Waziri Mwakyembe Amtembelea Wastara na Kutoa Msaada wa Matibabu.

Waziri wa sanaa , habari na michezo Mh.Harison Mwakyembe amekwenda kumtembelea msanii wa bongo movies Wastara Juma nyumbani kwake na kumjulia hali lakini pia ameweza kumsaidia kutoa shilingi mil.1 kwa ajili ya kuchangia fedha za matitabu zinazotakiwa kwa mwanadada huyo kwenda India kwa ajili ya matibabu yake. Mh.Waziri mwakyembe ambae aliambata na  katibu wa bodi ya filamu  walifika mpaka nyumbani kwake kwa ajili ya kumjulia hali msanii huyo.

Hata hivyo Waziri Mwakyembe amewaomba wasanii wote nchini kuwa na moyo wa kujitolea na kumsaidia Wastara Juma ambae anahitaji mili37 kwa ajili ya kurudi katika hospitali aliyokuwa akitibiwa hapo mwanzo kwa ajili ya kubadilishiwa baaadhi ya vifaa mwilini mwake vinavyomfaya aweze kutembea vizuri lakini pia  kuondoa maumivu makali anayokuwa anayapata kwa sasa maeneo ya mgongoni kwa muda mrefu na kusabaisha kuzimia kwa muda kutokana na maumivu hayo.

download latest music    

Uwepo wa Mh,Waziri nyumbani kwa Wastara kuna kuja baada ya msanii huyo kuamua kufunguka katika vyombo vya habari kuhusu hali yake hiyo baada ya kupata ajali ya pikipiki miaka kama  minne iliyopita na kumsababisha kukatwa mguu na ndipo alipowekewa mguu wa bandia ambao unahitaji kuhudhuria kliniki mara kwa mara lakini awamu hii alishindwa kurudi kutokana  na kushindwa kupata fedha za kumrudisha hospitalini huko.

Alipokuwa akiuulizwa kuhusu muamko wa watu na wasanii wenzake katika kuchangia  msaada huo , Wastara alisema anashukuru watanzania  wote ambao wamekuwa na moyo wa kujitolea kwa sababu wa sasa msaada wake unatoka mikononi mwa watu ingawa bado muamko wa wasanii wenzake unakuwa mdogo.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.