Wasanii Wamshauri Lulu Kukaa Jela Atumikie Kifungo Chake.

Sio muda mrefu umepita tangu mwanadada wa bongo movies Lulu Michael kuhukumuiwa jela kwa miaka miwili jela ili kutumikia kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia  kwa msanii mwenzie  Steven Kanumba mwaka 2012.Baadhi ya wasanii katika tasnia ya muziki na filamu wameibuka na kuongea katika nyakati tofauti tofauti ushauri wao kwa msanii huyo kuhusu swala la yeye kukata rufaa.

Hata hivyo  wasanii wanaonekana kumuhurumia msanii huyo lakini  bado wanamshauri kuwa ni bora zaidi akatumikia kifungo chake chote na kumaliza kuliko kukata rufaa.Na kwa sababu kukata rufaa bila kujua hatma yako ni sawa na kukaa kifungoni bil kujua adhabu itaisha lini.

download latest music    

Lulu Diva.

Nikipata nafasi ya  kumshauri au kuzungumza na lulu  ningemshauri bora tu atumikie kifungo chake na akimalize tu  ili awe huru.ana kila sababu ya kutumikia kifungo icho ili kuupoza  machungu ya mashabiki wa kanumba na familia yake pia.baadhi ya watu wamekuwa na mtazamo tofauti baada ya kifo hicho kuhusu yeye.

Snura:

Japo uwezekana wa  kukata rufaa inawezekana ila mimi ninamshauri sana amuachie Mungu tu  kwa kila jambao na anaejua kesho yake ni Mungu pekee.

Sandra.

Wala hasikate rufaa kwakweli kwasababu kesi ya mauaji ni kesi kubwa sana,na hata kama ataamua kukata rufaa ni mlorongo mrefu sana atapitia mpaka afanikiwe kile anachokitaka  na uwezekano wa kutokufanikiwa kwa rufaa yake ni mkubwa sana .Ni bora tu atumikie kifungo chake ili akimaliza awe huru na maisha yake mapya baada ya kifungo.

Davina;

Asikate tamaa maana kuna watu wanaona kabisa alilofanya kuwa ni kosa, hivyo ni bora zaidi akatumikia kifungo chake  kwa hiyo miaka miwili tu na baada ya hapo awe huru  na maisha yake ya kawaida yaendele kama mungu alivyopanga kuyasimamia.wala asikate ili mambo yaishe na atengenze usawa kwa watu.

Mlela.

Mimi ninamshauri tu  akabiliane na jaribu hilo ili awe huru.japokuwa jela sio mahali pazuri lakini midomo ya watu na maneno ya watu ni mabaya na yanakera zaidi .Kila linatolotokea kwa binadamu ni mungu ndie anapanga litokee na atampitisha ili awe kufika pale anapopataka yeye.

Pretty kindy:

Ni bora tu akatumikia kifungo chake, maana kwakweli baadhi ya mitazamo ya watu  katika jambo ilo ni tofauti sana.Amalize kifungo chake ili akimaliza kifungo  hakuna mtu hatakuwa na kinyongo na yeye tena.

Mary Mawigi:

Kwa upande wangu mimi naona bora tu amuombe mungu  amfanyie wepesi tu mbona miezi 18 tu.asikate tamaa  mungu yu pamoja nae.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.