Uvaaji wa Viatu kwa Wanaume

wanaume wengi wamekuwa wakionekana hawatilii maanani sana swala la uvaaji wa viatu kama vile wanavyofanya katika kuvaa na kununua nguo, wengi wanaweza kuvaa kitu chochote tu ilimraf amevaa nguo na kiatu bila kujali rangi ya kiatu na nguo aliyovaa.

swala la uvaaji wa viatu au kuwa na viatu vngi mara nyingi wanaona ni swala linalohusu sana wanawake.wanaweza kukumbuka kuhusu nywele, kunyoa ndevu lakini sio kukumbuka  ana pea ngapi za viatu na ipi labda imeharibika inaiaji kuwa -replaced.

download latest music    

kwa mfano unaweza kukuta mwanaume ni askari au mwalimu, lakini kiatu anachotumia kwenda nacho kazini hivho hivho atakwenda nacho kanisani, kwenye sherehe na hata anapopata mtoko tu wa famila au marafiki, kwao ni kitu cha kawaida kabisa.

Wataalamu wa mitindo wanashauri kuwa mwanaume anatakiwa kuwa na viatu zaidi ua jozi nne , ili kuwa anabadilisha badilisha .Hii itamfanya  mwanaume kuonekana ana kwenda na fasheni na anajua mitindo, lakini azingatia mahala husika panapotakiwa kuvaliwa viatu hivyo.

Ni vizuri pia kujua kuwa mara nyingi nguoa kama jeans au kaptula inapendeza kama mwanaume atavaa na raba kuzingatia na rangi  pia.

Ni vizuri kuwa mjuzi wa kuchagua nguo kulingana na kiatu husika, lakini pia  rangi ya kiatu na rangi  ya nguo, zingatia pia sehemu unayokwenda na wau unaoenda kukutana nao pia.Kumbuka unaweza kuwa na kasafari kadogo tu hivyo ni lazima kuvaa kiatu kitakacho kusumbua kama uko na safari ndefu , hii namaanisha kuwa waweza kuvaa viau vya wazi lakini pia kwa kuzingatia nguo yako ya juu.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.