Wafahamu Wanamitindo Watanzania Matajiri Nchi za Nje

Inawezekana umewahi kusikia tu kwa juu juu kuhusu wamamitindo kutoka Tanzania wenye fedha nyingi na wanaomiliki vitu vya thamani  na wanafanya vizuri wakiwa nje ya Tanzania,  kutokana na kazi zao za uanamitindo  wakina dada hawa wameweza kufanikiwa sana hata wengine kukumbuka fadhila na kuamua kurudi na kusaidia zaid nchini kwao Tanzania.Basi hawa hapa ni top five ya models bora kabisa wa kike wenye wadhifa wao kubwa nchi mbalimbali .

1.Miriam Odemba

download latest music    

Aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2008 akitokea Temeke,nafasi ambayo ilimfanya aendelee mbele   zaidi na kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Africa na baadae mshindi wa tatu katika M-net Face Of Africa.Kwa sasa anaishi Paris Ufaransa akifanya kazi zake kama model wa kujitegemea.Ameshawahi kufanya kazi na Kante West, Kim Kardashian na Chriss Jener.

2.Happiness Millen Magesse

Alishawahi kuwa miss tanzania mwaka 2001, lakini kwa sasa ana makazi yake Afrika ya Kusini na Marekani.Happy alishwahi kupata tuzo ya BET Global Group kutokana na juhudi zake za kusambaza elimu ya uelewa juu ya ugonjwa wa Endomitrisis, ugonjwa ambao hata yeye ulimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya achelewe kupata mtoto.Amefanya kazi katika nchi mbalimbali ikiwemo Paris,London, Newyork  na Johensburg.Mwaka huu happiness alifanikiwa kupata mtoto wake wa kwanza wa kiume.

3.Flaviana Matata

Flaviana alizaliwa mwaka 1988 mkoani shinyaga, amelelewa zaidi na baba yake baada ya mama yake kufariki katika ajali ya Mv Bukoba(1999) , alishawahi kushinda Miss Universe 2007, hii ikawa ni kama njia ya mafanikio kwake.alishawahi kufanya kazi na mashirika mbalimbali kama aAlexandria McQueen, na Tommy Hilfger.Lakini pia amekuwa akijipatia fedha kwa kutokea katika majarida mbalimbali ikiwepo la Marie Claire.Kwa sasa Flaviana ana brand kubwa ya rangi za kucha inayojulikana kama LAVY.Flaviana pia anatoa misaada katika jamii chini ya Flaviana Matata Foundation katika elimu.Flavy ameolewa mwaka 2016.

4.Tausi Likokola

Alizaliwa Tanzania lakini kazi zake nyingi amekuwa akifanyia Marekani na Ujerumani,ameshafanya kazi na mashirika makubwa ya orodha A ikiwemo Tommy Hilfger, Gucci, Eskada na Christian Dior.Ukiachana na urembo Tausi amekuwa akitoa misaada kwa  watu wasiojiweza chini ya Tausi Aids Funds katika elimu na afya.Tausi ni mwandishi wa vitabu na pia ni Motivational speaker katika sehemu mbalimbali.kwa sasa amejikita kusaidia walimbwende wachanga waweze kuinuka.

5.Herieth Paul

Huyu ni mwanamitindo mdogo kabisa aliwahi kufanikiwa katika kazi yake, Herieth alizaliwa mwaka 1995 nchini Tanzania,baadae familia yake ilihamia Canada.Heriet alishafanya kazi na makampuni mbalimbali ikiwemo Lacoste.kwa sasa anafanya kazi chini ya kampuni ya Women Manegement  ya nchini Newyork .Mwaka 2016 alishinda tuzo ya Canadian Super Model. Katika moja ya mafanikio makubwa ya Herieth ni kufanya kazi katika show ya Victoria Secret nchini Ufaransa akiwa pamoja na Kendal Kardashian, ikisemekana kuwa ni moja ya show aliyolipwa fedha nyingi sana zaidi ya billion moja.Yeye pia ni mwanamitindo mdogo mtanzania anaeishi Marekani katika nyumba aliyonunua mwenyewe.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.