Zari: Kamwe Siwezi Kumuanika Mwanaume Wangu Mtandaoni

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakuja kumuanika tena Mpenzi wake kwenye mtandao.

Baada ya kuachana na Diamond mwaka mmoja uliopita Zari hajawahi kumuweka wazi mwanaume ambaye yupo naye kwenye mahusiano ingawa ameshawahi kusema yupo kwenye mahusiano.

Zari

Zari alifikia hatua ya kuweka wazi hayo alipoulizwa kama kweli hana mpango wa kuolewa na Diamond na atamuanika lini mwanaume anayempenda am­bapo alieleza kuwa mwanaume wake si wa mitandao ya kijamii.

Mume wangu siyo wa social media, ni mume wangu siyo wetu“.

Zari ambaye ana watoto watano wawili kati yao amezaa na Diamond baada ya kuachana na Mbongo Fleva huyo amewahi kuhusishwa kimapen­zi na mwanaume anayeitwa Brian wa nchini Uganda ambapo mara mbili to­fauti alionekana kupiga naye picha za ukaribu lakini mwenyewe alidai kuwa ukaribu wao huo ni wa kikazi tu.

Tangu Diamond aachane na Zari ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wanawake kadhaa ikiwemo mama Watoto Wake Hamisa Mobetto Lakini pia Kim Nana na Sasa mrembo kutoka Kenya Tanasha.

“Hamisa Ndio Kiboko Ya Zari”- Maimartha

Mtangazaji mkongwe nchini Maimartha Wa Jesse amerudi tena kwenye headlines za mitandao ya kijamii Baada ya kutoa kauli tata ya Hamisa Mobetto dhidi ya Zarinah Hassan.

Siku mbili zilizopita mlimbwende Hamisa Mobetto alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa na mmoja kati ya watu waliojitokeza kumtakia Birthday njema n Maimartha.

Maimartha Kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuandikia ujumbe ambao ulizua maswali kwani alimuhusisha Mobetto na adui yake namba moja Zari ambapo aliandika maneno haya:

Happy Birthday Hamisa Kiboko ya Zari, ulijua kuwaparaganisha na Chibu…Zari alitamani akumeze ishi maisha dill yenye mafanikio”.

 

Maimartha Anyanyua Mikono Kwa Zari

Mtangazaji mkongwe na msanii wa Bongo movie Maimartha wa Jesse ameibuka na kumvulia kofia    mwanamama mfanyabiashara Zarinah The Bosslady Baada ya Kuvaa kiatu cha bei kupitiliza.

Kiatu hicho ambacho ni brandi ya Kanye West linalotajwa kugharimu dola 645 za Kimarekani (takribani shilingi milioni 1.5) wamekuwa wakionekana wamelivaa mastaa wakubwa duniani kama Rihanna na Kim Kardashian hivyo kuvaliwa na Zari kumewashtua wengi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Maimartha amesema kuwa bei ya buti hilo limemshtua lakini anaamini Zari ni mwanamke wa shoka hivyo Ana  uwezo wa kumiliki kiatu hiko:

Zari si mwanamke wa mchezo mchezo, kwa hili buti lake amewakalisha wengi, mara nyingi akiweka mavazi na bei zake watu husema ni feki lakini kwa kiatu hiki naamini bei yake ni ya ukweli.”

Zari Atangaza Zawadi Kwa Mashabiki Zake Uganda

Mwanamama mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda na Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ ametoa  zawadi Nono kwa mashabiki zake nchini Uganda.

Zari ameyafanya hayo muda mfupi baada ya kupata zali la kuwepo katika vivutio vikubwa vya utalii nchini humo akiwa kama balozi wa utalii ambapo atatembelea katika mbuga kubwa za wanyama pamoja na chanzo cha Mto Nile pande za Jinja.

Akizungumzia ishu hiyo ndani ya Hoteli ya Serena nchini Uganda, Zari alisema ili kuwavutia watalii na watu wengine ameona kuwa na kampeni maalum ya kuwashirikisha mashabiki wake na kampeni hiyo ameiita jina la Tulambule Ne Zari akimaanisha Tutembee Na Zari.

