Vannesa Ajibu Tetesi Za Kurudiana Na Jux

Kumekuwa na tetesi nyingi mitandaoni kuhusu uhusiano wao wa karibu licha ya kuwa walikuwa wapenzi na wakaachana, wengi walitegemea watu hawa watakuwa maadui, wengine wakisema kuwa uwepo wao wa karibu unamaanisha kuwa wamerudiana kutokana na ahadi alizoweka Jux kuwa atafanya juu chini na watarudiana na Vanesaa Mdee.

Vannesa na Jux walikuwa ni moja ya couple iliyokuwa ukiwavutia watu wengi sana hasa muonekano wao walipokuwa pamoja, ukiachana na mapenzi lakini pia walikuwa wakifanya kazi ya muziki na biashara pamoja hiki ni moja ya vitu vilivykokuwa vikivutia zaidi.

download latest music    

Hata hivyo, baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu kurudiana kwao hasa katika msimu huu wa tamasha la Fiesta ambapo mara nyingi walikuwa wakionekana kuwa pamoja na kuwa wote jukwaani na hata kuonyesha vitendo vya kukwepana kimahaba walipokuwa wakiimba Vannesa Mdee amuamua kufunguka na kujibu tuhuma hizo.

Vannesa alisema kuwa ukiachana na mapenzi lakini pia wao walikuwa wakifanya kazi pamoja na biashara, hivyo hata kama wamegombana katika swala la mapenzi haimaanishi kuwa wamapaswa kuwa maadui na kushindwa kufanya kazi pamoja.Wao watabaki kuwa washikaji tu na kufanya kazi na hakuna mapenzi.

kitu ambacho watu wengi hawajui ni kuwa jux ni mshikaji wangu sana,ni mt ambae tunapatana sana na tunaffanya kazi pamoja,na hata vitu vingi sana nje ya muziki jux amekuwa akinipa sapoti sana,kwaio hatuwezi kukaa tukagombana sasa hivi kwanza tunakuwa tukihatribu biashara. -Alifunguka vannesa

Vanesa ana Jux mara ya mwisho walipoonekana kuwa pamoja katika jukwaa la fiesta Morogoro Jux alikuwa akiimba kwa style ya kuomba msamaha ambapo Vanessa alimjibu atamsamehe akifika katika jukwaa la Mtwara, na walipofika mtwara wawili hao walionekana kuimba pamoja na kuonyesha ishara nzito za mahaba zilizofanya  mashabiki wengi khpji kama wamesharudiana au la.

Endapo wawili hao watarudiana itakuwa ni moja ya mambo yatakayo walidhisha mashabiki kwa sababu kwa muda mrefu mashabiki wamekuwa wakivutiwa kuwaona wawili hao kuwa pamoja na  wakiwaomba kwa muda mrefu wawili hao kutaka kurudiana

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.