Vannesa Mdee Atumia Zaidi Mil.100 kwenye Album Yake.

Msanii wa muziki wa bongo fleva vanesa mdee amefunguka na kusema kuwa ametumia zaidi ya mil10 kwa ajili ya kutengeneza album yake ambayo sasa hivi iko sokoni na amekuwa akiinadi katika vituo mbalimbali na hata kutembea nchi mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza album hiyo.

Vannesa anasema kuwa ametumia fedha nyingi sana katika kutengeneza album yae hiyo lakini haoni shida yoyote kwa kuwa anawapenda na kuwajali mashabiki wake sana.

download latest music    

nimetumia ela nyingi sana katika kutengeneza hii album lakini sijajali sana kwa sababu nilitaka watu wamtambue kuwa Vannesa  katika kukua kimuziki, lakini  fedha hizo nililipa katika idara zote kuanzia wasanii waliopo katika album hiyo , matangazo, video na nk na bado naendelea kutoa kwa sababu kuna matangazo mengi.

Vannesa hajutii kabisa kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutengeneza album hiyo,kikubwa ni kuangalia jinsi gani kazi hiyo  ingeweza kumuongezea heshima  na kuhakikisha kuwa inawafikia watu wote .

Vannesa anaingia katika orodha ya wasanii wachache wa kike wenye album Afrika na wanaofanya vizuru nje na ndani ya tanzania kwa kazi zao nzuri  amekuwa akiifanya.Hivi karibuni Vannesa aliachia album yake ya Money Monday katika viwanja vya mlimani City jijini Dar.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.