“Zamaradi Moyo Wangu Unaumia Kwa Ajili Yako”- Zari

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameibuka na kumtumia salamu za rambi rambi Zamaradi Mketema Baada ya Ruge Kufariki.

Marehemu Ruge Mutahaba alikuwa kwenye mahusiano na Zamaradi Mketema kwa miaka mingi na  kufanikiwa kuzaa naye Watoto wawili wadogo.

Tangu Ruge amefariki Zamaradi amekuwa akionekana mwenye majonzi na hasa kwa sababu baba wa Watoto Wake amefariki.

Zari amemtumia salamu za kumfariji Zamaradi kwa sababu na yeye mwaka jana alifiwa na baba wa Watoto Wake watatu Ivan Semwanga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameweka picha ya Zamaradi na Watoto Wake wakiwa kwenye msiba na kuandika maneno machache “My heart bleeds for you Zama”.

Diamond Hana Pesa, Nimeshakuwa na Wanaume Wenye Pesa-Zari

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ ameibuka na kumtupia dongo zito mzazi mwenzake huyo na kusema hana pesa.

Zari na Diamond walikuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne na walifanikiwa kuzaa Watoto wawili Lakini Penzi Lao liliingia shubiri mapema mwaka jana Baada ya Diamond kuchepuka na Hamisa na kuzaa naye mtoto.

Tangu waachane sio siri Diamond na Zari hawajawahi kuwa na mahusiano mazuri na siku ya Leo ameweka wazi kuwa Diamond hana pesa kama watu wengi wanavyosema.

Zari alifunguka hayo alipoulizwa na shabiki kama Diamond asingekuwa tajiri na maarufu basi Zari asingeweza kuwa naye kwenye mahusiano, Swali ambalo Zari alijibu kuwa Diamond hana pesa.

Siongei haya ili kuonekana na roho mbaya Lakini nimeshawahi kuwa na wanaume wenye pesa nyingi na yeye hayupo kwenye hao watu kwaiyo sikuwa naye Kwajili ya pesa na umaarufu. Wanaume zangu wote niliowahi kutembea nao ni matajiri lakini bado sijapata ambaye hatakuwa anabadilisha wanawake”.

 

Shilole Amtema Zari na Kumkubali Tanasha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amedaiwa kumsaliti na kumwaga Zari na kumkubali zaidi Mpenzi Mpya wa Diamond Tanasha.

Kama utakumbuka siku mbili zilizopita Shilole alisimama mbele ya waandishi wa habari na kumuomba Diamond aachane na Tanasha na kumuoa mama Watoto Wake Zari.

Lakini sasa Shilole ameonekana kukubaliana na hali halisi na kumkubali Tanasha kama wifi yake mpya na kusema wazi kuwa anapopenda Diamond basi na yeye hana budi kufuata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole ameandika maneno haya:

ANAPOPENDA KAKA YANGU SINA JINSI! HI TANASHA, DIAMOND PLATNUMZ WIFI YETU KARIBU DADA HII NDO TANZANIA NITAFANYAJE SASA JAMANI”.

Ni takribani mwaka mmoja tangu Diamond kuachana na Zari na kuanzisha mahusiano mapya na mrembo Natasha kutoka nchini Kenya. Hivi karibuni Diamond Platnumz alikaririwa na kituo hicho cha runinga akieleza kuwa ndoa yake aliyopanga kuifunga mwezi wa pili mwaka huu ameisogeza mbele.

Zari Ampiga Kufuli Diamond na Familia Yake

Mfanyabiashara maarufuu na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’  amedaiwa kuingia kufuli familia nzima ya Diamond.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa, Zari alianza kukata mawasiliano na Diamond, lakini alikuwa akiendelea kuwasiliana na ‘mkwewe’, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na wifi yake, Esma Khan kabla ya kuwa-block wote.

Unajua Zari ni mtu mwenye misimamo sana. Baada tu ya kutangaza kummwaga Mondi Februari 14, mwaka jana, alisema penzi lake na Mondi limekufa, lakini hawezi kukata mawasiliano na familia yake maana wao hawana makosa yoyote.

Ndiyo maana ulikuwa unaona akaunti ya mama Diamond anayotumia jina la mama Dangote kwenye Insta ilikuwa inaendelea kupendeza na picha za wajukuu zake, Tiffah na Nillan kwa sababu Zari alikuwa vizuri na mama Dangote (mama Diamond), lakini baadaye walivyoanza kumletea mapichapicha ya wanawake wengine, Zari akaona isiwe shida, acha awafyekelee mbali”.

