kama kuajiriwa kutanikuza zaidi.Kwaio ninapenda tu kupata na watu na kufanya kipindi flani na watu flani kwaio sijaajiriwa kwakweli.

Wema Aingilia Bifu La Zamaradi na Mobetto

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amejikuta Tena katika headlines za social media baada ya kuingilia kati bifu linalo trend hivi sasa kati ya Zamaradi Mketema na Hamisa Mobetto.

Zama na Mobetto waliingia Kwenye bifu hili baada ya kutifuana kuhusu mshono wa vazi alilovaa Zamaradi Kwenye 40 ya mtoto wake wiki chache zilizopita.

Zamaradi aliandika waraka mrefu wa kurasa tatu ukieleza namna alivyosikitishwa na maneno yanayosambaa mitandaoni kuwa alipewa mshono na Mobeto kwa lengo la kushonewa, lakini akauchukua na kwenda kuushona kwa mtu mwingine huku akimwaga chati zote za WhatsApp walizokuwa wakitumiana.

Lakini pia kwa Mobeto naye aliibuka na kupinga vikali waraka huo. Wakati hayo yakiendelea, Wema kupitia ukurasa wake alinunua ugomvi kwa kuandika; Tuendelee ama tusiendelee’.

Meneja wa Wema, Neema Ndepanya naye hakukaa kimya, aliingilia kati na kumkingia kifua Wema kwa kuandika waraka wake. “Kiki za kuchafuana zilishapitwa na wakati, hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa mnafiki, yaani nachukia mtu anajifanya kila wakati anaonewa yeye tu,”

.

Zamaradi Aongelea Swala la Dina Marious

Mwanadada Zamaradi Mketema amefunguka na kujibu tuhuma alizokuwa akizsudhiwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya page za udaku kuwa yeye ndui chanzo kikubwa cha Dina Marious kufukuzwa kazi Clouds media na kuanza kutafuta kazi sehemu nyingine.

Wakati Dina na Zamaradi wakifanya kazi clouds , walikuwa marafiki hapo mwanzo lakini dina alikuja kusikika ameacha kazi clouds ilikuja kusemekana kuwa kuna vitu vya chini chini vilikuwa vikiendelea kati ya dina na zamaradi vilivyosababisha mwanamama huyo kufukuzwa kazi.

Hata hivyo akiongea na bongo 5, Zamaradi anasema kuwa haiwezekani kuwa mahusiano yake na mkurugenzi wa vipindi clouds media usababishe kufukuzwa kwa Dina, huku akihoji kama Dina aliwahi kuwa mke mwenzie.

kuhusu Dina Marious , sikuwahi kugombana nae wala sikuwahi kuambiana nae mjinga au mjinga mwenyewe wala nini, na kwa mtu mwenye akili kubw unaweza kukaa ukawaza kuwa kwa mtu kama mimi ambae nilikuwa tu mtangazaji , ninawezaje kumfukuzisha mtu kazi.

siwezi kumlaumu mtu yoyote lakini ndio hivyo siku zote mti wenye matunda ni lazima utapigwa mawe.

hata hivyo alipoulizwa kuwa sababu kubwa ni kwa kuwa yeye kipindi icho alikuwa na nguvu kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi  na bossi ruge, ndipo zamaradi alipohoji ” kwani mimi Dina alikuwa mke mwenzangu “

Zamaradi Adai Uvumilivu Ulimshinda Akaamua Kumwaga Povu Mtandaoni

Mtangazaji wa Wasafi Tv Zamaradi Mketema amefunguka baada ya bifu lake na mrembo Hamisa Mobetto na kudai uvumilivu ulimshinda ndio maana akamwaga povu lile Instagram.

Siku chache zilizopita Zamaradi na Mobetto waliingia kwenye vita kali ya maneno baada ya kugombana kisa nguo ambayo Zamaradi alivaa kwenye 40 ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Zamaradi amefunguka na kudai kuwa alifunguka na kuongea mambo Yale kwa sababu alishindwa kuvumilia kusemwa vitu vya uongo ili hali ukweli upo.

