Tunda Afungukia Tetesi za ‘Kuliwa’ na Diamond

Socialite maarufu Bongo, Tunda amekana tetesi zilizoenea mjini kuwa anatembea na msanii maarufu wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Habari ya Tunda kutembea na Diamond na kuwa mchepuko wake ndio imekuwa habari ya mjini kwa kipindi cha wiki nzima sasa huku tetesi zikienea kwa kasi ya ajabu kuwa hivi sasa Tunda tayari ana ujauzito wa Diamond

download latest music    

Skendo hii imeendelea kuingilia kati uhusiano wa Diamond na mama watoto wake Zari kwani kupitia page yake ya Instagram amekuwa akimrushia madongo machache baba watoto wake hadi kufikia hatua ya kumu-unfollow kwenye Instagram.

Huku hayo yote yakiwa yanaendelea Tunda amezidi kushikilia msimamo wake na kusisitiza kuwa hana uhusiano wowote na Diamond na anashangazwa na habari hizo kwani anamheshimu sana Diamond.

Tunda alifunguka maneno haya machache alipoulizwa na paparazi kuhusiana na ishu hiyo:

Nimechoka mimi kuongelea hili suala, Mimi na Chibu hatuna uhusiano wowote wa kimapenzi nilishasema yaani hii ni mara ya nne nasema yule ni mtu ambaye namheshimu halafu unajua mimi ni timu WCB, nawapenda WCB wote ndio maana unaona nimekaa upande wa WCB kwaiyo haya mambo ya mimi kutoka na Naseeb siyo kweli, Naseeb ni mtu tu ambaye namheshimu na nampenda, halafu sina mimba kila siku mimba tu aaha nimechoka sina mimba mimi mbona jamani”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.