Vita ya Hamisa na Zari Yahamia Kwa Tunda

kwa muda mrefu wanamaa wawili hamisa mobeto na zari the bossy wamekuwa katika malumbano katika mitandao ya kijamii kuhusu nani kuwa juu zaidi ya mwenzie huku wote wakiwa wamezaa na bwana mmoja msanii mkubwa duniani diamond platinumz.

Mgogoro huu unaonekana kuendelea chini chini  lakini safari hii inaonekana kuhamia kwa mtu mwingineambapo   ni kati ya Hamisa Mobeto tena na Tunda ambae alishawahi kuwa video queen wa Diamond tena katika moja ya kazi zake.Siku kadhaa zilizopita kulikuwa na tetesi katika mtandao wa kijamii kuwa video queen huyo (Tunda) anatoka na msanii Diamond ingwa yeye mwenyewe alikanusha kabisa tetesi hizo.

Lakini mambo yanazidi kuwa moto tena hasa baada ya Tunda kuweka picha katika ukurasa wake wa instagram huku akiweka caption ambao inasemekana kuwa inalenga kutupia dongo kizani kwa Hamisa Mobeto.A

Alipoweka picha hiyo ambayo ilimuonyesha yupo katika kibao kata cha rafiki yake, ambapo hata Hamisa alihudhuria, Tunda aliandika caption ya kusema  “ebu angalia yule kinganganizi asiyejua maana ya kukataliwa na mwanaume‘ Maneno haya yanasemekana kumlenga Hamisa ingawa Tunda mwenyewe hakutaja jina la kinganganizi huyo.

lakini hata hivyo , inaonekana kuwa kwa muda sasa tunda amekuwa akiposti vitu vya kutaka kumuumiza roho hamisa mobeto , kwa mfano siku ya kuzaliwa kwa zari, tunda aliposti picha ya mwanamama huyo na kuandika “happy birthday mama T, wifi wa Taifa uliethibitishwa na Tbs,#nikiwamkubwanatakakuwakamawewe” Aliandika Tunda.

Ingawa mpaka sasa haijathibitika moja kwa moja lakini habari za chinichini zinasema kuwa tunda ana uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond.Lakini pia hata baada ya drama hizo zinazoendelea katika ukurasa wa instagram wa socialite tunda , hamisa hajataka kujibu chochcote kuhusu tuhuma hizo na wala kujibizana na mwanadada huyo.

Tunda na Hamisa wote kwa pamoja walishawahi kufanya kazi na Diamond katika moja ya nyimbo zake za mwaka uliopita wakiwa kama video queens katika wimbo wa Salome.

 

Esma Afunguka Sababu ya Kutohudhulia Party ya Zari S.A

Kumekuwa na maswali mengi watu wakijiuliza kuwa kwanini katika party kubwa ya familia ambayo Diamond aliifanya yeye na familia yake huko nchini Afrika ya Kusini dada yake Esma hakuwepo katka party hiyo na holidays zote ambazo familia hiyo ilisherekea nchini humo.

Ingawa kumekuwa na taarifa za chini chini kuwa hakuna maelewano mazuri kati ya Esma Platinumz na mwanamke aliyezaa na kaka yake huyo ( Zari ) kwa kipindi kirefu tangu kipindi ambacho Hamisa Mobeto  (mwanamke mwingine wa Diamond) alipojifungua ambapo dada wa msanii huyo alikuwa akionekana yupo karibu sana na Hamisa na kumuhudumia kwa kila kitu na kumfanya Zari kuchukia kitendo hicho na ndio maana wawili hao mpaka sasa hivi na kwamba Esma hajataka kwenda kwa sababu wamekuwa hawako vizuri kimahusiano.

Hata hivyo baada ya maneno hayo kusambaa sana ,kampuni ya habari ya GPL, iliamua kumtafuta Esma Platnumz na kumuuliza juu ya habri hizo ambazo zinasemekana kuwa zilisemwa na mtu wa karibu kabisa wa familia yao kuhusu kutoelewana kwake na wifi yake Zari na sababu ya yeye kutokuhudhuria katika party ya siku ya kuzaliwa na mtoto wa kaka yake ni kutokuelewana kwake na Zari.