Baada ya tetesi hizo kusambaa Gazeti lilimsaka Esma Platnumz  ambaye alikiri kupigwa block muda mrefu, lakini akasema haoni tatizo kwani hayo ni mambo yao binafsi, lakini zaidi ni kwamba wao wanamuunga mkono ndugu yao pale anapokuwa kwenye uhusiano wake.

Sisi hatuwezi kuingia sana kwenye uhusiano wa Nasibu (Mondi), lakini huwa tunamsapoti pale anapokuwa. Kwa sasa yupo na Tanasha, basi tunamuunga mkono“.

Siku za Hivi karibuni Zari ameonekana kuwa mbali na Familia ya Diamond na kuonekana akiwa bize na maisha yake na Watoto Wake nchini Afrika ya Kusini.

 

Zari Amwaga Povu Zito Baada Ya Kukosolewa Kwa Vazi Lake

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka na kuwamwagia Povu zito watu waliomponda Baada ya kuposti picha ya utata.

Siku chache zilizopita Zari aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram zilizomuonyesha akiwa amevaa mavazi ya ndani ‘Swimming costume’ na kupelekea watu kumrushia maneno.

Mashabiki walimjia juu Zari na kumtuhumu kwa Kiba nusu uchi na kuanika kwenye mitandao ya kijamii ilhali akiwa ni mama  wa watoto watano na huku watoto wengine wakiwa wakubwa kabisa.

Baada yapovu hilo la mashabiki Zari aliibuka na kuposti kipande cha video kujibu mashambulizi na kwa sababu asilimia kubwa waliokuwa wakimchamba ni Wabongo, akaona naye bora awachambe kwa Lugha ya Kishwahili.

Jamani nikitaka kuvaa swimming cost kwa swim­ming pool hiyo ni maisha yangu, ukitaka kuvaa dera hiyo ni maisha yako usini­pangie maisha vile mimi sikupangii maisha naomba tuheshimiane, samahani”.

Zari alivaa mavazi hayo pembezoni mwa bwawa la kuogelea ambapo Hivi sasa yupo nchini Uganda na familia yake.

Zari Afungukia Magumu Aliopitia 2018 na Kuupokea 2019

Mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amefunguka mwaka 2018 na kuupokea 2019.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari alisema kuwa mwaka 2017 alipitia katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mama yake mzazi pamoja na aliyekuwa mume wake, Ivan.

Lakini Pia Zari alieleza namna alivyoutumia mwaka 2018 katika kujenga na kuyarekebisha baadhi ya makosa yake na matatizo aliyopitia.  Anasema alijijenga zaidi baada ya kuondokewa na wapendwa wake hao wawili na kuahidi kuwa yuko tayari kwa mwaka 2019.

Mwaka 2019, niko tayari kwa mwanzo mpya… Katika maisha, sisi huumiza, tunafanya makosa, tunasamehe, tunaendelea. Lakini, zaidi ya yote tunajifunza. Asante 2018, bado nina pumua.   Asante, nishirikishe hadithi yako ya maisha kwa mwaka 2018“.

https://www.instagram.com/p/Br2SY6ln7KC/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=sy9rx7neaahn

Tanasha Avunja Ukimya Kuhusu Kupambanishwa na Zari

Mpenzi mpya wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh mrembo kutoka Kenya amefunguka kuhusu kupambanishwa na Baby mama wa Mpenzi Wake Zari The Bosslady.

Tangu Diamond aweke hadharani kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Tanasha Baada ya kuachana na Zari kumekuwa na mgongano katika ya timu hizo mbili za ushabiki wa Zari na Tanasha.

Lakini Tanasha ameibuka na kuzima tetesi zote za kuwepo na Bifu kati yake na Zari na kuweka wazi kuwa yeye una tatizo binafsi na mwanamama huyo na kuwataka watu wasiwachokonoe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shabiki mmoja alimuuliza Tanasha kama anamfahamu Zari na yeye moja kwa moja alijibu:

Hapana simfahamu Zari lakini naamini ni mama wa Watoto wawili ambaye ni mchapakazi na watu tafadhali was he kutupambanisha na kuanza kututengenezea maugomvi yasiyokuwa na maana badala yake watuinue wote kwa pamoja”.

