Wastara Atamani Kifo Baada Ya Kupatwa na Majanga

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka na kuweka wazi kuwa anapitia kipindi kigumu sana kiasi ya kwamba alitaka kujiua Baada ya kuibiwa kila kitu siku za Hivi karibuni.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wastara ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la mguu wake wa kulia kwa muda mrefu baada ya kukatwa, bado amekuwa akipambana kujikimu kimaisha kupitia filamu lakini juzikati watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwake, Sinza-Kwa Remmy jijini Dar na kumuibia vifaa vyote vya ‘production’ pamoja na vitu vingine.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Wastara alifunguka juu ya majanga yaliyomkuta huku akisema kuwa, imefika wakati anatamani asiwepo duniani:

Napita kwenye wakati mgumu sana jamani, kila likitoka hili, linaingia lingine, natamani hata nijiue. Ni kweli juzi nimeibiwa vifaa vyangu ninavyotumia kuzalishia filamu na vipindi vya TV, vifaa vina thamani kama ya milioni tisa hivi.

Sielewi naanzia wapi, hapa nilipo nina kazi za watu ambazo zilikuwa kwenye ‘external’, nililetewa kwa ajili ya kuwafanyia kazi, wamechukua, kuna vipindi vya TV ambavyo nilikuwa nikivifanya kwa sasa sijui nitarekodi vipi tena, nimechanganyikiwa, natamani niondoke kwenye mgongo wa ardhi”.

Lakini pia Wastara ameweka wazi kuwa ameshawashirisha polisi juu ya janga hilo na anaamini ulikuwa ni mchongo wa ndani:

Ishu iko polisi, washukiwa wawili ambao ni mlinzi na kijana mmoja ambaye ananisaidia kazi zangu walikamatwa na kuwekwa ndani kwa siku nne. Yaani kikubwa nipate hata kamera yangu ya kazi maana nafikiria tena mambo ya kukodi kamera, sijui itakuwaje”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.