Vannesa na Jux Wazidi Kupagawisha Mashabiki Fiesta

Baadhi ya watu wanapokuwa katika mahusiano na ikatokea wao kugombana au kuachana kabisa basi watu hao wanakuwa maadui maisha yao yote, lakini hii imekuwa tofauti kwa Vannesa Mdee na Jux ambao walikuwa katika mahaba mazito lakini baadae walikuja kuachana na habari  zilisambaa kila kona nje na ndani ya T5anzania.

Hali ni tofauti kwao kwa sabbau sasa hivi wawili hao wanaonekana kufanya vizuri na wapo karibu katika kufanya kazi zao  tena hasa wanapo kuwa jukwaani huwezi kujua tofauti zao zozote, hii imetokea wikiendi o iliypita walipokuwa waki-perfom katika jukwaa la Fiesta Iringa ambapo  wawili hao walitakiwa kupanda jukwaani ili kuimba wimbo wa juu ambao waliimba wote kipindi wapo katika mahusiano yao,katika show iyo, jux alifikia hatua ya kuimba mpaka kumpigia magoti Vannesa Mdee.

download latest music    

Hii imetokea tena katika tamasha la Fiesta Mbeya lilikuwa likijulikana kama  Tigo Fiesta Classic Mbeya, ambapo wawili hao walianza kuimba wimbo wa nimezama wa kidumu ,kisha kuimba tena wimbo wa juu bila kuonyesha tofuati zao. Hata hivyo wawili hao wanapokuwa wanaimba huwa  nyuso za furaha na kuonyesha mahaba kiasi kwamba ni vigumu kujua kuwa wapo katika mgogoro.

Vannesa na jux walikuwa ni moja ya couple iliyo-trend na kupendwa sana na mashabiki, na imefika hatua kwamba mashabiki kila kukicha wamekuwa wakiwaomba wawili hao waweze kurudisha penzi lao lakini inaonekana  kushindikana bado.Wawili hao wamekuwa wakiteteana hata katika mitandao pale inapotokea shabiki anapomshambulia mtu mmoja kati yao.

Hii inadhiirisha nini, inawezekana wawili hao wameona ni muda muafaka wa kuacha ugomvi na kufanya kazi hata kama huko nyuma kulikuwa na historia ya mapenzi kati yao.Au wameamua kusikiliza maombi ya mashabiki wao na wameanza kurudisha mapenzi yao taratibu ,kwa sababu  Jux  alishawahi kusema mahusinao yao bado wapo katika mazungumzo.Hata hivyo kwa kipindi chote cha kuachana kwao hakuna aliwahi kuweka wazi sababu za kuachana kwao zaidi ya tetesi ambazo hazina uthibitisho kutoa kwao wenyewe.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.