Vyakula Vinavyoweza Kutunza Urembo Wako

ASALI.

download latest music    

Asali husaidia kutunza unyevunyevu katika ngozi, na pia ina kiwango kikubwa cha  sukrai na asidi amabyo uweza kuzuia  vijidudu ambavy vianweza kuathiri ngozi yako.Hutengenezwa na nyuki waliokusanya viambata vingi vya asili kutoka katika mimea mbalimbali.

MAYAI.

Mayai pia ni mazuri kwa afya ya ngozi,kiini chake huwa na vitamini A na B,Ilhali ute wake mweupe una protini nyingi sana ambazo huwa ni nzuri kwa afya ya ngozi.husaidia ngozi kuwa nyororona yenye kungaa zaidi.pia inasaidia ngozi kujikinga na mionzi ya jua.

MATUNDA.

Matunda hususani machungwa na malimao,matunda haya utengeneza collagen kwa ngozi ya mwili wa binadamu ambayo husaidia  katika utengenezaji wa ngozi.

Vitamins hivi husaidia sana katika kuondoa mikunjo na vivimbe katika ngozi za mwanadamu.

MBOGA ZA MAJANI.

Mboga za majaini husaidia sana sio kwa ngozi tu bali kwa mwili wote kwa ujumla kwa sababu vinakuwa vimesheheni virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini.Mboga za majani zina virutubisho vyenye kusaidia kuondoa seli zilizokufa na kuzalisha seli mpya katika ngozi.

VYAKULA VYA BAHARINI.

Vyakula vya baharini vingi vina Zinc na Omega 3 ambazo  ni muhimu kwa siha ya ngozi.Omega 3 husaidia kukakamaa kwa ngozi na ukavu wa ngozi yako, kupunguza uvimbe na kukunjamana kwa ngozi.Lakini pia inasaidia kufanya mzunguko wa damu uwende vizuri ivyo kuleta ngozi nzuri.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.