Waliozoea Kuvaa Vichupi Sasa Basi,JPM Kula Nao Sahani Moja

Jana katika kikao cha wazazi CCM kilichofanyika mkoani Dodoma , Mh. Raisi Magufuli aliongea na wazazi kuhusu maadili ya wasanii hasa wa kike ambao wamekuwa wakivaa nguo fupi na kuwaacha miili yao wazi.Raisi Magufuli amesema kuwa amekuwa akishangazwa sana pale anapowasha tv na kuona wanaume wakiwa wamevaa vizuri lakini jinsia ya kike wakiwa uchi kabisa na ni kitu ambacho akimpendezi kabisa.

M. Raisi amesema kuwa anazitaka maamlaka husika hasa TCRA, kuwachukulia hatua wote ambao wamekuwa wakipiga picha za utupu  na kutupia katika mitandao ya kijamii na kama wanataka kukaa uchi basi wakae huku huko katika club lakini sio kuwka katika mitandao.

download latest music    

Mh Raisi alisema kuwa ni aibu kwa wazazi kuangalia katika televisheni watoto hasa wa kike wakiwa uchi na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na mamlaka husika.

Baadhi ya maadili yameanza kupotea na nyinyi wazazi , na mmeshindwa kuyakemea , unapofungulia muziki  ukitaka kuwaona wanaocheza utakuwa ni wanawake tu ndo wako uchi,lakini wanaume hapana baadhi ya wanawake wanaachia viungo vyao.

kwanini uwavulie hata wasiotaka kuoona huo uchi,tena kwa wakati ambao sio muafaka ,nyie kama jumuiya ya wazazi inafika wakati inapaswa  kuyakemea haya , tunaelekea wapi sasa?tunawafundisha nini watoto?kwani akicheza amevaa nguo hatafurahisha?

vyombo vyetu vya habari viko wapi, vyombo vinavyosiamamia hayao wako wapi,je TCRA ambao wana mamlaka ya kufungia hata vyombo vya habari ambavyo vinarusha video za utupu iko wapi?

Ujumbe huu wa mh raisi unaenda moja kwa moja kwa wasanii wengi tanzania hasa wa kike ambao wamekuwa na tabia hii ya kuvaa nguo zinazoonyesha utupu wao, Gigy Money, Sanchoka,Amber Lulu, Pretty kindy , Kidoa na wengine wengi.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.