Loading...

Tutaendelea Kuzunguka Mikoani Kutoa Shukrani.:-Vikings

March 13, 2018 at 10:30
Tutaendelea Kuzunguka Mikoani Kutoa Shukrani.:-Vikings

Wasanii wakongwe ambao kwa sasa wameanza kurudi tena  kwenye game baba na mwana , wamefunguka na kusema kuwa baada ya kufanya shoo yao kubwa Dar  sasa hivi wanaanza kuweka nguvu yao kubwa kuzunguka mikoani kwa ajili ya kukutana na mashabiki wao wa nje ya dar.

Nguza Viking anasema kuwa sababu kubwa ya kufanya kazi hiyo ya kuandaa show kubwa dar es salaam na nje ya Dar Es Salaam ni kuwashuru watuu wote waliokuwa wakiwaombea kipindi cha shida na wale wanaofurahia uhuru wao.

Loading...

Kikubwa ilikuwa ni kukutana na mashabiki zetu na kutoa shukrani zetu kwao, na kwa sasa tumepanga kuanza tutoa dance mikoani ili kuendelea kuwashuuru watu wanaotusapoti.nawashukuru sana watanzania na nina wapenda sana.

Nae Papii Kocha akimsapoti baba yake anasema kuwa wakazi wa mikoani wakae kuwapkea kwa sababu wameanza kujipanga kwa ajili ya kuzunguka mikoani.Hata hivyo akiongelea kuhusu uongozi wao mpya, papii anasema kuwa kwa  muda ule asingeweza kuongea chochote lakini baada ya wiki mbili mambo yatakuwa wazi.

Papii Kocha  na Nguza waliandaa showyao kubwa ya kwanza tangu walipotoka gerezani mwaka jana walipoachiwa huru baada ya kukitumikia kifungo zaidi ya miaka 14.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.