Utovu Wa Nidhamu Wamponza Calisah.

Mbunifu wa mitindo mkongwe na aliyefanikiwa sana kimataifa Mustafa Hasanali amefunguka na kuongelea maendeleo ya tasnia ya mitindo nchini na vile inavyoendelea kukua siku hadi siku, hata hivyo mwanamitindo huyo amesema kuwa katika wanamitindo wanaofanya vizuri Tanzania hawezi kumuweka Calisah kwa sababu hana sifa za kuwa mwanamitindo bora na ndio maana mwanamitindo huyo wala haiendelei kimataifa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo Hassanali amesema kuwa wakianza kuangalia sifa za wanamitindo bora Callisah hawezi kuwekwa kokote kutokana na utovu wa nidhamu na kutokuipenda kazi hiyo na kuipa heshima kama wengine wanavyoipa heshima.Anaongezea kwa kusema kuwa kama angekuwa na heshima basi mwanamitindo huyo angekuwa anafanya vizuri Tanzania na hatimaye angeenda kimataifa zaidi lakini kutokana na tabia zake ataishia kukaa hapa hapa bongo.

download latest music    

Mustafa anaendelea kusema kuwa tasnia ya mitindo inahitaji nidhamu kubwa sana , na kutolea mfano wa mwanadada Herieth Paul ambae aliweza kushiriki hadi fashion ya Victoria Secret , hiyo yote ni kutokana na heshima aliyojiwekea kwake na kazi yake.

Calissah sio model , acha ugomvi uanze tu,unajua London Fashion Week Herieth Paul alifanya hadi Victoria  Secret ambayo ilifanyika Shanghai, kama anaweza kujiita Super model mbona hata Swahili Fashion hayupo?,kila mtu ana staili yake ya maisha na vile anataka kuishi , asiyefundishwa na mamaye hufundishwa na nani?kama mtu hawezi kurespect na kuthamini  biashara ya ubunifu hawezi kuendelea hata kidogo. Alisema Mustafa Hassanali

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wabunifu na wanamitindo wakubwa na wakimataifa kumzungumzia Callisah kuwa hamna sifa za kuwa mwanamitindo , Daxx Cruz mwanamitindo wa kitanzania anaefanya kazi zake Afrika ya Kusini pia alishawahi kusema kuwa Calissah hana sifa za kuwa mwanamitindo na ataishia kufanya hiyo kazi hapa bongo lakini hawezi kutoka kimataifa..

Hii yote inatokana na picha na maneno ya kejeli anayokuwa anayatamka mwanamitindo huyo katika mitandao pale watu wanapokuwa wanam-judge au kumkosoa kuhusu kazi yake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.