Loading...

Vannesa Mdee Awajia Juu Mashabiki Kisa Jux

October 12, 2017 at 09:50
Vannesa Mdee Awajia Juu Mashabiki Kisa Jux

Msanii wa muziki Vannesaa Mdee amejikuta akiingia katika mgogoro na mmoja wa shabiki wake wa kike  pale ambapo aliyekuwa mpenzi wake kuposti baadhi ya picha na videos  za tamasha la Fiesta lililofanyika Iringa walipokuwa waki-perfom wote jukwaaani.Hata hivyo  shabiki huyo alimtolea Jux maneno ya kashfa kuwa kwanini anajikuta kumpost sana  mwanamke ambae ameshaachana nae wakati Vannesa  hana jitihada zozote za kumpost yeye na Vannesa hana kitu chochote cha kumpa kwa sababu mapenzi ya Vannesa kwa Jux yameshakwisha , inakuwa kama Jux anajipendekeza kwa Vannesa pale anapokuwa anapost picha zake.

Hata hivyo Vannesa alishindwa kuvumilia maneno ya shabiki huyo wa kike na kujikuta akimtolea povu na kumjibu kwa hasira kidogo na kusema kuwa yeye sio msemaji wake hata hivyo Vee anasema kuwa amekuwa akiona mwanadada huyo akitukana sana katika page ya Jux mara nyingi kwaiyo inawezekana anamtaka Jux kimapenzi labda anakuwa anashindwa kuongea.

download latest music    

Jux na Vannesa Mdee ni moja ya couple iliyokuwa ime-trend sana katika mitandano kipindi cha uhusiano wao, lakini baadae wawili hao walikuja wakagombana huku hakuna anaetaka kutoa sababu yoyote ya mifarakano yao, hata hivyo kwa muda sasa mashabiki wa Vanesa na Jux wamekuwa wakiwaomba sana katika page zao waweze kurudiana, lakin bado mambo yanaonekana kutokuwa mazuri. Kuachana kwao kimapenzi bado hakujafanya kiharibike kitu kwa sababu wawili hao bado wanaonekana kufanya pamoja katika kazi zao za kimuziki ukizingatia kuna baadhi ya nyimbo waliimba pamoja kipindi walipokuwa na mahusiano yao kwaiyo pale kunapokuwa na uhitaji wa wao kutokea pamoja mbele ya mashabiki wao wamekuwa wakifanya hivyo.

swala la mapenzi ni la watu wawili kwaiyo  mashabiki wanapaswa kusapoti muziki wa msanii wanaempenda bila kusababisha makwazo kwa wasnii wao, ingawa kwa Tanzania imekuwa ni swala la kawaida kwa baadhi ya mashabiki kuingilia sana mahusiano ya wasanii na kusababishwa makwazo kwa watu hao wanaowasapoti.Hivyo kama mashabiki wanawapenda wasanii wao basi wajikitye san akutoa ushauri kuhusu kazi za muziki na si vinginevyo.

 

Share

Comments

  1. Ni ukweli waachane kama sio kiki wanatafuta

  2. Kama mmeachana mnafata nini tena

  3. Waacheni wanajaribu kutumia mahusiano kujinufaisha kimziki

  4. Yakimwagika hayazoleki Mdee

  5. Kuvimbia mashabiki hakuweza saidia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…