NI kweli nimeongea na kuweka vitu wazi lakini yule sio mimi ila kuna muda  tu vitu vinakufika kooni na kushindwa kuvivumilia kwa sababu hata uongo unapozungumzwa sana hugeuka na kuonekana kama ndio ukweli na Watanzania ni watu wa kuchukua kitu kama kilivyo na kila mtu hongea lake na sikuongea kama ni povu bali nilitaka kuweka wazi ili watu waelewe nini kinaendelea”.

 

Hamisa Mobeto na Zamaradi Hapatoshi.

Mwanadada Hamisa Mobeto na mwanamama Zamaradi Mketema wameingia katika bifu zito na kujibishana  maneno katika mitandao ya kijamii baada ya Zamaradi kumshushia maneno mazito hamisa Mobeto kwa kumsambazia habari za uongo kuhusu makubaliana yao ya kushonewa nguo kwa ajili ya 40 ya mtoto wa Zamaradi.

Katika kurasa za udaku , hapo awali kuna ukurasa uliandika mambo mengi kuhusu zamaradi ikiwa ni pamoja na kwamba nguo alivaa siku ya sherehe hiyo ilitakiwa kushonwa kwa hamisa lakini cha ajabu baada ya hamisa kumpa mshono zamaradi, basi zamaradi akakimbia kwa fundi mwingine , lakini pia kuwa sherehe hiyo ilichangishwa pesa kutokwa kwa wadau na mshabiki zake .

Baada ya maneno hayo ndipo Zamaradi naeo alipoamka na kutaka kuonyesha ushahidi wa yote yaliyokuwa yakiongelewa na kusema kuwa pesa hakuwahi kumchangisha mtu yoyote zaidi ya pesa ya zawadi ambayo wanakikundi waliamua kumpa siku hiyo na wala hakuwa anajua hilo.”tukija kwenye nguo naambiwa kuwa nilipewa mshono na mwingine na nikaenda kushona kwa mwigine, funny nimeattach hapo juu na picha muone kuwa mimi ndio nilietuma mshono wake na wala sio yeye.kutokana na kupishana na muda nikaona bora nikashone kwingine , kwanza ni uamuzi wangu kuamua kushona popote pale.”

Hata baada ya zamaradi kuongea hivyo, Hamisa nae aliamua kuja na kuongea  nakuweka picha za chat  zinazoonyesha mazungumzo yake na zamaradi na kwa jinsi gani mwanamama huyo alimtafuta na kuomba ushauri wa nini cha kushona siku hiyo.

 

 

Hamisa na Zamaradi Ndani Ya Bifu Zito

Mtangazaji na mfanyabiashara Zamaradi Mketema ameingia ndani ya bifu zito na Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz Hamisa Mobetto wameingia kwenye majibizano makali Kwenye mitandao ya kijamii.

Kisa cha majibizano hayo ni baada ya kuwepo kwa tuhuma za Zamaradi kuiba idea ya mshono wa nguo yake aliyovaa Kwenye 40 ya mtoto wake kutoka kwa Hamisa Mobetto kisha kwenda kushona kwa fundi mwingine bila hata taarifa.

Baada ya tetesi hizo Zamaradi aliandika Kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hakuchukua idea ya mshono kutoka kwa Hamisa  bali yeye ndiye alimpa Hamisa mshono lakini alishindwa kushona kwake kutokana na muda.

Nimeambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine, na nimeshangazwa na uongo mkubwa wa namna hii, Mimi ndio nimetuma mshono kwake na sio yeye, hakuwa anaufahamu kabla, kutokana na kudai kupishana na muda nikaamua nikashone kwingine na zaidi swala la kushona kokote ni uamuzi wangu since sijachukua mshono wa mtu”.

Baada ya povu hilo la Zamaradi, Hamisa na yeye alimwaga povu zito sana na kuandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

https://www.instagram.com/p/BmdYoQZlCv_/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1as2jxfy2tqvq

Zamaradi Amtumia Ujumbe Mzito Shamsa Ford

Mtangazaji na mdau mkubwa wa Bongo movie Zamaradi amemtumia ujumbe mzito msanii wa Bongo movie Shamsa Ford katika siku yake ya kuzaliwa.

