Waziri Mkuu Atangaza Adhabu Mpya Kwa Wanaowapa Mimba Wanafunzi

Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametangaza vita kali dhidi ya wanaume Ambao watakutwa na hatia ya kuwapa Mimba wasichana wenye umri mdogo na kusababisha kuwakatisha masomo.

Waziri amesema kuwa kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana jumla ya wanafunzi wa kike 57 walikatishwa masomo baada ya kupata mimba na hadi sasa kesi zilizofunguliwa ni sita tu, ambapo ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha wahusika wote wanakamatwa.

download latest music    

Waziri Mkuu aliyasema hayo Februari 24, 2019) alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Isanja, Sanya Juu wilayani Siha wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro.

Jambo hili halipendezi, kesi sita tu ndio zimefikishwa mahakamani. Hakikisheni wahusika wote waliowapa mimba wanafunzi wanatafutwa popote walipo, wakamatwe na wachukuliwe hatua kali za kisheria.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo.

Watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na Serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.

Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenu vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela, sasa tafakari kabla ya kutenda.”

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.