Loading...

Watanzania Wanapenda Sana Mapenzi Kuliko Kula- Queen Darleen

December 06, 2018 at 09:03
Watanzania Wanapenda Sana Mapenzi Kuliko Kula- Queen Darleen

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Queen Darleen ameibuka na kuweka wazi sababu za kupendelea kuimba nyimbo za mapenzi.

Queen Darleen amesema anapenda sana kuimba nyimbo za mapenzi kwa sababu Watanzania wanapenda sana mapenzi kuliko kula kwaiyo nyimbo za mapenzi zimekuwa na soko zaidi Bongo.

Loading...

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Queen Darleen ameweka wazi kuwa wasanii wengi Bongo soko lao lipo kwenye nyimbo za mapenzi ndio maana hata ukiangalia nyimbo hizo ndizo zinafanya vizuri zaidi.

Unajua Watanzania wanapenda sana Mapenzi kuliko kula kuliko hata kufanya kazi ndio maana nyimbo za mapenzi zinafanya vizuri zaidi kwenye Bongo fleva na ndio maana wakina Mbosso, Lavalva wanafanya vizuri na Diamond Mpaka leo yupo kwenye chati kisa nyimbo za mapenzi “.

Queen Darleen amesema anatamani Label ya WCB isaini Msanii wa kike ili yeye apate chagamoto ya kufanya kazi nzuri zaidi.

 

4
Leave a Reply

avatar
4 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
4 Comment authors
YasminLeilaLoviKunta Recent comment authors
newest oldest most voted
Kunta
Guest
Kunta

Msaini Nandy

Lovi
Guest
Lovi

Tafadhali mkikata chukua msanii wa kike mchukueni Amber Lulu manake mziki wake nautambua sana

Leila
Guest
Leila

Si uwongo watanzania wanapenda sana mapenzi

Yasmin
Guest
Yasmin

Sasa basi mtaimba nini kingine cha maana


in Entertainment

Loading…

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.