Loading...

Tahiya Aachia Ngazi Kwa Mwanaume wa Hamisa Mobetto

March 04, 2019 at 10:47
Tahiya Aachia Ngazi Kwa Mwanaume wa Hamisa Mobetto

Video vixen maarufu kama Tahiya John ambaye Hivi karibuni aliingia kwenye headlines Baada ya kuchukuliana mwanaume na Msanii Hamisa Mobetto.

Tahiya na Hamisa waliingia katika mgogoro kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya Hamisa kumnyakua Mpenzi wa Tahiya anayejulikana Kama Alex hadi kupelekea kuwafumania wawili hao Zanzibar.

download latest music    

Lakini Hivi karibuni Hamisa na Alex walionekana wakiwa katika Penzi zito Baada ya kuongozana pamoja katika tuzo za SZIFF zilizofanyika Wiki iliyopita.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Tahiya aliulizwa kama ameachana na mwanaume huyo ndipo alipoweka wazi kuwa amemsusia mwanaume huyo kwa Hamisa:

Siwezi kusema nimeachana Alex  au sijaachana naye. Bwana ee kama wameongozana watajijua wenyewe mimi sitaki kuwazu-ngumzia kabisa”.

Juzikati bwana huyo alionekana akiwa ameongozana na Hamisa kwenye Tuzo ndipo watu mitandaoni wakaibuka tena na kuanika kuwa wapenzi hao hawakuachana baada ya kufumaniwa na sasa mambo yapo hadharani. Hamisa aliposakwa kumzungumzia mpenzi wake huyo mpya alipokea simu na baada ya kuelezwa madai hayo alikata bila kusema chochote.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…