Nisingeweza kuiacha biashara yangu na duka langu ambalo ni elifungua tu hivi karibuni eti niende kwenye pati,wateja wangu wasingenielewa kabisa  na ningerudi ingechukua muda mrefu kidogo kuwarejesha kwakweli.Watu wanapenda kuongea sana lakin ukweli ni kwamba mimi na Zari  hatuna tatizo lolote , kama hauamini siku nyingine akiandaa pati ntaenda tu. Alifunguka Esma Platinumz

Hata hivyo siku ya mkesha wa mwaka mpya Zari alipost video akiwa na wifi yake huyo na kusema kuwa wanavuka mwaka mpya kwa pamoja huku wakionekana na furaha.

Zari amjia juu mzazi mwenzie

Ikiwa hata interview haijaisha kati ya Diamond na kituo cha habari cha Clouds Media Zari amjibu mzazi mwenzie kuhusu yale aliyokuwa anayasema leo katika interview iyo.Diamond ambae leo ameamua kusema ukweli kuhusu tetesi zilizokuwa zinasambaa mitandaoni juu ya mtoto wa video quen Hamisa Mobeto .

Diamond amekiri kuwa alitembea na Hamisa na amepata mtoto nae  na kusema kuwa alishaongea na mzazi mwenzie (Zari) na kwamba mama wa watoto wake yuko sawa na walishayamaliza lakini Zari ameonekana kupinga maneno hayo .

Katika ukurasa wake wa Snapchat Zari aliandika “haha… u playing yourself ..the lies telling about me knowing about your side chic..try and fix your mess and stop  with lies .Me being quite doesnt mean am stupid .Be very careful with your words’ aliandika zari akikanusha kuwa kitendo cha Daimond kusema kwa yeye alikuwa anajua juu ya yeye kuwa na mahusiano na Hamisa ni uongo.

Hata hivyo Zari anaongezea na kusema kuwa  kitendo cha yeye kukaa kimya ni kwa sababu yeye ni mama wa watoto wake ” i may be the mother of your kids  and that’s the reason am keeping silence &respect. You might want to Google about ‘Defarmation of character law suit’ Dont try me” aliandika Zari

Majibu haya yamekuja baada ya Diamond kukubali na kuomba msamaha kuhusu ukweli kuwa mtoto alizaliwa kwa Hamisa Mobeto ni wakwake lakini alikaa kimya ili kuweka kwanza mambo sawa ndipo atangaze.

Akiwa bado katika  mahujiano Diamond aliulizwa kuhusu maneno hayo aliyopost mama wa watoto wake , na alijibu hivi “Anavyosema hivyo namuelewa  anachokizungumza,najua hawezi kuwa sawa kwa muda huu, lakini pia yapo baadhi ya mambo nimeyazungumza hapa  ,  hakuwahi kuyasikia.” alipoulizwa ni mambo gani alijibu vitu kama ela za matumizi , kumnunulia gari Hamisa ni vitu ambavyo hakuwahi kumwambia Zari ivyo ana haki ya kuijsikia vibaya.

Zari na Diamond  wamekuwa katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitatu na wamefanikiwa kupata watoto wawili wakike moja na kiume mmoja.

Harmonize amtetea Zari vikali

Harmonize amemtetea Zari dhidi ya madai kuwa anaponda raha siku chache tu baada ya kumpoteza mama mzazi. Zari, Diamond na Harmonize walionekana Mombasa, Kenya wakijivinjari jambo ambalo halikuwapendeza baadhi ya watu.

Harmonize ata hivyo alimtetea Zari kwa kusema kuwa mtu akipata msiba alafu akapelekwa sehemu nzuri kwa ajili ya kufurahi ni kitu cha kumshukuru mwenyenzi Mungu. Alisisitiza kuwa maisha lazima yaendelee ata mtu akipoteza wapenzi wake.

Harmonize na Zari

“Kwa sababu haikuwa rahisi, unajua kufiwa na mazazi sio kitu kidogo. Tumefika (Mombasa) tumemkuta yupo fresh, yaani kasharidhika na matokeo kwa sababu anajua hakuna binadamu atakuja kuishi milele. Kwanza ukiona mtu anazungumza hiyo ujue haijui dini, kwa sababu dini imeandika kila mtu atakufa, kifo ni kitu cha lazima, ukiwa unaijua dini huwezi kuhofia suala la kifo. Mtu kafariki ni lazima uumie ila ni lazima maisha mengine yaendelee kwa sababu hata ukae ndani miaka sita hawezi kurudi,” Harmonize ameiambia kipindi cha XXL ya Clouds FM.

 

Hii ndo sababu Diamond alirejea Tanzania kwa upesi baada ya kuzika mamake Zari

Diamond alisafiri kuelekea Uganda kwasababu ya mazishi ya mama mkwe wake ambaye aliaga dunia Alhamisi wiki jana akipata matibabu hospitalini.

