Vannesa Aamua Kutoa Fursa kwa Vijana wa Kike.

Mwanadada anaefanya vizuri katika anga za musiki nchini Vannesa Mdee ameamua kutoa fursa kwa wadada wanaojua kucheza kwa kuwapa nafasi ya kufanya nao video mpya inayokaribia kutoka hivi karibuni.

Vannesa ambae ameanzisha zoezi la kutafuta vijana wa kike wanaojua kucheza ili aweze kufanya nao ngoma yake mpya amewataka wadada hao kutoka sehmu mbalimbali tanzania kujirekodi wakiwa wanacheza na kuituma video hiyo kwenye Twitter na kuweka hashtag ya #pickmevannesa ili anaejua kucheza ataweza kuitwa na kufanyiwa usaili kwa ajili ya video hiyo inayokuja.

download latest music    

Wasanii wengi sasa wamegundua kuwa hata mitaani kuna vipaji amabvyo vinahitaji kufunuliwa katika anga za sanaa hivyo wameanza kufanya vitu vitakavyo wasaidia watu waliopo nje yatasnia ambao wanaweza nao pia wafanye kazi.

Wiki iliyopita mwanadada Lady Jay Dee,nae pia alifanya audition kubwa jijini Dar kwa ajili ya kutafuta vijana watakao weza kucgeza vizuri nyimbo za ndani na nje ya nchi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.