Niambie sehemu unayopenda kutembelea Uganda, unaweza ‘ku-google’ vivutio vyote vya utalii Uganda na ukasema ni sehemu gani unapenda kutembelea,” alisema Zari na kuongeza: “Nitatoa ofa ya gharama zote za safari na ujue tu mimi ni Boss Lady kwako na kwa mwenzako au familia yako”.

Hili ni moja tu Kati ya madili  ambayo Zari  amekuwa akiyapiga tangu aachane na aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz Lakini pia Kumekuwa na tetesi za ubalozi wa nchi unaoweza kumuangukia mrembo huyo.

Zari Amchana Diamond Baada Ya Kugoma Kuwaona Watoto Wao

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameingia vitani na mzazi mwenzake mfanyabiashara Zarinah Hassan baada ya kumtuhumu kwa kutokwenda kuwaona watoto wao na kutojua wanaishije mpaka hivi sasa.

Diamond na Zari walikuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka minne na zaidi lakini mwaka huu mwezi wa Pili Zari alivunja Mahusiano yao baada ya kuchoshwa na michepuko ya Diamond lakini alisisitiza kuwa watabaki marafiki kwa ajili ya watoto wao.

Lakini sasa urafiki huo umeelekea ukingoni kwani Zari amempa makavu Diamond na kumtaka aende akawaone watoto wao kwani watoto hawajamuona Baba yao kwa miezi kadhaa sasa.

Zari amemtolea povu hilo Diamond Kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo amewatolea maneno pia mameneja wake na kuwataka wamshauri msanii wao akawaone watoto wao kwani watakuwa wameshaanza hata kumsahau Baba yao:

 

Zari na Watoto Wake Waendelea Kula Bata Dubai (Picha)

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameendelea kula bata Dubai na watoto wake.

Zari ameenda Dubai kwa ajili ya mapumziko ya Pasaka pamoja na familia yake ambapo ameongozana na watoto wake watatu wakubwa na mpiga picha wake.

Hizi ni baadhi ya picha za Zari na familia yake wakila bata:

 

 

 

 

 

 

.

Faiza: Ina Maana Watanzania Wote Hamkuwaona Mpaka Mkampe Dili Zari

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally amerudi tena Kwenye headlines baada ya kutoa povu zito Baada ya Zari kutangaza kama balozi mkuu wa bidhaa za Softcare.

Siku ya jana Zari pamoja na kampuni ya Softcare walifanya mkutano na waandishi wa Habari ambapo walimtangaza Zari kama Balozi wa kuuza Bidhaa hizo ambazo ni pampas za watoto.

Lakini dili hilo lilizua minong’ono kutoka kwa watu hasa kwa sababu kampuni ni ya Tanzania lakini Zari ni Mganda anayeishi nchini South Africa kwaiyo inakuwaje waache mastaa wote wa hapa Tanzania waende Uganda.

Faiza alitoa povu zito juu ya hilo na kuihoji kampuni hiyo kwa nini imewaacha wanawake wengine wengi ambao ni mastaa hapa Tanzania ambao nao wengeweza kufanya kazi hiyo na kumchukua mtu ambaye hata sio Mtanzania.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Faiza alitoa povu hili:

Hii sio mara ya kwanza kwa Watanzania kulalamika baada ya Zari kupewa Dili la kutangaza bidhaa za Tanzania alishawahi kuwa balozi wa Danube na Vodacom.

Zari Asaini Dili Nono na Kampuni Ya Softcare

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amesaini dili nono na kampuni ya Softcare nchini Tanzania.

Zari aliingia nchini Tanzania siku ya Jumanne na kufikia Katika hoteli ya Hyatt Regency na fununu za ujio wake zilisambaa. Zari alitangaza kuhusiana na ujio wake kupitia ukurasa wake wa Snapchat.

