Loading…

‘Vannessa hata akitembea na mtu barabarani ni mtu wake’-JUX

September 11, 2017 at 21:38
'Vannessa hata akitembea na mtu barabarani ni mtu wake'-JUX

Tukirudi katika kumbukumbu vannesa mdee na juma jux walikuwa ni moja kati ya couple pendwa na ya kupendeza hata jwa kuiangalia kwa picha za mitandaoni huku wawili hao walikuwa wakionekana wapo katika mahaba mazito kabisa.lakini hali ilikuja kubadilika baada ya ibirisi kuingulia mapenzi ya wawili hao na mapenzi yao mazito kukoma.Na hivi karibuni kumekuwa na uvumi mitandaoni kuhusu mahusiano mapya ya msanii vannesa mdee na mtu  mwingine maarufu kutoka katika kundi kubwa na maarufu la Wcb wasafi ingawa msanii huyo mpaka sasa bado hajajulikana wazi kuwa ni nani ,jux mpenzi wa zamani wa vannessa mdee nae amezungumzia ilo.

Alipokuwa akiongea  na mtangazaji wa Ayo Tv usiku wa  tarehe 9 septemba katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume mkoani Arusha katika uzinduzi wa tamasha la fiesta, jux  amesema kuwa kwa sasahivi kila mtu ataongea lake na kila atakaeonekana kuongozana na vannessa basi ataonekana  anatembea nae”kila mtu atakaeonekana na vee utaaambiwa hivyo,leo itakuwa huyu,kesho huyo..” alisema jux. hata hivyo alipoendelea kuulizwa alisema kuwa hawezi kuliongelea swala ilo kiundani labda aliongelee vannessa mwenyewe.

Loading...

Jux aliyekuwa akionekana anajibu kwa wasiwasi kidogo kuhusu tuhuma hizo  na alikuwa akikataa katukatu kuendelea kuuliza maswali  kuhusu mahusiano ya vannesa huku akimtaka mtangazaji kumuuliza maswali hayo mhusika ambae ni vannnesa.na hata alipotakwa kuuliza swali lolote la kimziki kwa vannessa alishindwa na alikataa kabisa kuchimbwa kiundani kuhusu mpenzi wake huyo wa zamani.

jux na vannessa walikuwa katika mahusiano mazito ya kimapenzi na hata baada ya kuachana kumekuwa na utata mkubwa wa nani atasema ukweli na kufunguka kuhusu sababu kubwa ya kuachana kwao,huku kila mmoja kwa nafasi yake akionekana kukiri kuwa bado anampenda mwenzio.

katika interview hiyo pia Jux alitoa taarifa tena kuhusu kubomolewa kwa duka lake la nguo lenye brand ya ‘African boy’ ila amewahakikishia wateja wake kurudi kwa duka hilo hivi karibuni maana pameshapatikana mahali pengine,ivyo wateja wakae mkao wa kula.

Comments

  1. JUX ni mpole sana ila Mdee nafeel bado hajatulia

  2. fungeni ndoa basi,mda ni moshi haungoji yeyote

  3. Vanessa Mdee,ningekua wewe ningeolewa na Juma Jux tayari,ni mkaka mature sana

  4. Pole sana,hzo bomoa bomoa zimeleta hasara JPM wananchi wanaumizwa sana

  5. huwa ninamkubali sana Vanessa mdee kwa kweli yuko simple

  6. I love u Jux Can’t get enough of u

  7. Nakupenda hadi mtoto wangu anakupenda

  8. mm napenda muwe pamoja maana mnapendezana Sana

  9. Nakubalee sana broo

  10. Juma jux…mashaallah MTU mwenye swaggz zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.