 

Zari Amkumbuka Ivan Katika Siku Yake Ya Kuzaliwa

Mwanamama mjasiriamali na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amkumbuka Marehemu Ivan katika siku yake ya kuzaliwa.

Zari amemuandikia ujumbe mzito aliyekuwa mume Wake Ivan Semwanga ambaye alikufa mwaka jana kutokana na maradhi ya moyo.

Mbali tu ya kuwa alikuwa mumewe kwa miaka mingi Lakini pia ni baba wa watoto watatu wa kiume.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika maneno haya kama ishara ya kumkumbuka:

Leo ungetmiza umri wa miaka 41 kama ungekuwepo hai, lakini Mungu alikuwa na mipango yake mingine, ndio ingawa tunakukosa wewe kuwa hapa kimwili lakini nahisi kama hujaondoka upo na sisi. Ninakuona kupitia watoto wako, ninahisi uwepo wako kila mahali mimi nilipo, Urithi wako unaendelea kuishi, Endelea kulala kwa amani mpaka tutakapokutana tena.”

Natafuta Mwanaume Ambaye Atakuwa Baba Kwa Watoto Wangu-Zari

Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kuweka wazi tangu ameachana na Diamond amekuwa akitafuta mwanaume ambaye atakuwa kama baba kwa Watoto Wake.

Baada ya mahusiano ya takribani miaka minne Zari alimtosa Baba Watoto Wake Diamond mapema mwaka huu katika siku ya wapendanao tena kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Sasa Zari ameweka wazi kuwa tangu aachane na Diamond  ameshakuwa na mahusiano na wanaume kadhaa lakini hivi sasa anataka mwanaume ambaye atakuwa mfano bora wa baba kwa  watoto wake wa kiume na mwanaume ambaye binti yake wa kipekee atatamani kuwa mfano wa mwanaume wa kuolewa naye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari ameandika maneno haya:

Zari Awajibu Wanaomtaka Ahame Kwenye Nyumba Ya Diamond

Mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda Zari The Bosslady ambaye pia ni mzazi mwenzake na staa was Bongo fleva Diamond Platnumz, ameibuka na kuwajibu mashabiki ambao wamekuwa wakimtaka ahame Kwenye Nyumba ya Diamond.

Miaka michache iliyopita wakati Diamond na Zari wapo kwenye mahusiano Diamond alinunua Nyumba ya thamani nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya Zari na Watoto Wake lakini Baada ya kuachana Zari bado anaishi kwenye nyumba ile.

Mashabiki mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wamtaka Zari ahame Kwenye Nyumba ya Diamond kwa sababu wamekwisha achana na yeye anajitamba kuwa ni tajiri.

Baada ya kuchoshwa na maneno hayo Zari amewajia juu amshabiki hao kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuwa hawezi kutoka Kwenye Nyumba hiyo kwani yeye na watoto wake walinunuliwa ili waishi.

Zari amewatolea watu wajue kuwa yeye kuishi pale sio kwamba hana Nyumba Bali ana Nyumba nne South Afrika lakini anaishi pale kwa sababu ni Nyumba yake aliyonunuliwa na baba wa Watoto wake.

 

Mama Diamond Afungukia Uhusiano Wa Ommy Dimpoz na Zari

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra Kassim maarufu kama Mama Diamond amefunguka na kuongelea uhusiano na kinachoendelea kati ya Zari na Ommy Dimpoz.

Siku chache zilizopita msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mzazi mwenzake na Diamond Zari the Bosslady walitengeneza headlines baada ya picha zao wakiwa pamoja nchini South Africa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi, Mama Diamond amesema kuwa ukaribu wa Zari na Dimpoz ni wa kawaida kama watu wengine na kuwataka watu waache maneno maneno yasiyo na msingi.

Kwani kuna ubaya gani? Hivyo ni vitu vya kawaida kwa mtu kukumbatiana na mtu aliyekutana naye Mimi sijaona hiyo picha ambayo kamshika pajani lakini bado nasema hayo ni mambo ya kawaida tu. Ina maana Zari asiongee na watu? Watu wanasema Nasibu na Ommy wana ugomvi, mimi sijaona wakipigana, najua wanaongea na wala mimi sina ugomvi na mtu”.

Siku za nyuma Diamond aliwahi kuingia kwenye ugomvi mzito na Ommy Dimpoz uliopelekea kutukanana matusi ya nguoni hadi Ommy kumkashifu Mama Dimoand lakini tangu alipougua kuna tetesi kuwa bifu hilo limeisha na wasanii hao wamesahameana.

