Tunda Amtupia Dongo Zito Hamisa Baada Ya Kumuona na Diamond

Video vixen maarufu Tunda Sebastian amerudi tena Kwenye headlines baada ya kumtupia Dongo Zito hasimu wake namba moja Hamisa Mobetto baada ya video zake za chumbani na Diamond kuvuja mtandaoni.

Usiku wa jana Diamond na Hamisa walizua gumzo baada ya kuonekana pamoja chumbani wakiwa wanakumbatiana kwenye mahaba mazito jambo lililozua gumzo kuwa wamerudiana.

download latest music    

Lakini muda mfupi baada ya Hamisa kuonekana na Diamond video zilizomuonyesha Diamond na demu wa kizungu wakila Madenda nazo zilivuja mtandaoni jambo lililowachanganya watu wengi kuona Diamond na wanawake wawili tofauti katika usiku mmoja.

Kama utakumbuka Tunda na Hamisa wameshawahi kuwa na bifu siku za nyuma huku ikiaminika kuwa walikuwa wanamgombania Diamond kwani wote wawili wameshahusishwa kuwa na Mahusiano na Diamond.

Tunda ameibuka na kumpa Dongo Zito Hamisa baada ya video zake na Diamond kusambaa mtandaoni ambapo amedai kuwa anamuonea huruma Hamisa maana amedhalilishwa na mwanaume ambaye ni wazi kabisa kuwa hamtaki.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Tunda kaandika maneno haya:

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.