Tunda Awatolea Povu Wanamhoji Kwa Urafiki Wake na Casto Dickson

Video vixen maarufu katika tasnia ya Bongo fleva Anna Kimaro maarufu kama Tunda amefunguka na kuwatolea Povu zito wanaomhoji Baada ya kumposti aliyekuwa Mpenzi Wake Casto Dickson.

Tunda na Casto walikuwa kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa Mpaka pale walipoachana miezi michache nyuma ambapo ilidaiwa kuwa Tunda alimtosa Casto na kumwacha na bonge la tattoo ya jina lake katika mkono wake.

download latest music    

Siku chache zilizopita Tunda alionekana kuwashangaza watu wengi Baada ya kuamua kumposti tena Casto kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika na maneno:

Happy birthday mzee vizuri @ Castodickson ishiiiii”.

Baada ya kuposti hivyo kuna tetesi ziliibuka Kama wamerudiana ndipo Global Publishers walimsaka Tunda na akafunguka haya:

Mnajua nyie mnachekesha sana, sasa kwani kuna tatizo gani mimi kumposti huyo kaka, kwa sababu binafsi sioni kama ni tatizo kwa kuwa kila mtu alishaamua kushika hamsini zake, hakuna mapenzi tena sasa hivi tumebaki washikaji tu naomba mnielewe”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.