Wako Wapi Wasanii Walioumizwa na Kifo cha Akwilina Akwilini

Ikiwa jana ndio siku ambayo mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji kuagwa mwili wake na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao kwa ajili ya mazishi watu wengine wameonekana kusikitishwa na kuhoji wako wapi wale wasanii ambao walipata mshtuko mkubwa siku ya tukio.

Mategemeo makubwa ya mashabiki ilikwa  ni kuona wingi wa wasanii katika kuaga mwili huo siku ya jana ikiwa siku ya kifo chake wengi walionekana kuguswa lakini kitu cha ajabu  wasanii waliojitokeza ni wachache tena wanahesabika.

download latest music    

Acha tuone sababu, je ni kweli wasanii hao waliguswa na msiba lakini kila mtu alikuwa busy na shughuli zake akashindwa kutoa heshima za mwisho kwa mwanafunzi huyo ambae kifo chake kimeumiza watu wengi.

Je ni kweli kuwa wasanii walishindwa kujua kuwa jamii ya wanafunzi wa chuo pia ni  jamii kubwa inayosikiliza muziki wao hivyo kutokea katika msiba kungewafariji wafiwa na wanafunzi lakini pia kungewafanya wanafunzi na wafiwa kuona kuwa hata wao pia  sehemu ya maisha ya wasanii.

Je uwepo wao katika msiba na kuagwa kwa mwili huo sio kuwa ndio fursa ya wasanii kukutana na mashabiki wao hata kama wapo katika hali ya uzuni.

Yako wapi yale majonzi waliyokuwa nayo wasanii hao katika page zao za instagram siku mwanadada huyo anapoteza maisha.

Hapa tunajifunza kuwa wasanii wengi wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii katika kuonyesha hayo yote lakini wanashindwa kutambua kuwa mashabiki wao pia wanawahitaji sana katika kujumuika nao katika matatizo kama hayo.

Hata hivyo, wapo waliojitokeza  kama Bilnass ambae alionekana kwenye misiba na akapata nafasi ya kuongelea masikitiko yake juu ya msiba huo na kusema “kazi ya mungu haina makosa, kikubwa ni kumuombea tu.natoa pole kwa wanafamilia, wanafunzi na wafiwa wote kwa ujumla.

Mwisho wa yote tunatoa pole kwa wafiwa  hasa ndugu wa marehemu na Mungu awatie moyo katika kipindi hiki kigumu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.