Zari amepata dili hilo la kuwa Brand ambassador (Balozi mkuu wa bidhaa) wa pampers za watoto kutoka kampuni ya Softcare huku thamani ya dili bado  haijawekwa wazi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari aliandika ujumbe huu kuhusiana na dili hilo alilo Saini:

 

Zari Amedai Kuwa Hawezi Kuzaa Tena na Diamond, Akitaka Akazae na Wanawake Wengine (video)

Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari the Bosslady’ amefunguka na kudai kuwa hawezi kuendelea kuzaa na mpenzi wake na mzazi mwenzake mwanamuziki Diamond Platnumz na akiona anahitaji watoto zaidi akazae na mwanamke mwingine.

Zari na Diamond walipoanza mahusiano yao kimapenzi miaka kama minne iliyopita walianza kwa kasi ya ajabu kwani mara tu baada ya kuwa pamoja kwa miezi michache Zari alibeba ujauzito na kujifungua mtoto wao wa kwanza Tiffah na miezi michache baadae alijifungua mtoto wao wa mwisho Nillan.

Miezi michache iliyopita Zari alipitia kipindi kigumu kwenye mahusiano yake na Diamond baada ya kugundua kazaa tena na mwanamke mwingine ambaye ni Hamisa jambo lililopelekea watu wengi kudhani ataachana na Diamond lakini wamesameheana na wapo wote pamoja.

Lakini pamoja na kwamba bado wapo wote Zari amesisitiza kuwa hawezi tena kuzaa na Diamond na kudai endapo atataka mtoto mwingine basi yupo huru kwenda kuzaa na wanawake wengine lakini sio yeye.

Zari alifunguka hayo yote kwenye mahojiano aliyofanya na Milard Ayo TV:

Kwa upande wangu mimi wametisha siwezi kuongeza wengine lakini kama Diamond anataka watoto wengine anaweza akawa nao wengi atakavyo hilo ni tatizo lake sio langu mimi Niko fresh tu”.

 Zari ambaye tayari ana watoto watatu wakubwa wa kiume aliozaa kwenye ndoa yake na Ivan kwaiyo kufanya jumla ya watoto watano alionao hivi sasa.

Mimi na Hamisa sio Marafiki- Zari

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz Zari the Bosslady ‘Zarinah’ amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na hasimu wake namba moja Hamisa sio marafiki na wala hawawezi kuwa marafiki.

Warembo wao wawili wapo kwenye bifu kali baada ya Hamisa kuzaa na Diamond miezi michache iliyopita. Tangu kipindi cha nyuma kabisa kulikuwa na tetesi za Diamond kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Hamisa kitu ambacho Diamond alikikataa kata kata lakini mara tu baada ya habari za ujauzito kuenea na hatimaye mtoto kuzaliwa Diamond alikiri kumsaliti Zari na kuzaa na Hamisa.

Lakini baadae Zari na Diamond walisameheana na kuendelea na mahusiano yao lakini tangu kipindi hicho Zari na Hamisa wamekuwa maadui na bifu hilo lilidhihirika zaidi wiki iliyopita pale wote wawili walipoandaa party zao siku moja nchini Uganda.

Kwenye interview aliyofanya na Millard Ayo Tv Zari amefunguka kuhusu hali iliyopo sasa na hasimu wake Hamisa Mobetto:

Mimi binafsi sina ugomvi na Hamisa chochote kilichotokea kati yake na Diamond watajuana wenyewe mimi hivyo vitu havinisumbui wala sijali nina maisha yangu nina nina watoto wangu nina kazi zangu nina mambo mengi ya kufanya sawa kina mambo yalitokea kati ya Baba Tiffa na Hamisa lakini natakiwa nijiulize nataka nifike huko? Yaani nimuache mume wangu kwa ajili yake? Hakuna kitu kama hicho lakini mwisho wa siku mwanaume ni mwanaume utampa kila kitu lakini akitoka atatfuta hata mifupa hivyo sina time ya kumuangalia anachepuka na nani sijui. Ila mimi  na Hamisa sio marafiki na hata tukikutana siwezi hata kumsalimie”.