Mamake Zari – Halima Hassan alizikwa Ijumaa kulingana na itikadi za Kieslamu ambayo inasema wafu wanafaa kuzikwa chini ya masaa 24 baada ya kifo.

Mama mkwe wa Diamond alizikwa Kalama, mji ambao uko katikati ya Uganda. Baba Tiffah alihudhuria mazisho hio huko Kalama.

Diamond akiwa kwa mazishi ya mama mkwe wake

Staa huyo hata hivyo aliabiri ndege kurudi Tanzania siku hio hio ya Ijumaa baada ya mwenda zake kuzikwa. Diamond alirejea Tanzania kwa upesi kwasababu alikua na show Jumamosi pale Leader Club.

“Mitihani ni sehem ya Maisha na Huletwa na Mwenyez Mungu , na Siku zote huletwa kwa sababu, na ndiomaana tumefunzwa kushukuru kwa kila jambo….. Allah nakushkuru kwa yote, Nakushkuru kwa kunifikisha Uganda na Kumaliza kila jambo salama….Naomba pia Uniongoze katika safari yangu hii ya sasa ya Kuelekea Dar es Salaam….na unitie nguvu siku ya kesho nikiwa kazini pale Leader Club… ? @mama_dangote,” Diamond aliandika.

Diamond na mamake wakiwa wanarejea Tanzania

 

Zari azua utata kwa kufanya hili kwenye kaburi la Ivan Ssemwanga

Zari Hassan amezua utata baada ya kuonekama akikaa juu ya kaburi ya aliyekuwa mume wake wa kitambo – Ivan Ssemwanga.

Ivan alifariki Mei akiwa Afrika Kusini alipokuwa akipata matibabu, mzazi mwenza wa Zari alizikwa kwao Kayunga, nchini Uganda.

Hatua ya Zari kuketi kwa kaburi ya Ivan imezua kelele kwenye mtandao wa jamii kwani kuna wale wanasema Zari haeshimu mwenda zake.

ray_officially: sasa huyu cameraman/women ulimwambiaje twende kwenye kaburi la ivan unipige picha au ulimuambiaje jaman@zarithebosslady

wisdomnelsonsalome: Jamani, kila mtu anastaili yake ya kuishi, unaweza ukawa na pesa lakini ukatumia kwa akili, wengine wakipata pesa anawaza kubadili nguo na mikoba, msimuhukumu mtu kwakile alicho penda. Wingine kutwaa kwenye majumba ya kupanga afu unamdc mwenzio kwann analife style ile ile, mwacheni boss Lady afanye anachopenda, mbona ninyi

homa_ya_jiji__: Daa hii picha inaujumbe mpana sana

dianamtenga: Wabongo wanafki jmn..watu huwatunaenda kuzika makaburini nawatu wa nakaa juu yamakaburi mara kibao..ila leo amekaa zari bc nizambi

 

Zari asherekea ushindi wa Rayvanny

Rayvanny aliwasili Dar jana kutoka Marekani ambapo alituzwa katika tuzo la BET. Muimbaji huyo alishinda katika kitengo cha Best International Viewers Choice Award.

Zari, ambaye hakua amesema lolote kuhusu ushindi wa Rayvanny, alisherekea ushindi wa Ray kwa kumpongeza kwa kupeleka Afrika Mashariki katika kiwango kingine

“Traffic imepunguka? We are so proud of you, you took East Africa and Africa in general on another level regarding the music industry. Be blessed @rayvanny cc @diamonplatnumz the Godfather of @wcb_wasafi where hits? are made,” Zari aliandika.

Wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki walimpongeza Rayvanny kwa ushindi wake. Jua Cali kutoka Kenya alisema ushindi wa Rayvanny unaupa sifa muziki wa East Afrika kwa kuutangaza zaidi.

“Unajua dream yetu sisi wote ni kupeleka ngoma za East Afrika huko nje. Unajua competition ziko nyingi sana, tunapigana na watu wa South Africa, West Africa, Marekani, watu wa Europe and the moment kuna msanii wetu anashiunda tuzo kama hiyo, kwa sababu hiko ni kitu kikubwa sasa kinaweka East Afrika mahali pazuri especially kwanza kiswahili. Unajua mimi ni mtu wa wa Kiswahili so nikiona msanii anaimba kwa Kiswahili na ameshinda inapendeza sana,” Jua Cali alisema akiwa katika Citizen Radio.

