Ujumbe wa Wema baada ya Manji kuachiwa huru

Jana Septemba 14, kulizagaa stori mitandaoni na vyombo vya habari vingi kuhusu kuachiwa huru kwa mfanyabiashara maarufu nchi bwana Yusuph Manji,kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam  jana ilifika ukomo baada ya Manji kuwekwa huru, mrembo wa shindano la Miss Tanzania 2006 na msanii  mkubwa na mkongwe wa Bongo Movies  Madam Wema Sepetu alioneshwa kufarahishwa na tukio ilo la kuachiwa kwa mfanyabiashara huyo na kuamua kuposti picha katika ukurasa wake wa instagram na kuand ika machache yanayoonysha shukrani na furaha “Alhamdullilah” aliandika Wema, Wema ameonekana kufurahishwa na jamba ilo kwa sababu kwa muda sasa mfanyabiashara huyo amekuwa hakiangaika na kesi iyo mhakamani.

Manji na wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa nchi kwa zaidi ya miezi sita sasa  ambapo walikutwa na mabunda  35 ya vitambaa vya kutengenezea nguo za jeshi  zenye thamani zaidi ya sh. milion 190 , wameachiwa huru jana baada ya mwendesha mashtaka wa mahakama ya Kisutu jijini Dar Es Salaam  kuamua kufuta  kesi iyo.

download latest music    

Katika kuonyesha hisia zake Madam  Wema  Sepetu amekuwa ni mtu anayepost picha za Manji karibia kila mara huku akiandika maneno ya kusikitisha au kumtia moyo mfanyabiashara huyo kuhusu kesi hiyo kwa muda mrefu sana ,kwa mfano mwezi February mwaka huu,  baada ya Manji kupata dhamana ya kesi  na kuachiwa huru Wema alipost katika ukurasa wake wa instagram na kuonyesha kushukuru na kufurahia jambo hilo.

Katika mahakama hiyohiyo pia Wema bado anakabiliwa na kesi yake ya madawa ya kulevya ambayo mara ya mwisho ilisikilizwa wiki hii na bado itaendelea kusikilizwa mahakamani hapo.msanii huyu wa kike amekuwa akifanya vizuri katika tasnia ya filamu kwa sasa na hivi karibuni ametoa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Heaven Sent’ aliyoshikirikisha wasanii wenzie wengine akiwemo msanii wa kuime anaefanya vizuri kwenye game pia Gabo Zigamba , movie iyo iliyozinduliwa hivi karibuni imepokelewa vizuri na mashabiki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.