Wolper Akumbwa na Fedheha Ya Aina Yake Mwanza

Muigizaji wa Bongo movie na Mbunifu wa mavazi Jacqueline Wolper amejikuta akipata fedheha ya aina yake Baada ya kula mweleka wa nguvu mbele za watu.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa mbwembwe zilizmponza Wolper kwenye ukumbi uliopo katika Ufukwe wa Jembe ni Jembe jijini Mwanza ambapo Lebo ya WCB  chini ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platinum’ au ‘Mondi’ ilikuwa ikifanya pati ya awali (pre-party) ya onesho lao la Wasafi Festival lililofanyika katika Uwanja wa CCM-Kirumba, juzi.

download latest music    

Katika tukio hilo, wakati watu wakipata kilaji, mastaa ambao walitarajiwa kufanya makamuzi kesho yake kwenye Wasafi Festival walikuwa wakitambulishwa. Ulipofika wakati wa Wolper, yeye aliamua kupanda juu ya meza kama wafanyavyo wanenguaji wa staili ya kusasambua. Akiwa juu ya meza, DJ aliweka Wimbo wa Kwangwaru ambapo Wolper aliendelea kuonesha umahiri wa kukicheza kwa kukata mauno baab’kubwa. Kwa bahati mbaya, wakati akiendelea kufanya yake, maskini mwanadada huyo mrembo alipiga mwereka matata na kuangukia kisogoni.

Hata hivyo, alisaidiwa kunyanyuka na mabaunsa na mashabiki waliokuwa karibu ambao walimuinua kisha wakamkagua na kubaini hakupata maumivu makali hivyo shoo yake ikaishia hapo. Baada ya kushuhudia tukio hilo, baadhi ya mashabiki walisikika wakisema, eti huenda mambo yaliyompata Mondi kule Sumbawanga yalitaka kujirudia kupitia kwa Wolper.

Source- Ijumaa Wikienda

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.