 

 

Zari na Hamisa Wameingia Tena Kwenye Bifu Kali Baada Ya Kurushiana Maneno Mazito Mtandaoni

Wazazi wenza wa Msanii Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto wameingia tena kwenye bifu zito baada ya kila mmoja kumrushia maneno mwenzake mtandaoni.

Kisa cha ugomvi huo kilianza siku chache zilizopita baada ya Zari na Hamisa kujikuta wana sherehe siku moja nchini Uganda Jana hapo ndipo mashindano yalipoanza huku kila mmoja akijinadi atakuwa juu zaidi huku wakisaidiwa na timu.

Party hizo mbili zilifanyika Jana usiku kwenye kumbi mbili tofauti lakini kwa wakati mmoja. Baada ya party hizo picha zilianza kusambaa mtandaoni huku kila mmoja akijitahidi kuonyesha kuwa alikuwa na nyomi kubwa kuliko mwenzie.

Baada ya muda warembo hao wawili walianza kurushiana maneno katika mtandao wa Snapchat na Instagram huku kila mmoja  akimtambishia mwenzie kuwa amepata mafanikio zaidi ya mwenzake lakini pua walifikia hadi hatua ya kurushiana maneno ya kashfa.

Zari ameibuka akumrushia maneno haya Hamisa kupitia kurasa yake ya Snapchat:

Kuna tofauti kubwa Kati ya tembo na mbu, baraka juu ya  baraka Asante Mungu, Watu wenyewe ni maslay cartoons, wezi wa wanaume za watu wanataka waishi kwa kutegemea child support lakini wapi hawawezi kushindana na mimi, wameenda mpaka kisutu lakini wameambulia patupu”.

Baada ya kurushiwa maneno hayo Hamisa alishindwa kuvumilia kwani na yeye amefunguka ya kwake na kumrushia Zari madongo:

Siwezi kubishana na bibi yangu, Mimi nina umri wa binti yako wa kwanza unemzidi mama yangu miaka 3…Mama yangu amenifundisha kuheshimu wakubwa walionizidi alafu ungejiamini wako angetulia…alaku wewe endelea kulilia kuvalishwa pete wakati mwenzako mume wa mtu tayari”.

 

Hamisa na Zari Ndani Ya Uganda Siku Moja.

Imepita muda mrefu zile chokochoko za wanawake wawili Zari The Bossy pamoja na Hamisa Mobeto  zimetulia katika mtandao na kukawa na matumaini kuwa wasichana hao wawili ugomvi wao utakuwa umeisha , lakini kumbe sio kama vile watu wanavyofikiria kwa sababu inawzekana hichi kinachokuja sasa hivi kikawa ni  kikubwa zaidi.

Ni muda mrefu tangu Zari The Bossy Lady atangaze kuwa atakuwa na party yake inayifanyika uganda kila mwishoni  mwa mwaka inayojulikana kama zari all white party, na kweli party hiyo imeshaanza kuwa na maaandalizi yake nchini Uganda, lakini kitu cha kushangaza na kujiuliza ni kwamba Hamisa pua ametangaza kufanya party yake nchi Uganda siku moja na ile ambayo Zari anategemea kufanya party.

Tarehe 21 December, Zari atafanya party nchi Uganda na siku hiyo hiyo Hamisa Mobeto mrembo kutoka Tanzania anategemea kufanua party yake nchini humo, hii ina maana gani , je ni kweli kuwa sasa Hamisa ameamua kushindana na Zari mpaka kwenye maswala kama hayo, je anataka kumuaribia soko au waandaaji wa tamsha hilo kutoka Uganda wameona hiyo ndio njia sahihi ya kumzima Zari.

Zari na Hamisa Mobeto waliingia katika bifu zito baada ya hamisa mobeto kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie na Zari ,Diamond Platinumz, ambapo wawili ho walifanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume.

