Uwoya Abainisha Sifa za Mwanaume Anayemtaka

Muigizaji wa Bongo movies maarufu na mrembo Irene Uwoya ambaye pia amewahi kuolewa na mcheza mpira maarufu kutoka Rwanda, amesema anataka mwanaume atakaye kuwa naye awe na ngeu nyingi mwilini za kuchanwa na visu!

Irene amesema watu kama hao ndo anawataka yeye kwani inaonyesha kuwa ni uanaume halisi, na sio mwanaume anakuwa laini kama mtoto wa kike.

download latest music    

Irene alinukuliwa akisema:

“Sijasema napenda mwanaume mwenye sura mbaya nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume,  mwanaume uwe na ngeu, mimi bwana wangu ana ngeu, kachanwa visu yaani”.

Irene kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake mapya tangu kuwe na tetesi za kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Msami Baby na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi wazi kwa watu.

Ingawa kumekuwa na tetesi mitandaoni kuwa Uwoya anatoka kimapenzi na mwanamuziki kijana mdogo Dogo Janja ingawa Uwoya ameshakataa kwamba hakuna chochote kinachoendelea baina yao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.