Wanaonyoa Kiduku Kusakwa na Polisi,Je hii Itahusu Wasanii.

Ilianza kwa kuwafungua wasanii hasa wa kike wanaovaa vibaya ili kulinda maadili ya taifa na wale wote wanaochapisha picha za utupu mitandaoni.zoezi limegeukia upande wa pili na sasa ni watu wote wanaonyoa mtindo unaojulikana kama kiduku ambao mtu hunyoa nywele za pembenina kuacha zilizopo katikati.

katika moja ya magezo yanayotoka kila siku, gazeti la nipashe ya leo imeweka habari kuwa mapolisi jijini dar es salaam wameanza kamata kamata ya vijana wote wanaonyoa style ya nywele inayojulikana kama kiduku na kuweka ndani mara moja.Msako huu utawahusu watu waote wanaonyoa hivyo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kutunza na kulinda maadili ya Taifa.Baada ya kufanya uchunguzi gazeti hilo limebaini kuwa vijana hao wanakamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kuvunja maadili ya kitanzania.

download latest music    

swala la kujiuliza ni kwamba je kamata kamata hii inahusu vijana wa mitanai tu au hata wasanii wengi ambao sasa hivi style hii ya nywele imeshakuwa ni kama ya kawaida kwao.Na kama ukamataji huu unamhusu kila kijana mtanzania basi kamata kamata hii itakuwa inawahusu wasanii wengi wakubwa na wadogo wakiwemo Diamond Platinumz.

Ingawa bado haijabainika tamko la kukamtwa kwa vijana wanaonyoa viduku limetoka wapi lakini,lengo kubwa ni kulinda maadili ya TaIfa ingawa pia watu wengi katika mitandao wameonyeshwa kukerwa na ukamataji huo wa vijana.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.