 

Mama Diamond na Zari Wadaiwa Kuwa Ndani Ya Bifu Zito

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah au maarufu kama Mama Diamond amedaiwa kuwa kwenye bifu zito na mazi mwenzake na mwanaye mwanamama Zari The Bosslady.

Global Publishers wanaripoti kuwa kuna bifu zito linaendelea kati ya Zari na Mama Diamond huku mtu wa karibu na familia hiyo kuanika kuwa wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya mama Mondi kubeba ujauzito.

Inaripotiwa kuwa Mama Mondi alipata ujauzito na kumueleza mkwewe huyo kuwa anahitaji daktari mzuri kutoka Afrika Kusini ili ahakikishe kuwa ujauzito huo hautoki kwani anahitaji kupata mtoto na mumewe Maisala Shante ‘Anko’ ili aifurahie ndoa yake.

Unajua kwa nini mama Mondi na Zari waliingia kwenye bifu akamchukia? Ni kwa sababu alimpa siri ambayo alikuwa hajamwambia mtu yeyote ya ujauzito wake yeye akamwambia meneja mmoja wa Diamond ambaye naye alimtania mama bila kujua kuwa ilikuwa ni siri”.

Aidha, mtoa habari huyo alisema kuwa baada ya Zari kumueleza meneja huyo bila kujua kuwa hakutaka mtu ajue na meneja huyo akamtania mama Mondi kuwa ni mama kijacho kitendo ambacho kilimkera ndipo bi’mkubwa huyo alipomchamba Zari.

Unaambiwa mama Mondi alimchamba Zari vibaya na bahati mbaya ujauzito wenyewe ukatoka kwani ulitoka hata kabla hajapata msaada aliokuwa anautaka”.

Baada ya tetesi hioz za bifu na Zari gazeti la Amani lilimsaka Mama Diamond ambaye alikana kabisa bifu hilo na mkwe wake na kufunguka;

Sina bifu na Zari mbona huwa nawasiliana naye kwa njia ya WhatsApp na mara ya mwisho amenitumia picha za watoto na kuhusu kumposti kwenye Instagram mbona tulishaacha kupostiana siku nyingi ndio maana sijamposti lakini hatuna bifu lolote“.

Mama Diamond alipoulizwa kuhusu taarifa za ujauzito alidai kwamba ameshezaa tayari na kwa sasa mtoto wake ameshakuwa mkubwa tuu.

 

Mobetto Apata VISA Ya Marekani Baada Ya Zari na Wema Kupigwa Chini

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva  Hamisa Mobetto amewabwaga mahasimu wake wakubwa Zari The Bosslady na Wema Sepetu na Kufanikiwa kupata visa ya kwenda Marekani.

Hamisa amewaacha mbali Zari na Wema baada ya kujipatia VISA yake ya kuingia nchini Marekani kwa ajili ya kupiga kazi.

Miezi michache iliyopita Wema Sepetu alitangaza kuwa atakuwa nchini Marekani kwa ajili ya kufanya appearance Kwenye Tanzania day lakini hilo halikufanikiwa baada ya kunyimwa VISA ya kwenda nchini humo.

Lakini vivyo hivyo ilikuwa kwa Zari ambaye Miezi michache nyuma alitangaza kuwapeleka Tiffah na Nillan kwa Diamond aliyekuwa nchini Marekani Kwenye ‘A Boy from Tandale Tour’ lakini baadae ilishindikana baada ya Zari kunyimwa VISA ya kuingia nchini Marekani.

Hamisa ameonekana kuwashinda mahasimu wake hao kwani hivi sasa yupo njiani kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya appearance katika miji mbali mbali.

 

 

 

Rommy Jones Adai Mwanamke Pekee Anayemfaa Diamond ni Zari

Kaka wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Rommy Jones ameibuka na kudai mwanamke pekee  anayemfaa mdogo wake ni Mpenzi wake wa zamani na mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari’.

Mahusiano ya Diamond yameendelea kutengeneza headlines Kwenye mitandao ya kijamii hasa sasa kutokana na warembo wawili ambao ni Kim Nana na Lynn kuonekana kugombani Penzi la staa huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Rommy Jones, amefunguka kuwa mke pekee ambaye anamfaa mdogo wake huyo ni mzazi mwenziye Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’.

