Loading...

Tamasha la Jide Kuwashusha Nyumbani Wasanii Wakubwa Afrika.

October 12, 2018 at 14:48
Tamasha la Jide Kuwashusha Nyumbani Wasanii Wakubwa Afrika.

Mwanadada Lady Jay Dee ameamua kukamilisha kile alichokuwa amekihaidi kwa muda mrefu baada ya mashabiki wake kusubiri kwa muda mrefu sana tamasha hilo lililoanza kutangazwa muda mrefu nyuma.

Lady Jay Dee ambae aliwahi kusema kuwa kuna kitu kinakuja kati yake na Juliana kanyomozi kutoka Uganda, basi kitu icho kinaenda kukamilika kutokana na tamasha la Vocal nights kufanyika October 26 mwaka huu na kuleta wasanii wengi.

Loading...

Akizungumza na Show biz , Lady Jay Dee anasema kuwa tamsha hilo litawaleta wasanii wengi akiwemo Zahara kutoka Afrika ya kusini na pia Juliana kanyomozi kutoka uganda.

Jay De anasema”nina lengo la kulifanya onyesho hilo kuwa kubwa na la kila mwaka, na lengo kubwa ni kuwakomboa wale wanawake ambao wamekuwa wakilazimishwa kuuza utu wao ili kufanikiwa katika kazi zao.kama unavyojua kuwa wanaume wameshika karibia kila sehemu ya hii sanaa. “

Jay dee anasema kuwa wasanii wengi wa kike wana vipaji lakini hawasikiki kwa sababu hiyo anasema kuwa tamasha hil litakuwa kama daraja kwa baadhi yao huku akimtolea mfano Grace Matata.

Kama mtu anakuwa hayuko tayari kutoa rushwa ya ngono basi hawezi kufanikiwa kwaio mimi nataka kuwa darala kwao, ndo maana nimeamua kumchukua Grace matata maana anafanya kazi nzuri lakini hasikiki.

Mbali na wasanii hao pia atakuwa aliyewahi kuwa mshiriki wa big brother miaka iliyopia UTI NWACHUKU ambae atakuja kwa ajili ya kunogesha tamasha hilo.

Uti pia ni msanii kule kwao kwaio nimemleta pia ili kuchanganya radha ya tamasha,ninategemea kupata sapoti kubwa kutoa kwa mashabiki ambao kila mara wamekuwa na mimi kwa kila jambo.

 

Share

Comments

  1. Nice

  2. Awesome

  3. 👏👏👏

  4. vyema zaidi

  5. Can’t wait

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…