Siku ya jana ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Shamsa Ford wasanii mbali mbali walimtumia salamu za pongezi na mmoja kati ya watu hao ni Zamaradi ambaye ni rafiki wa karibu wa Shamsa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zamaradi alifunguka na kuelezea mapenzi yake mazito kwa Shamsa na hata kudai wana uhusiano zaidi ya urafiki ambapo alimtaka asimuite rafiki bali ndugu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zamaradi aliandika;

https://www.instagram.com/p/Bl47YgNgT_n/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=6j5t59lks2z3

Zamaradi Afunguka Kuhusu Mapenzi na Mume wake, ni Kila Kitu Kwake.

Ikiwa jana ni siku muhimu kwa familia ya zamaradi mketema kutokana na sherehe kubwwa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu  ya 40 ya mtoto wake aliyejifungua siku kadhaa zilizopita, mwanadada Zamaradi alipata fursa ya kumtambulisha mumu wake katika sherehe hiyo na kujikuita akifunguka mengi kuhusu baba huyo.

Akiongea mbele ya umma Zamaradi anasema kuwa mume wake ni kama baba kwake kutokana na ukweli kuwa amekuwa  mtu muhimu , anaemuelewa na kumjali kwa kila kitu tangu amekuwa nae  katika maisha yake.

Zamaradi pia amesema kuwa siri kubwa ambayo wengi inawezekana walikuwa hawaijui ni kwamba , mume wake ndie alikuwa akimkanda na maji ya moto kwa kipindi chote alichojifungua mtoto wake huyo wa kiume.

Zamaradi pia amesema kuwa kwake sio shida kuzaa na kuendelea kuongeza familia na mwanaume huyo hata kama anawatoto watatu tayari.

Amenikubali kama nilivyo na kunipenda na mimi nimemkubali kama alivyo na kumpenda pia,mpaka hapa tulipo tuna familia pamoja na tunategemea kuongeza familia pamoja ,nataka tu kumwambia kuwa nina kupenda sana na asante kwa kila kitu.

kitu ambacho wengi hamjui ni kwamba kipindi chote cha kujifungua nimekuwa nikikandwa na yeye na hii kutokana na kwamba hakukuwa na mzazi wa kunikanda mimi, wazazi wangu wote walishatangulia mbele ya haki.

Picha Za 40 Ya Mtoto Wa Zamaradi Mketema

Siku ya jana tarehe 25/7 Mtangazaji wa Wasafi Tv, Zamaradi Mketema alifanya 40 ya mtoto wake wa mwisho anayeitwa King Salah ambaye alikuwa anafikisha siku 40 tangu azaliwe.

Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Zamaradi maeneo ya Mbezi Beach na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa Bongo fleva na hasa Bongo Movie.

Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Diamond Platnumz, Jokate, Uwoya, Wema, Kajala, Irene, Harmonize, na wengineo.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio hayo;

.

 

Zamaradi Aomba Kutohusishwa na Lolote Kuhusu Kesi ya Mtoto wa Muna.

Mwanadada Zamaradi ambae alikuwa mstari wa mbele na kuhamasisha watu katikakuchangishwa pesa kwa ajili ya kumsaidia mtoto wa Muna ili kupata pesa kwa ajili ya matiabu amewaomba mashabiki na watu katika mitandao kutomhusisha na kitu chochote kinachoendelea hasa kesi iliyopoa kati ya wanafamilia ya kugombea mwili wa marehemu  Patrick.

Zamaradi ambae anasema aliguswa na ugonjwa wa mtoto akiwa kama mama na alisikia uchungu hivyo kujitolea kufanya aliloweza kulifanya lakini kwa kuwasiliana na mama wa mtoto anasema kuwa mgogoro wa kfamilia unaoendelea yeye hajui chochote hivyo anaomba watu wasimhukumu wala kumuingiza katika maswala hayo.

ikumbukwe kuwa kipindi mtoto wa muna anaanza kuumwa zamaradi alikuwa mtu wa kwanza kuomba wadau na mshabiki walioguswa na maumivu ya mtoto huyo kuchangia ilikumsaidia mama huyo katika mzigo mkubwa wa matibabu lakini baada ya kutokea kwa msiba na mkanganyiko baina ya wazazi wa pande mbili zamaradi amekuwa akihusishwa na kutuhumiwa kujua baadhi ya mambo kuhusu migogoro hiyo.