Ukweli kuhusu biashara ya Wema kupigwa stop

 

Msanii Wema Isaack alikuja na biashara mpya ambayo wakidada wengi waliipenda kwa sababu ya uzuri wa bidhaa za mrembo huyo, Wema ambae aliaanza kwa kuzitambulisha lipstick zake zilizojulikana kama Kiss by Wema Sepetu zilipoingia kwa mara ya kwanza Tanzania wakidada walizigombania kama njugu sokoni hivyo bidhaa hiyo kuisha, shida imekuja katika kuendeleza bidhaa hizo kwa kuagiza mzigo mara ya pili ambapo kumekuwa na tetesi mbaya kuhusu bidhaa hizo.

download latest music    

Kumekuwa na tetesi kuwa biashara hiyo inaweza kufa kutokana na mzigo mpya ambao umeagiza umepigwa stop kisa tu bidhaaa hizo zinaonekana hazina ubora kama mwanzo.Tetesi hizo zinasema kuwa kutokana na kupendwa kwa lipstick izo sokoni ndio maana mzigo wa pili ulitengenezwa haraka bila kujali ubora wowote,  na ni hatari kwa matumizi ya watu hivyo bidhaa hizo kukatazwa kuingia sokoni.

Lakini pia zipo tetesi kuwa inawezekana kuna watu wanaotaka kuchafua jina la msanii huyo  kwa kusambaza tetesi hioz au kuingia mzigo fake kwa kutumia jina la Madame ili tu  kumuharibia msanii jina.

Hata hivyo alipokuwa akitoa maelezo ya uwepo wa tetesi hizo katika kituo cha EATV , meneja mpya wa Madame Wema Sepetu aliejulikana kwa jina la  Happy  Shame  amesema mzigo huo haupo sokoni kwa sasa kwasababu  msimu wa kuangiza mzigo mpya bado  na sio kweli kwamba mzigo umezuia kwa sababu hauna ubora .

“Hicho kitu sijakisikia na wala sijatumia katika email yangu  kwamba lipstick zimezuiwa . Hivi vitu vinaenda na msimu , muda wake ukifika tutaziachia  kwaiyo hakuna ukweli  isipokuwa kuna baadhi ya vitu  tunavikamilisha baadae mzigo utatoka” anasema Happy Shame.

Hivyo basi uwepo wa tetesi za kusimamishwa kwa bidhaa za lipstick za Wema Sepetu zinaweza kuwa  si za kweli ilhali meneja wa msanii huyo amethibitisha kuja kwa bidhaa hizo endapo taratibu za uingizaji wa bidhaa hizo nchi utakamilika, hivyo kwa wateja waliokuwa wanasubiri bidhaa hizo wanaweza kutokwa na wasiwasi kwa kusikiliza pia maneno ya meneja.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.