Viongozi Wa Dini Walimshauri Shiloleh Ndoa Ya Kimyakimya

December 15, 2017 at 09:36
Viongozi Wa Dini Walimshauri Shiloleh Ndoa Ya Kimyakimya

Msanii wa muziki wa bingo fleva nchini zuwena mohamed maarufu kama shiloleh amefunguka na kusema kuwa kufunga ndoa ya kimya kimya alishauriwa na viongozi wa dini na ndio maana ndoa yake ilikuwa haijatangazwa ingawa watu walikuwa wakijua kuwa atafungua ndoa.Lakini pia shilole anasema kuwa upinzani alioupata kutoka kwa dada yake ambae hakutegemea kwa sababu alikuwa mtu wa karibu nae ulimfanya kufunga ndoa kwa haraka zaidi.

Shiloleh alisema kuwa viongozi wa dini walimshauri kuwa ndoa haitangazwi kwa sababu kuna watu wanaweza kuwafanya kubadilisha maamuzi yenu na mkashangaa ndoa ikabadilika na ikashindwa kufanyika kabisa.

Loading...

Niliambiwa kuwa sio kila mtu anapenda kusikia jambo jema hilo, wengine wanaweza  kukufanyia husda ili jambo lako jema lisifanikiwe  kwaio nikaamua kuwasikiliza lakini sio kwamba sitafanya sherehe. –Alifunguk Shiloleh

Akiongelea swala la dada yake kumkataza kufunga ndoa na mwanaume wa ndoto zake shilole anasema kuwa

Unajua haya mambo ni ya kifamilia, lakini mimi ninawatoto wawili kwaio hawezi kunipangia  mwanaume wakuolewa nae. Alisema Shishi baby.

Hata hivyo shiloleh anasema kuwa pamoja na kwamba ndoa ilifanyika kimya kimya lakini anatehemea kufanya sherehe kubwa itakayo kata na shoka na wale watu wake wa karibu wote watahudhuria na kufahia sherehe hiyo ambayo amehaidi kutangaza hivi karibuni huku ikisemekana kuwa sherehe ya ndoa hiyo itafanyika December 25 mwaka huu.

shilole alifunga ndoa na Uchebe , mwanaume ambae inasemekana pia kuwa alimuacha mke wake kwa ajili ya shiloleh na kuamua kumpa talaka mwanamke aliyekuwa nae kwa kipindi hicho.Hata hivyo mapenzi yao yamedumu mpaka sasa wameamua kufunga ndoa.

 

 

Leave a Reply

avatar

in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.