Loading...

Ujumbe wa Diamond kwa Mzee Yusuph kufuatia kifo cha mkewe na mtoto wake

June 19, 2017 at 15:03
Ujumbe wa Diamond kwa Mzee Yusuph kufuatia kifo cha mkewe na mtoto wake

Mzee Yusuph alimpoteza mke wake mdogo Chiku Khamis Tumbo na mwanawe mchanga ambao waliaga dunia usiku wa Jumamosi katika hospitali la Amani Dar es Salaam Tanzania.

Chiku alifariki akijifungua, mtoto wake wa kike pia aliaga dunia wakati huo. Mwenda zake alikimbizwa hospitalini na Mzee Yusuph usiku huo alipoanza kuskia uchungu wa kujifungua.

Mashabiki wa Mzee Yusuph wamekua wakitoa salamu za rambirambi kwenye mitendao za kijamii kufuatia kifo cha bibi yake.

Chiku Khamis Tumbo

Diamond Platnumz pia amemfariji Mzee Yusuph kwa ujumbe aliyoandika kwa Instagram; alimpa roho kwa kumwambia Mola ndo hupanga kila kitu duniani.

“Stay strong bro, Mwenyez Mungu ndio mpanga wa kila jambo… tumshukuru na kuwaombea waendapo wapumzike kwa Amani…Amin, Inshaallah🙏” Diamond aliandika.

 

Leave a Reply

Be the First to Comment!

Notify of
avatar
wpDiscuz

in Entertainment
Loading...

Ultimate keyboard ninja dedicate to bring you the juiciest stories in blogosphere