Thea na Mike Sangu Bado Mahabani Hata Baada Ya Ndoa Kuvunjika

Msanii mkongwe wa Bongo movie Salome Urassa maarufu kama Thea na aliyekuwa mume wake ambaye pia ni Msanii Mike Sangu wamedaiwa kuwa bado wanapendana licha ya ndoa ya kuvunjika.

Thea na Mike Sangu walikuwa kwenye ndoa Lakini waliishia kutengana kwa muda mrefu, juzikati walionesha kuwa bado wanapendana kwa kui­tana majina matamu, kitu ambacho kiliwaacha wengi mido­mo wazi.

download latest music    

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa tukio hilo lilichukua nafasi maeneo ya Yombo Dovya jijini Dar ambapo wasanii hao walikwenda kutoa msaada kwa Hamisi, mtoto anayesumbuliwa na uvimbe.

Ilikuwa hivi; wakiwa eneo hilo mmoja wa wasanii alimtania Thea na kumwambia kuwa, Mike anamuita. Bila ku­tarajia Thea alimsogelea Mike na kumuuliza kwa sauti iliyotokea puani; ‘Eti kweli unaniita mume wangu?’

Maneno hayo yaliyotoka kwa sauti ya kimahaba yaliwafanya wasa­nii waliokuwa eneo hilo kuamini kuwa bado wawili hao wanapendana na huenda siku moja wakarudiana kwani waswahili wanasema; penzi la kweli halifi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.