 

Familia Yaingilia Kati Bifu La Zari Na Hamisa

Hakuna ubishi kuwa Zari adui yake mkubwa hivi sasa ni Hamisa hiyo ilianza tangu siku Hamisa alivyoanza kutembea na Diamond huku akijua wazi kuwa ni baba watoto wake.

Bifu hilo lilianza rasmi mwaka 2015 pale ambapo Zari alipata taarifa kuwa Hamisa anatembea na Diamond. Bifu lilipamba moto miezi miwili uliopita baada ya Zari kugundua kuwa Diamond amezaa na Hamisa na hapo walianza kurushiana vijembe mtandaoni

Zari na Hamisa wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii, gazeti la Risasi limeelezwa kwa nyakati tofauti kila mmoja aliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa mzazi mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mtandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao ukizingatia kosa limeshafanyika na amekiri hadharani.

Walichoelezwa ni kwamba tu waache kutupiana vijembe mtandaoni kwani wao hivi sasa hata kama hawata kuwa wake wenza lakini tayari Diamond ana damu yake kwa Hamisa, ameshakiri aliteleza na kujikuta kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kuzaa naye. Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama hataendeleza mahusiano na mwanaye”.

Chanzo hiko ambacho ni mwana familia wa karibu aliendelea kutiririka kuwa sasa hivi wanashukuru Mungu, kwani warembo hao wawili kila mmoja kwa wakati wake ameelewa somo na hivyo kuacha kurushiana maneno maneno kwenye mitandao ya kijamii maana zamani ilikuwa haipiti siku mbili bila kutibuana mitandaoni.

Hamisa Mobetto na Vera Sidika Wavurugana Kisa Zari

Hamisa Mobetto na Mrembo kutoka Kenya Vera Sidika maarufu kama Queen Vee, wameingia katika vita ya maneno mtandaoni kisa ni Zari.

Sakata hili lilianza baada ya Hamisa ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya kukutana na Vera na kumrekodi wakati wanasalimiana na kisha kutuma hiyo video Snapchat. Tendo hilo liligeuka ugomvi kwani inajulikana wazi kuwa Vera ni rafiki kipenzi wa Zari ambaye ni hasimu mkubwa wa Hamisa (kwani wote wamezaa na Diamond)

Baada ya Video hiyo kusambaa mtandaoni mashabiki wa Zari walimjia juu Vera kwa kitendo chake cha kuwa na urafiki na Hamisa wakati ni adui wa shoga yake Zari. Baada ya kuona hilo ndipo Vera alipoingia mtandaoni na kuanza kujitetea kuwa hana urafiki na Hamisa bali alisimama kumsalimia mtu mwingine aliyekuwa na Hamisa na hakujua kuwa anarekodiwa na Hamisa.

Vera amedai hana urafiki na Hamisa na anashangaa kwanini alimpiga picha bila ruhusa.

Baada ya kuona hivyo Hamisa alimjia mjuu Vera na kudai kuwa aache uongo kwani alijua wazi kuwa alimrekodi na kabla hajaituma video ile alimuonyesha na akakubali, pia Hamisa amedai Vera alimuomba amtafutie mashabiki Tanzania pia alimualika Nyumbani kwake akamtembelee yaani kwa kifupi walikuwa mashoga ila saivi anamruka kwaajili anamuogopa Zari.

Hamisa amchana kuwa kwa sababu ana urafiki na Zari hana haki ya kumsema vibaya

Sakata halikuishia hapo kwani Hamisa alimrushia maneno Vera kuwa ni mtu mzima ovyo mwenye maziwa fake na kajichubua na Beta kamsema Hamisa kwa kitendo chake cha kuzaa na wanaume wenye hela ili wamsaidie maishani kwani hana kazi yoyote.

Vera akimchana live Hamisa
Hamisa akimpa makavu Vera

Mpaka sasa Zari hajachangia lolote juu ya bifu hili je unahisi nani yupo sahihi?