Jua Cali

 

“Sina ukaribu wa kihivyo na Zari” Jacqueline Wolper afunguka kwanini hakumfariji Zari Ivan Ssemwanga alipofariki

Watu wengi akiwemo Wema Sepetu walimfariji Zari Hassan alipofiwa na mmewe wa kitambo Ivan Ssemwanga. Lakini Jacqueline Wolper alishindwa kumfariji Zari.

Lakini ni kwanini Wolper hakuenda kumfariji Zari? Akizungumza na Wikienda, Wolper alisema kuwa Zari na yeye si marafiki wa karibu.

Ivan na Zari

Mrembo huyo pia alisema Ivan alipokufa alikuwa nchini Burundi alikokwenda kwa ajili ya kuchukua mzigo wa dukani kwake hivyo alikuwa bize na hata kama angekuwepo Tanzania bado hangeenda kumfariji Zari.

“Nilikuwa bize na biashara na hata kama isingekuwa hivyo nisingeenda kwa sababu sina ukaribu wa kihivyo na Zari bali siku zile kwenye video iliyosambaa nilikuwa namtetea kwa sababu sipendi mtu aonewe, yaani watu wanamweka mitandaoni amezeeka wakati ukimuona live ni mzuri na mrembo kabisa, sipendi uonevu katika maisha yangu, mimi ni mtetezi wa wanyonge, sema watu hawanijui wananichukuliaga tofauti,” alisema Wolper.

 

 

Diamond afunguka kuhusu mimba ya Hamisa Mobeto na vita yake na Zari

Ujauzito wa Hamisa Mobeto umezua utata kwani wambeya wanadai kuwa Diamond Platnumz ndo amempachika mimba mrembo huyo.

Wiki jana mbeya Soudy Brown alimpigia simu mamake Diamond Sanura ‘Sandra’ Kasim kudhibitisha kama ni ukweli kuwa Hamisa Mobeto amebeba mtoto wa Diamond tumboni.

Soma pia: “Napatana na Zari aliyeniletea watoto hao wengine siwajui” Mamake Diamond amkana Hamisa Mobeto

Akiongea katika kipindi cha XXL ya Clouds FM jana, Diamond alikana kuwa yeye ndo baba wa mtoto aliye tumboni mwa Hamisa Mobeto.

“Hizo zote ni za uongo, mama T pia anajua ni story ya uongo. Naskia kwamba ni mjamzito, sasa mjamzito pia watu wameunganisha hio story ikawa ni mimba yangu. Story zinazungumzwa mimi siwezi kufanya kitu chochote,” Diamond alisema.

Staa huyo pia aliguzia ishu ya Zari kuonekana akiongelea kwa spa na mwanaume aliyekuja kugunduliwa kuwa binamu wa Ivan Ssemwanga.

Diamond alieleza kuwa alikusudia kuweka picha ya Zari na Edwin Lutaaya kwenye Instagram kwani alidhani kuwa mkewe ako na uhusiano wa kimapenzi na Edwin.

“Nlikua nimekusudia, unajua…upande mwingine mimi ni binadamu kama binadamu wa kawaida mimi pia nakua naskia uchungu na maumivu. Na katika mahusiano yangu yote nshakuwa nayo basi mahusiano ya Zari nimejitahidi kujitoa sana kwa kila hali na mali. So nlikutana na ile picha kwenye mtandao sikuelewa…mi kwanza nkajua ime editiwa. Ehh nkampigia simu nikamwambia “mbona kuna picha nimeiona hivi na hivi”. Akaniambia “bwana huyo ni shemeji wangu, hapo pia tulikua na wife wake lakini kutokana na kwasiko kwa maji inaonekana kama kanikumbatia lakini haikua hivyo”. Mi nikapanic nkaona kama huyu mchongo tu yani ni kama anajifanya, anajitetea. Nkamwambia “kwa hio mbona hujaiposti kwenye account yako imetokea kwa watu wengine tu, imekuaje?”. Nkamwambia “ulikua unataka boost, unataka kiki au vipi kwasababu mimi ntakupa kiki ntakupost kabisa ili isambazike mtu aone dunia, si unataka kila mtu aone?” Kwa hivo nkaposti, kwa hivyo baada ya kuposti alikua ofisini akarudi haraka amekuja amepagawa ndo kaja na zile picha “ si unaona nlikua na huyu wife wake na nini na nini…na huyu wife wake ndo alinipiga picha kwa hivyo na hivi na hivi…. Baada ya kunionyesha ndo nkatoa ,” alisema Diamond.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=xnxcRkq6_34