Watanzania Kuwania Tuzo za Soundy City Nigeria, Diamond aongoza.

Tuzo za Soundy city awards nchini nigria imetoa majina lukuki ya wasanii watakao wania tuzo hioz kwa mwaka 2019, wakati huo wakitoa idad iyo ya wasanii jambo la kufurahisha ni kwamba kwa Tanzania muziki unazidi kukua na wasanii wanazidi kujulikana nje ya nchi.

Diamond Platnumz atawala nominations nchini Nigeria katika tuzo za Sound City Awards 2019 kwa jina lake kuonekana Mara 11 kwenye vipengele tofauti akiwa single na vya kushirikishwa. Diamond ametajwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kiume wa mwaka, digital artist wa mwaka, msanii bora wa pop, msanii bora wa mwaka, etc. Maua Sama anawania msanii bora wa kike wa mwaka Africa akichuana na kina Tiwa Savage na Yemi Alade, .

download latest music    

Vanessa Mdee anawania digital artist of the year pamoja na kina Davido, Diamond, Wizikid, Yemi Alade, Kwangaru ya Harmonize na African Beauty wa Diamond wanawania wimbo bora wa mwaka. Harmonize na boss wake Diamond wote wanachuana kutwaa msanii bora wa kiume Africa. Mboso anawania msanii bora mpya Africa

Kenya imepata nominations kupitia Sauti Sol, Kalgraph Jones , ambapo kwa upande wa mwaka 2018, khaligraphs jones amekuwa moja ya wasanii waliongoza sana Kenya kushinda tuzo mbalimbali ndani na nje ya kenya.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa mwakani huku tegemea kkubwa la wasanii hawa ni kura kutoka kwa mashabiki wenyewe.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.