Wakili wa Sheikh Mbonde Afunguka, Babu Tale Anaweza Kukaa Mahabusu Kwa Muda Usiojulikna

Wakili wa Sheikh Mbonde amefunguka na kusema kuwa inawezekana kabisa meneja wa Tip Top connection Babu Tale akakaa rumande kwa muda usiojulikana kutokana na kushindwa kufikia kwa muafaka kati  yao hasa baaada ya alitoa amri ya kukamatwa kwake kutokuwepo mahakamani hapo.

Akielezea hali ilivyokuwa, wakili huyo alisema kuwa hata baada ya kukaidi amri ya mahakama kwa muda mrefu,Babu Tale alipofikishwa mahkamani alipewa muda wa kuyazungumza madai hayo na aliyemshitaki lakini walishindwa kuelewana na ndipo hakimu aliposema Babu Tale anapaswa kumsubiri naibu msajili wa mahakama kuu atakaporejea kutoka safari.

download latest music    

Katika kesi hiyo, wakili huyo anahadithia kuwa babu tale na Sheikh Mbonde walikubaliana  kurekosi masomo ya kiislamu na kisha kuauza kwa jamii lakini baadae  Babu Tale alimkatia mawasiliano Sheikh huyo na kumwambia kuwa amhairisha kufany kazi hiyo hivyo atafute mtu mwingine wa kufanya hivyo.

Hata hivyo Sheikh Mbonde alipokwendaDodoma alikutana na video hizo aina ya DVD baadhi ya sehemu zikiwa zinauzwa  ndipo alipomua kufikisha swala hilo mahakamani.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.