 

 

 

Zari Apata Dili Zito na Mercedes Benz

Mfanyabiashara na mzazi mwenzie na mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan maarufu Kama Zari the Boss lady amepata dili zito baada ya kufanikiwa kuwa balozi wa Mercedes Benz.

Zari amefanikiwa kukwaa dili la kuonyesha magari aina ya Mercedes Benz kwa ajili ya kampuni ya AMG Performance Center iliyopo nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari aliweka picha tofauti tofauti na kuambatanisha na maneno Amgperfomancecenter is your center for class & state the Art cars. Thank you for the car na nyingine #closedealsinheels

Ingawa Zari hajaweka wazi taarifa zaidi kuhusiana na  dili hilo nono alilolipata ikiwemo ni shilingi ngapi atatengeneza kutokana na dili hilo.

Zari amezidi kuweka mambo take binafsi zaidi name kuelejeza nguvu zake katika kufanya kazi hii imetokana na mambo tote aliyopitia na Diamond ndani ya miezi hii michache.

 

Inawezekana Ni Kweli Diamond Na Zari Mapenzi Yameisha

Tunakuwa na furaha sana katika kumbukumbu za sikukuu zetu za kuzaliwa  tena hasa tunapopata salamu za upendo kutoka kwa watu wetu wa karibu, kwa Dunia hii ya sasa ya utandawazi imekuwa ni kawaida kumtakia kheri ya sikukuu ya kuzaliwa mtu wako wa karibu kwa kuweka picha yake katika mitandao ya kijamii kama Facebook , Twitter lakini hasa hasa ni ukurasa wa Instagram ambao watu wengi kwa sasa  wanautumia.

Tarehe 2  October mwaka huu ilikuwa ni siku muhimu kwa msanii Diamond Platinumz kwa sababu alitimizia miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake,katika siku hiyo Diamond alifanya sherehe mfululizo siku tatu(pre-birthday party) akijumuika na baadhi ya ndugu na marafiki zake wa karibu.Lakini bado kunakuwa na utata kwa sababu tangu  kumeanza kwa shamrashamra hizo, mama mzazi wa watoto wa Diamond hajaonyesha muamko wowote wa kufanya lolote katika siku iyo ya kuzaliwa ya mpenzi wake.

Ikiwa ni kama wiki imepita tangu Zari afanye birthday party yake nchini Afrika ya Kusini , Diamond na team yake nzima ya Wasafi walisafiri na kwenda, je hii haikupaswa kutokea hata kwa Diamond ambae amefanya sherehe hii nchini Tanzania, je ni kweli Zari hakuona umuhimu wa kuudhulia sherehe hiyo , na je kama alikuwa amebanwa na kazi nyingi alishindwa kuonyesha upendo na furaha kwa mzazi mwenzie kwa kumpost katika ukurasa wake wa instagram ilhali akiendelea kupost picha zake? haya  ni baadhi ya maswali ambayo mashabiki wamekuwa wakijiuliza, au zile hasira za Diamond kuzaa na Hamisa Mobeto bado hazijaisha.

Ikumbukwe kuwa kusafiri kwa Diamond kwenda Afrika Ya Kusini ilikuwa ni moja ya vithibitisho kuwa wawili hao walishaweka mambo sawa, sasa je nini kinaendelea,hivi karibuni Zari na Diamond walikuwa katika majibizano ya mtandaoni kuhusu kosa la Diamond kuiri katika media kuhusu yeye kuzaa na video queen Hamisa Mobeto ilhali akikiri kuwa alikuwa anatoa hata matumizi kwa siri bila mzazi mwenzie huyo kujua chochote.

Hakuna aliyeamua kuweka wazi mpaka sasa kuhusu mahusiano yao, lakini kwa kuwa Diamond ni msanii na ana mashabiki pia, mashabiki wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nini kinaendelea kati ya wazazi hao wawili ambao tayari walishaanzisha familia inayowahitaji sana.