Vanessa Mdee Azidi Kupata Mafanikio na Albamu Yake Ya ‘Money Mondays’

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amezidi kufanya vizuri na albamu yake ya ‘Money Mondays’ kwani albamu hiyo imetajwa kuwa ndio inaongoza Afrika Mashariki nzima.

Kupitia mtandao wa Boomsplay ambao unahusika na upakuaji wa nyimbo kadhaa umeweka wazi kuwa Albamu hiyo ndio kinara kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo wameandika ujumbe huu:

download latest music    

Hongera nyingi sana kwake @vanessamdee kwa kuwa na albamu namba moja kwa mauzo na kusikilizwa, ukanda wa Afrika Mashariki nzima ! Wewe kama shabiki wake mkubwa uliyewezesha hili, tunakupa pongezi pia na endelea kuipa support “Money Mondays” kila siku!”.

Vanessa Mdee alionyesha kufurahishwa na taarifa hiyo kwani alitumia ukurasa wake wa Instagram kushukuru mashabiki zake kwa kuweza kupakua wimbo mpaka kufanya uwe namba moja:

Thank you Asante Sana for making #MoneyMondaysTheAlbum the NO 1 ALBUM in East Africa @mdeemusicofficialmmetishaaaaaa @boomplaymusic_tz@boomplaymusicke @boomplaymusicngwith over a million plays/streams. #SwimmingInJesusJuice #BestFansInTheWorld.”

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.