Wasanii ni Wanafiki Wanasubiri Kutoa Pole Badala Ya Kusaidia”- Steve Nyerere

Msanii wa Bongo movie na komedian maarufu Steve Nyerere amefunguka na kutaka Wasanii Wenzake waache unafiki na kupaaza sauti sasa ili Soudy Brown na Maua Sama waweze kuachwa huru.

Maua Sama na Soudy Brown wamewekwa  ndani tangu siku ya Ijumaa mpaka leo hawajapata dhamana baada ya kuposti video clip iliyowaonyesha kundi la watu wakicheza wimbo wa Iokote wa Maua Sama huku wakirusha pesa na kuzikanyaga.

download latest music    

Steve Nyerere amewatolea povu wasanii Wenzake na kuwataka wajitoe kuwasaidia wasanii wenzao katika kipindi hiki cha shida badala ya kukaa kimya halafu kuja kutoa pole wakija kutoka hapo baadae.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve Nyerere amemwaga povu hili:

Sisi wasanii ni waoga na wanafiki, limeanza kuhusishwa sijui kuna ugomvi na RC Makonda hawa wamekosea, sio wakitoka ndio tuanze kutoa pole, Ndio nilipanga kufanya hivi, Hapana muda ndio huu tuombe radhi kwa serikali vijana wetu wapewe dhamana”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.