Wanawake Wengi Wananitaka Kimapenzi- Emmanuel Mbasha

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha na aliyekuwa mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Flora Mbasha, amekiri kuwa amekuwa akisumbuliwa sana na wanawake wanaomtaka kimapenzi.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa Emmanuel Mbasha amekiri kuwa amekuwa akipata usumbufu huo hasa kupitia kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.

download latest music    

Kwenye kipindi cha Enews Mbasha alifunguka;

“Unajua watu wakiona umempost msichana kwenye page yako wanaamini ni mpenzi wako lakini sio kweli wengi wao no mashabiki tu nakutana nao wanaomba wapige picha na mimi basi ila kwa sasa sina mpenzi sina mke nipo tu mwenyewe na mambo yangu ila itakapofika wakati sahihi na ninaamini binti niyakayempata atakuwa ameletwa na Mungu hivyo sina sababu ya kukurupuka kwa sasa nimetulia nasubiria make sahihi, unajua nimetokea kwenye ndoa iliyokuwa na changamoto kubwa sana angepitia mtu mwingine angedata lakini mimi nashukuru nilisimama na Mungu nikamuomba anivushe salama na nashukuru nimevuka sasa sina sababu ya kuharakisha mambo kwa sasa”.

Pia Mbasha aliendelea kufunguka kuhusu changamoto anayopata kutoka kwa wanawake;

“Unajua wadada wengi wananipenda wa kila aina wote wanataka kuwa na mimi yaani nikikuonyesha meseji zangu wanazonitumia za kunitaka zimejaa kibao kwenye mitandao yote facebook, instagram kote huko lakini namshukuru Mungu kwakibali hicho maana kupendwa nako ni kibali jambo ambalo lipo wazi, Kwa sasa siwezi kukurupuka tu nikamchukua yoyote nisije nikaingia kwenye majanga namuomba Mungu anioneshe mwanamke mwema”.

Mbasha pia amekiri kuwa usumbufu huo anaopata kutoka kwa wanawake wengi ameuzoea kwani tangu kipindi  ameoa amekuwa akipata usumbufu huo huo kutoka kwao. Mbasha ameweka wazi hayo baada ya tetesi kuenea kuwa ana mpango wa kuoa hivi karibuni mara tu baada ya aliyekuwa mke wake Florah kuolewa tena.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.