Nasema ukweli ndani ya moyo wangu, Zari ni mwanamke ambaye anafaa kuwa mke na kuwekwa ndani kwa sababu anajielewa na anasimama kama mama kuanzia kwenye ulezi wa watoto wake na kila kitu ndani ya nyumba”.

Rommy amesema anatamani Zari awe shemeji yake wa maisha na ikiwezekana wafunge ndoa kwani ana kila sifa ya kuwa mke na ndiye mwanamke pekee anayeweza kumuweka sawa mdogo wake na akaenda kwenye njia sahihi.

Unajua kila familia ingependa sana kuona mtoto wao anapata kitu kilicho bora, yaani mke ambaye anaweza kusimama vyema kama mama hivyo mimi leo nikiamka Diamond aniambie anamuoa Zari, nitafurahi sana kwa sababu najua atakuwa amepata kilicho bora kabisa”.

Lakini pia Rommy hakusita kuwaongelea Lynn na Kimnana ambapo amesema;

Unajua Diamond kwa hao (Lynn na Kim Nana) ni kama tu zile za mwanaume kutenda kosa na kuchepuka nje, lakini akawa na msimamo na mwanamke wake, kwa hiyo kwa hao siwezi kumuongelea sana kwa sababu pia sisi hata siku moja hatukai na kujadiliana naye mambo yake ya kimapenzi, ila ukizungumzia mke, basi nitakuambia ni Zari tu”.

Zari Kula Sahani Moja na Baba Yake na Beyoncé

Mfanyabiashara maarufu Afrika mashariki ambaye pia ni mzazi mwenzake na Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady anatarajiwa Kula sahani moja na Baba yake na staa wa Muziki Beyoncé.

Zari anatarajiwa kuwa Mshehereshaji (Host) katika hafla hiyo lakini sambamba naye atakuwa Mathew Knowles ambaye ni Baba mzazi wa Msanii Beyonce Knowles.

Tuzo hizo maarufu zaidi barani Afrika zenye lengo la kutambua mchango wa viongozi na wafanyabiashara walioleta mabadiliko kwenye jamii zao, zitatolewa siku ya Jumatano Oktoba 17, 2018 katika ukumbi wa The Sun Time Square Arena mjini Pretoria, Afrika Kusini.

Viongozi wakubwa wa kisiasa na watu maarufu duniani watakuwepo k mwa ajili ya Kupewa tuzo mbali mbali lakini pia wasanii maarufu kama rapper  Ice Prince na  Omotola Jalade Ekeindþe wote kutoka Nigeria, Jah Prayzah kutoka Zimbabwe.

 

Zari Adaiwa Kutafuta Mwanasheria Wa Kumshughulikia Diamond

Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amedaiwa kutafuta mwanasheria kwa ajili ya kumsimamia mzazi mwenzake.

Tangu Diamond na Zari walipoachana mapema mwaka huu wamekuwa wakijaribu kutafuta njia bora ya kulea watoto wao wawili wadogo na mara kwa mara Zari amemtuhumu kwa kushindwa kutimiza majukumu yake kama Baba.

Global Publishers wanaripoti kuwa Zari mwanasheria kwa ajili ya kumsimamia Diamond ili awalee watoto wake katika misingi bora licha ya kuwa wameshatengana.

Chanzo cha karibu cha Familia hiyo kimeiambia gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa Zari ni mwanamke ambaye yuko ‘siriaz’ na malezi ya watoto hivyo ameamua kumwekea mzazi mwenzake huyo mwanasheria ili aweze kuwajibika kwa asilimia mia moja bila kukosa hata jambo moja la msingi.

Unaambia siri ya Diamond kwenda Sauz (Afrika Kusini) kila mwezi ni baada ya kuwekewa mwanasheria huyo ambaye anamfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha haendi kinyume na matakwa ya sheria.

Unajua hata akiwa na shoo vipi ameambiwa ajipange ili kutofautiana na ratiba za watoto na akifika nyumbani pale kwa Zari wanalala chumba tofauti ingawa siku nyingine anakwenda kulala hotelini”.

Baada ya taarifa hizo GPL lilimsaka Diamond ambaye alifungukia tuhuma hizo na kusema:

Waswahili nimewazoea sana tu, wasiponiongelea na Zari hawaoni sawa, mimi huwa nakuja huku kwa ajili ya kuwaona watoto wangu, natimiza majukumu kama baba, hayo mengine nawaachia wao”.