Wazazi Wa Nandy Wafungukia Video Ya Utupu Ya Nandy

Wazazi wa Msanii wa Bongo fleva Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy wamefunguka na kuiongelea video ya utupu ya Nandy ambayo ilivujishwa mwaka jana kwenye Mitandao ya kijamii.

Baba mzazi wa Nandy amefunguka na kusema video hiyo ya binti yao iliwatia aibu sana kama Familia kiasi cha kumtaka Nandy aachane kabisa na kufanya muziki.

download latest music    

Katika interview aliyofanya Baba Nandy alisema kwamba siku iliyovuja video hiyo alikuwa akipigiwa simu kila dakika kumlaumu kwa kitendo chake cha kumuacha mtoto afanye sanaa, licha ya ndugu zake wengi kutofurahishwa na suala hilo.

Nilikuwa ofisini kwangu napigiwa simu nyingi nyingi wananilaumu vipi mtoto, yaani kama vile kitendo alichokifanya Nandy ni kama nimekifanya mimi, kwa jinsi wanavyotoa shutuma, nikawa najiuliza kumetokea nini, katika kuchunguza ndio nikaambiwa, mimi sijaiona hiyo picha, niliambiwa tu, nilichokifanya nikasema huu ndio mwisho wa huyu mtoto, mwisho wake wa kuimba umefika, sababu yale niliyokuwa nayaogopa naona yameshakuja”.

Lakini pia Mama mzazi wa Nandy amesema kwamba tukio lile lilimpa wakati mgumu, kwani alishindwa hata kula na kumfanya akae njaa kwa siku tatu, na kusema kwamba iwapo atarudia kufanya vile basi huenda akapoteza maisha kabisa.

Nilikuwa sipokei simu kwa sababu nilikuwa najua nitakachoulizwa, nilikosa raha nilikaa siku tatu sijala kitu zaidi ya kunywa chai tu, alipokuja kuona alizimia akashtuka yuko hospitali, lakini ni mateso, sikufichi ni mateso, Nandy siku akirudia naweza nikafa kabisa”.

Mwaka jana video iliyomuonyesha Nandy na Mpenzi Wake kwa wakati ule Billnas wakiwa chumbani faragha kabisa ilivuja kwenye Mitandao ya kijamii na kuzua kizaazaa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.