Wanasema Anaumwa Kwa Ajili Yangu, Sijawahi Sikia Ugonjwa wa Mapenzi :-Uwoya

Mwanadada Irene uwoya amejikuta akimwaga povu katika baadhi ya mahojiano yake na station mbalimbli hasa wanapotaka kila mara kumuuliza kuhusu mahusiano yake na msanii dogo janja aliefunga nae ndo mapema mwaka huu na kusemekana kuwa ndoa hiyo kwa sasa imeota mbawa.

download latest music    

Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu wawili hao huku ikisemekana kuwa  ndoa ya wawili hao imevunjika kwa sababu irene amepta mwanamue miwngine mwenye pesa kumzidi Dogo janja na ndio maana kumekuwa na kutokuelewana kwao.

Hata hivyo ,Dogo janja aliwahi kulazwa hospitali na kusemwa kuwa sababu kubwa na msanii huyo kulazwa na kutokana na stress zinazotokana na kuumizwa na mapenzi, akijibu swali hilo Irene anasema ‘

wanasema kuwa anaumwa kwa sababu yangu, basi hayo ni makubwa .sijawahi kusikia mtu ana umwa ugonjwa wa mapenzi, ina maana mimi ndo huwa natesa watu je mimi huwa siteswi, maana kila mtu uwoya uwoya… ina maana kila siku katika mapenzi mimi ndio  natesa watu, ina maaana mimi ni tesatesa au mimi chinjachinja wa mapenzi.

Ni kweli kuwa mimi ni mkali lakini huyo mwanaume atakuwa na ugonjwa wake miwngine tu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.